Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Ujamaa ni nadharia tu ni ngumu kuwa hali halisi, utumika kama fimbo tools ya kuwafanya wananchi wawe masikini ili iwe rahisi kuwatawala ( inferiority complex) hali ya kutokujiamini kwa mtawala wao wanaamini ni rahisi kumtawala masikini mwenye njaa hiii ni kweli hata sisi tunawapa ujira Mdogo sana watufanyiao Kazi na wao ufanya tu sababu ni masikini. Nyerere na viongozi wote awakuishi ujamaa yaani kuwa sawa na waliowataka wawe sawa mfano atuoni popote kama waliwahi pigia meno mkaa,vaa Viatu vya tairi km vile vya kimasai,kunywa uji Bila sukari,kufulia majani ya mpapai kwa kukosa sabuni,kupanga foleni maduka ya ushirika,kushona viraka,nk.Viongozi wote wa kijamaa duniani uishi maisha ya kitajiri tofauti na wanaowaongoza.
 
Siyo kweli, maisha kabla ya vita hayakuwa mazuri. Uchumi ambao mwalimu Nyerere aliachiwa na wakoloni mwaka 1962 ulikuwa mzuri. Na uchumi ule ulikuwa mzuri mpaka kufikia Azimio la Arusha. Baada ya Azimio la Arusha uchumi ukaanza kudolola mfululizo, mpaka kufikia miaka ya 1980 ndiyo kikawa kiama kabisa. Vita ya Uganda huwa inatumiwa kama kisingizio tuu cha failed economic policies za mwalimu.
"...uchumi alioachiwa na wakoloni ulikuwa mzuri..." kwa nani? Wakati uchumi huo uliokuwa mzuri ulipoanza kuharibika...unadai ni sera za Mwalimu ndio zilizoharibu uchumi; unaweza ukaeleza dunia ya wakati huo, na hasa Afrika ambako uchumi wake ulikuwa unafanya kazi vizuri sana. Kama katani ambalo lilikuwa ni zao kuu la kutuingizia pesa za kigeni bei duniani kote ikawa mbovu kwa sabau ya polyethylene kuwa mbadala wake, pesa ingeingia toka wapi?

Hatukatai, kuna mambo tuliyofanya au hatukuyafanya yaliyochangia hali kuzidi kuwa ngumu, pamoja na ugumu ulioletwa na mambo yaliyokuwa nje ya uwezo wetu. Kama viwanda vilijengwa vingi tu tukashindwa kuviendesha kwa ujuha wa watu wetu tu, hiyo sio kushindwa kwa sera zilizolenga viwanda hivyo kutuinua.
Kama kuhamia vijijini bila ya mpangilio maalum kuruhusu watu waende mashambani kwao wakalime, utekelezaji mbovu sio kushindwa kwa sera.

Hata sasa mambo mengi tunayojipangia kuyatekeleza tunashindwa kuyatekeleza vizuri, pamoja na kwamba sera za Mwalimu tulishazitelekeza!
 
Ujamaa ni nadharia tu ni ngumu kuwa hali halisi, utumika kama fimbo tools ya kuwafanya wananchi wawe masikini ili iwe rahisi kuwatawala ( inferiority complex) hali ya kutokujiamini kwa mtawala wao wanaamini ni rahisi kumtawala masikini mwenye njaa hiii ni kweli hata sisi tunawapa ujira Mdogo sana watufanyiao Kazi na wao ufanya tu sababu ni masikini. Nyerere na viongozi wote awakuishi ujamaa yaani kuwa sawa na waliowataka wawe sawa mfano atuoni popote kama waliwahi pigia meno mkaa,vaa Viatu vya tairi km vile vya kimasai,kunywa uji Bila sukari,kufulia majani ya mpapai kwa kukosa sabuni,kupanga foleni maduka ya ushirika,kushona viraka,nk.Viongozi wote wa kijamaa duniani uishi maisha ya kitajiri tofauti na wanaowaongoza.
Haya sasa, kila mtu na uelewa wake kuhusu ujamaa. Na wewe haya uliyoeleza hapa ndio ufahamu wako wa 'ujamaa'!
 
Hata sasa mambo mengi tunayojipangia kuyatekeleza tunashindwa kuyatekeleza vizuri, pamoja na kwamba sera za Mwalimu tulishazitelekeza!
Hata mabepari nao hushindwa kwenye sera zao na jinsi wanavyozitekeleza na ndiyo maana kuna maneno kama "Foreclosure" "Financial Crunch" "Economic Slump" "Recession" na mengine mengi.

Uzuri wenzetu wako makini na wanajua umuhimu wa uchumi Imara kwenye maisha yao ya kila siku. Hapa kwetu biashara zinafungwa watu wanasema "wacha wafunge walikuwa ni wapiga dili".

Kwa ivo Mwalimu alikuwa na mapungufu yake na kubwa kuliko yote ni kuamini kuwa waliokuwa wamemzunguka kama na wao wanakubaliana na sera za ujamaa kama alivyokuwa anaziamini yeye.
 
"...uchumi alioachiwa na wakoloni ulikuwa mzuri..." kwa nani? Wakati uchumi huo uliokuwa mzuri ulipoanza kuharibika...unadai ni sera za Mwalimu ndio zilizoharibu uchumi; unaweza ukaeleza dunia ya wakati huo, na hasa Afrika ambako uchumi wake ulikuwa unafanya kazi vizuri sana. Kama katani ambalo lilikuwa ni zao kuu la kutuingizia pesa za kigeni bei duniani kote ikawa mbovu kwa sabau ya polyethylene kuwa mbadala wake, pesa ingeingia toka wapi?

Hatukatai, kuna mambo tuliyofanya au hatukuyafanya yaliyochangia hali kuzidi kuwa ngumu, pamoja na ugumu ulioletwa na mambo yaliyokuwa nje ya uwezo wetu. Kama viwanda vilijengwa vingi tu tukashindwa kuviendesha kwa ujuha wa watu wetu tu, hiyo sio kushindwa kwa sera zilizolenga viwanda hivyo kutuinua.
Kama kuhamia vijijini bila ya mpangilio maalum kuruhusu watu waende mashambani kwao wakalime, utekelezaji mbovu sio kushindwa kwa sera.

Hata sasa mambo mengi tunayojipangia kuyatekeleza tunashindwa kuyatekeleza vizuri, pamoja na kwamba sera za Mwalimu tulishazitelekeza!
Nitakupa mfano mdogo tuu wa uchumi waliouacha wakoloni, kwa darisalama.
Miaka ya 60 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 70, mja mzito alikuwa akijisikia uchungu wa kuzaa, unapiga simu 999, ambulance ya serikali inakuja kumchukua kumpeleka hospitalini. Na baada ya kujifungua alirudishwa nyumbani kwake na Ambulance ya hospitali ya serikali. Babu yangu alikuwa dereva wa Ambulance. Baada ya wabantu kuchukua uongozi, maisha waliyoyaacha wakoloni yakaanza kudidimia mpaka leo hii mzazi akienda kujifungua anatakiwa aende na mkasi, nyembe, gloves, ndoo n,k 😀

Kwa ufupi, mwalimu alikuwa completely inept kwenye uchumi and all matters of economic policy planning. yaani mjomba alikuwa zero kabisa kwenye anga hizo.
 
Hakuna sababu ya kujifananisha na Wazungu. Tujiulize tuu, namna Kenya ilivyo leo, sisi tutachukua miaka mingapi kuyafikia maendeleo ambayo Kenya wanayo leo hii.
Na kwanini wametupita sana wakati tumepata huru wakati mmoja.
Jibu ni kwamba, they were blessed with The great Jomo Kenyatta, and we were not.
 
Nakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.

Mchana wa jua kali la Darisalama tukiwa tumekaa barabarani kusubiri gari la "Ugawaji" litaelekea mwelekeo upi na sisi tulifukuzie kwa nyuma. Hakuna aliyejua leo ni zamu ya duka gani kupelekewa chakula ama mahitaji mengine muhimu ili wakazi wa eneo letu waende wakanunue.

Shuleni wanafunzi wanavaa nguo zisizo na rangi maarufu kama "Maradufu" kutokana na viwanda vya kuzalisha nguo kukosa rangi za kuweka ili vitambaa hivyo viwe na rangi ya Bluu Maalum zama hizo kwa sare za shule za msingi.

Mitaani watu wanavuta sigara kwa "Puff" kwa hela ulizo nazo. Watu wanafua nguo zao kwa kutumia majani ya mpapai, sukari inakaangwa ili kutengeneza chai kwa kuwa hakuna majani ya chai na wenye majani ya chai wanaweza kutumia sukari guru badala ya sukari ya kawaida kama kiungio.

Unakwenda kwenye duka la ushirika kwa mfano kununua Sukari unalazimshwa kununua na kitu kingine kwa mfano Chujio la chai ama birika. Watu wa Darisalama tuliteseka sana na wanawake wengi walibakwa na watu waliojifanya wana bidhaa hizo "adimu" majumbani mwao..

Wakati ule Mgambo na wenyeviti wa maduka ya Ushirika walikuwa kama ni Miungu watu. Sisi kwetu kulikuwa na mgambo aliyetembea na wake za watu alivyopenda kisa yeye ana nafasi kubwa sana ya kupata vitu kwenye duka la Kaya la Mtaani kwetu.

Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.

CC: Mshana Jr Pascal Mayalla
Waliteseka wote sio Dar tu.
 
Umenikumbusha maduka ya RTC, bidhaa kwa foleni na kwa kipimo fulani, uji wa bulga, unga wa yanga (njano)
 
Kwa ivo Mwalimu alikuwa na mapungufu yake na kubwa kuliko yote ni kuamini kuwa waliokuwa wamemzunguka kama na wao wanakubaliana na sera za ujamaa kama alivyokuwa anaziamini yeye.
Kuwa na watu 'committed' katika kufanya jambo lolote, hasa maendeleo ya nchi ni kitu mhimu sana.

Sasa hivi utawasikia hao wanaoimba wimbo wa Magufuli (katika mazuri aliyonayo kuyafanya kwa nchi hii) ukifuatilia mambo wanayofanya hayaendani kabisa na kufanikisha juhudi hizo.

Akipatikana kiongozi wa ku'focus attention' yake moja kwa moja kwa hawa watendaji na kuwavuruga na kuwanyima raha kama hawatimizi yaliyopangwa, nina hakika tutaenda mbele zaidi kwa kasi. Ni lazima apatikane dikiteta 'special' wa kulisimamia kundi hili la watendaji serikalini na kwenye mashirika ya umma.
 
Nitakupa mfano mdogo tuu wa uchumi waliouacha wakoloni, kwa darisalama.
Umezungumzia uchumi waliouacha wakoloni Dar es Salaam, na hukutaka kuzungumzia uchumi wa mlalahoi wa hapo pembeni tu mwa Dar er Salaam, Mwanarumango!
Tena umezungumzia dereva wa ambulance tu hapo Dar, na wala hujaenda kumtafuta dereva huyo au mwalimu wa shule ya msingi pale Rufiji, daktari dispensari ya Ikwiriri, n.k, n.k..

Lakini ni sawa, kama kwako unaona kuwa sera za kujaza Dar es Salaam na neema ndio bora zaidi kwako.
Mimi nazisifia zile sera za Mwalimu kutuwezesha hata sisi watu wa mabonde kwinama kwa haraka kabisa kututoa pale tulipoachwa na wakoloni na kutufikisha tulipoweza kufika kwa juhudi zilizofanyika kutuwezesha kufanya hivyo.
 
Hakuna sababu ya kujifananisha na Wazungu. Tujiulize tuu, namna Kenya ilivyo leo, sisi tutachukua miaka mingapi kuyafikia maendeleo ambayo Kenya wanayo leo hii.
Na kwanini wametupita sana wakati tumepata huru wakati mmoja.
Jibu ni kwamba, they were blessed with The great Jomo Kenyatta, and we were not.
Hapa ndipo panapokufunua na kuonyesha kukosa umakini katika hoja zako.

Unaweza kuwahadaa wasiojua tofauti iliyopo kati ya Tanzania na Kenya kimaendeleo na wakakuamini.
Hakuna tofauti kubwa kati ya nchi hizi. Tofauti inajitokeza zaidi sasa hivi kutokana na mfumo wetu wa elimu uliovurugwa hapo katikati, hata baada ya Mwalimu kustaafu. Elimu yetu imekuwa ni bomu lililotuangamiza, na itachukua muda kutoka kwenye maangamizi hayo. Kama marekebisho hayatafanyika haraka kuimarisha elimu yetu, hata ulete sera zipi, tutaendelea kuangukia pua tu.

Nina ufahamu mzuri sana wa msingi wa uchumi wa Kenya; kwa hiyo huwezi kunihadaa na taarifa za kijumla tu za kusifu kama ulivyoandika hapo juu.
 
Nahisi umejifunua mwenyewe ujinga wako. Unaishi "in denial" ndugu yangu. Kenya wametupita mbali mnoooo kimaendeleo.
Tuanze na enzi hizo za Mwalimu. Big G, zilikuwa zinatoka Kenya. Sabuni Rexona zilikuwa zinatoka Kenya. Sabuni Revola zilikuwa zinatoka Kenya. Viatu chachacha vilikuwa vinatoka Kenya.
Kwa faida yako na wabishi wengine kama wewe, Kenya hawakupoteza miaka 25 katika kujaribu mfumo ambao ulishashindwa duniani kote.
Najua unajaribu kuulaumu mfumo wa elimu wa baada ya mwalimu kujiuzulu ili umuokoe mwalimu katika hili. Kwa taarifa yako, mwalimu ndiyo aliyeanza kuivuruga elimu ya Tanzania. Unaijua "Universal Primary Education"? au UPE?
UPE alianzisha mwalimu nyerere, na kuna watu walichaguliwa kutoka darasa la saba kwenda kusomea ualimu. Nao wakaja kufundisha wenzao 😀
Tanzania imekuwa soko la bidhaa zinazotengenezwa Kenya miaka nenda miaka rudi.
Mwaka 2005 niliwahi kupita Nairobi Airport, nilimwaga machozi baada kuifananisha na Airport yetu.
Sisi saizi yetu imaendeleo ni Uganda na Malawi.
 
Back
Top Bottom