Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...

Azimio la Arusha lililoleta utaifishaji Mali za watu ni zile zile itakadi za chuki kwa matajiri kwa dhania umasikini wao uliletwa na matajiri wakati fursa zilikuwepo tele yeyeto tu angetaman kuwa tajiri angekuwa.
MR.Timiza hukusoma vizuri Azimio na kulielewa. tulitaka njia kuu za uzalishaji mali ziwe mikononi mwa umma wa walio wengi.

tukakata mirija ya unyonyaji. siyo matajiri tu hata wazembe na wazururaji na wanao kaa kwa mjomba tu bila kufanya kazi.

So aliye weza kufanya kazi na afanye kazi kwa faida ya wote. pia kuweka misingi ya kuheshimiana kuondoa matabaka ya Mabwana na watwana,

Mfumo wa kibeberu haukutoa fursa kwa makabwela kama ulizonazo leo. mfano Nijibu hapo ulipo matumizi ya hivi vitu2;
DHAHABU
ALMAS
ELEPHANT TASK
URANIUM
Hapo ni kwa ufupi tu. hakuna nchi hata moja Africa inayonunua, wala kuuza,au kuitumia kama malighafi. faida wanataka mabeberu wao tu na kamwe hutapewa hiyo fursa ya kujua
Tulitaifisha ili tuzalishe wataalamu wetu harakax2 ambao walihitaji pesa masomoni. mfano Tumtemake sanga.Prof Sarungi.Mkapank.tuliwapata nchi ikasonga
 
Ni kweli kwamba njia kuu za uchumi zilikuwa mikononi mwa Umma. Umma ulikuwa unafanya maamuzi kwa kutumia njia zipi?
 
Nakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.

Mchana wa jua kali la Darisalama tukiwa tumekaa barabarani kusubiri gari la "Ugawaji" litaelekea mwelekeo upi na sisi tulifukuzie kwa nyuma. Hakuna aliyejua leo ni zamu ya duka gani kupelekewa chakula ama mahitaji mengine muhimu ili wakazi wa eneo letu waende wakanunue.

Shuleni wanafunzi wanavaa nguo zisizo na rangi maarufu kama "Maradufu" kutokana na viwanda vya kuzalisha nguo kukosa rangi za kuweka ili vitambaa hivyo viwe na rangi ya Bluu Maalum zama hizo kwa sare za shule za msingi.

Mitaani watu wanavuta sigara kwa "Puff" kwa hela ulizo nazo. Watu wanafua nguo zao kwa kutumia majani ya mpapai, sukari inakaangwa ili kutengeneza chai kwa kuwa hakuna majani ya chai na wenye majani ya chai wanaweza kutumia sukari guru badala ya sukari ya kawaida kama kiungio.

Unakwenda kwenye duka la ushirika kwa mfano kununua Sukari unalazimshwa kununua na kitu kingine kwa mfano Chujio la chai ama birika. Watu wa Darisalama tuliteseka sana na wanawake wengi walibakwa na watu waliojifanya wana bidhaa hizo "adimu" majumbani mwao..

Wakati ule Mgambo na wenyeviti wa maduka ya Ushirika walikuwa kama ni Miungu watu. Sisi kwetu kulikuwa na mgambo aliyetembea na wake za watu alivyopenda kisa yeye ana nafasi kubwa sana ya kupata vitu kwenye duka la Kaya la Mtaani kwetu.

Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.

CC: Mshana Jr Pascal Mayalla
Magu awakazie hivyo hivyo, hiyo hali haiwezi jirudia, sio kwa sababu ya imf, sababu there is a lil bit balance duniani sasa hivi.
 
Dark days!
 
Kwanza watu wengi wanashindwa kuelewa kabisa..eti Mwl.Nyerere alitaka mali zote ziwe chini ya umma HAPANA kabisa Mwl.Nyerere alikua anajenga State Capitalism yaani Dola la Kibepari
Hili nadhani Kalamu1 atalielezea vizuri sana.
 
smaki ingawa huu si mjadala wa Mwalimu Kujua ama kutokujua Kiswahili lakini si kweli kwamba Mwalimu alikuwa hajui Kiswahili wakati akija Darisalama, bali inawezekana wakati akitoka Butiama kwenda shule ya Msingi Mwisenge ndiyo alikuwa hajui Kiswahili.

Tofautisha kati ya Lafudhi, lahaja na mtu kutokujua Lugha. Umewahi kukisikia Kiingereza cha Wanaijeria na wahindi. Utasema hawajui Kiingereza?
Ni kweli mkuu siyo mjadala tuna elimishana na kufurahishana, sehemu zoote hizi nimeziishi na kusoma nao, yaani hawajui kabisaa walikuwa wanatuona kama tumeshuka hivi. shuleni ni kilugha tu mpaka nikajua kikurya.Kijiji cha ujamaa Moghabirii. Mkurya akijitahidi kuongea atachanganya na maneno ya kikurya.kama tabhuta-tupa,(kikurya) atasema tafuta iyo(kiswahili) yaani itupe hiyo nk.

Mhindi akiongea anaeleweka hata M-Nigeria kama ulivosema ni local vernacular accent hata black Americans wanazo.

hapo sasa utaelewa nini tafuta hiyo, ukweli niliendelea kutafuta kwa kujiuliza sana nitafute nini mpaka alipo nipa ishara.

au mfano mutotho ana bhita tiricha anaingia taracha, nitamu imechuka sana. mwenyekiti wa kijiji alitoa hotuba seriously. utaelewa kweli muheshimiwa?
 
Magu awakazie hivyo hivyo, hiyo hali haiwezi jirudia, sio kwa sababu ya imf, sababu there is a lil bit balance duniani sasa hivi.
"A lil bit balance" inayoshindwa kuikwamua Zimbabwe, wamejaza Wachina ambao ndiyo wanazidi kuididimiza matopeni. Kuna tafauti kubwa kati ya kuwa shibiki full of wishful thinking na kuwa realistic.
 
MR.Timiza hukusoma vizuri Azimio na kulielewa. tulitaka njia kuu za uzalishaji mali ziwe mikononi mwa umma wa walio wengi.

tukakata mirija ya unyonyaji. siyo matajiri tu hata wazembe na wazururaji na wanao kaa kwa mjomba tu bila kufanya kazi.

So aliye weza kufanya kazi na afanye kazi kwa faida ya wote. pia kuweka misingi ya kuheshimiana kuondoa matabaka ya Mabwana na watwana,

Mfumo wa kibeberu haukutoa fursa kwa makabwela kama ulizonazo leo. mfano Nijibu hapo ulipo matumizi ya hivi vitu2;
DHAHABU
ALMAS
ELEPHANT TASK
URANIUM
Hapo ni kwa ufupi tu. hakuna nchi hata moja Africa inayonunua, wala kuuza,au kuitumia kama malighafi. faida wanataka mabeberu wao tu na kamwe hutapewa hiyo fursa ya kujua
Tulitaifisha ili tuzalishe wataalamu wetu harakax2 ambao walihitaji pesa masomoni. mfano Tumtemake sanga.Prof Sarungi.Mkapank.tuliwapata nchi ikasonga

True ndio maana ujamaa autekelezeki ni nadharia zaidi kuliko hali halisi. Uzembe na uzururaji ni tabia ya kuzaliwa pia kwa Africa haiwezi tekelezeka,sababu kwetu Kazi ni adhabu sio ibada Kama wenzetu. Hata ktk ujamaa matabaka huwezi yakwepa sababu kila mmoja ana matamanio.
 
Hata ktk ujamaa matabaka huwezi yakwepa sababu kila mmoja ana matamanio.
Sijui ni kwa nini kuna watu wanatamani matabaka yasiwepo duniani. Ninachojua kinachowezekana ni kuzuia matabaka yenye nguvu kuyaonea matabaka yale yasiyo na nguvu.
 
MR.Timiza hukusoma vizuri Azimio na kulielewa. tulitaka njia kuu za uzalishaji mali ziwe mikononi mwa umma wa walio wengi.

tukakata mirija ya unyonyaji. siyo matajiri tu hata wazembe na wazururaji na wanao kaa kwa mjomba tu bila kufanya kazi.

So aliye weza kufanya kazi na afanye kazi kwa faida ya wote. pia kuweka misingi ya kuheshimiana kuondoa matabaka ya Mabwana na watwana,

Mfumo wa kibeberu haukutoa fursa kwa makabwela kama ulizonazo leo. mfano Nijibu hapo ulipo matumizi ya hivi vitu2;
DHAHABU
ALMAS
ELEPHANT TASK
URANIUM
Hapo ni kwa ufupi tu. hakuna nchi hata moja Africa inayonunua, wala kuuza,au kuitumia kama malighafi. faida wanataka mabeberu wao tu na kamwe hutapewa hiyo fursa ya kujua
Tulitaifisha ili tuzalishe wataalamu wetu harakax2 ambao walihitaji pesa masomoni. mfano Tumtemake sanga.Prof Sarungi.Mkapank.tuliwapata nchi ikasonga

Acha watu wawe huru mwenye speed ya kuzalisha azalishe kadri atakavochoka na apendae kulala alale atakavopenda.Mwingine nyumba moja inamtosha mwingine mmoja haimtoshi so usimbane mwenye uchu ya zaidi kwa expenses za aliyetosheka.Hulka ya tajiri ni kutokutosheka kwa kuwa na kiu ya kuendelea kutaka zaidi yaani kufungua miradi zaidi kumbuka hii miradi atoajiri wajomba zake ataajili masikini hivo masikini watapata kipato,pia tajiri atakatwa kodi zitakazotumika kutoa huduma muhimu kwa masikini. Ujamaa ni nadharia iliyojikita zaidi kwenye kuwatawala watu kwa kuwafanya wawe masikini ili iwe rahisi kuwatawala maana huwezi mtawala aliyeshiba.Uchumi inatakiwa uwe huru.Ujamaa ni mfumo wa kishetani, mfumo sahihi hata Mungu aliouagiza ni ubepari thus kasema asiyefanya Kazi asile,apendae usingizi atavuna umasikini, apandae kwa nguvu atavuna,mwenye nacho ataongezewa,nk.Hata ukilinganisha masikini ni wengi kwenye ujamaa kuliko kwenye ubepari.Viongozi wote wa kijamaa hawakuishi kijamaa waliishi kibepari
 
Azimio la Arusha lililoleta utaifishaji Mali za watu ni zile zile itakadi za chuki kwa matajiri kwa dhania umasikini wao uliletwa na matajiri wakati fursa zilikuwepo tele yeyeto tu angetaman kuwa tajiri angekuwa.
Propaganda za Mabeberu wa Magharibi hizi ni laini na tamu mnoo, ajabu mpaka leo watu huziamini, White wash ni kitu kibaya sana.
wewe ni lengo la mafanikio ya Mabeberu wa Magharibi,

Babu zetu walipinga sana ujinga huu na uelewa wao mdogo,
Waumini , misikitini na makanisani mliambiwa huwezi kwenda mbinguni kama utapingana na utawala wa mtu anayefanana na Mungu,
Eti wao ni watoto wa Mungu, amewatuma watawale, by the way Yesu ni Mzungu, mtume MSW ni Muarab walewale waliponyonya hamkujua kabisa, wao wana amini mtumwa mzuri ni yule asiyejua kuwa ni mtumwa kama wewe Timiza

Julius Baba Nyerere alipowapendelea akawapa mali za Wazungu kwa kuzitaifisha ili msome na kumiliki,Akawajengea National Housing mpaka leo mwaishi kisasa. mnaona alikuwa na chuki, dhidi ya mnyonyaji wenu walio kupigeni mijeledi wakati mnalima shambani kwa jembe.rejea Kibanga ampiga mkoloni ulisoma hii?

Sasa mwataka nini mmezoea kuchukiwa? Julius alijionea ujinga huu hii mijitu ndo ilivo, akajiondokea kijijiniii!.

Semina zote Tanzania zinazo dhaminiwa na mzungu. anatoa malipo mazuri kwa kila mwana semina, Mswahili mmoja jasho linamtoka anaumia, ana shawishi hela ipunguzwe, eti ''unawapa hela zote za nini, wamekula vizurii na guest house nzuri, halafu uwape hela? hawa washamba hawa kwanza wanashukuru. '' basi hata achukue yeye zimsaidie! no, zinarudishwa kwenye Tasis ya Mzungu zinakaa tu, kwa matumizi mengine.

Hawa ndo type yako,

Unamtetea Ji beberu kiasi cha kujidhalilisha hivi, sababu tu Mwafrika mwenzio asipate, eti atatanua Eheee!. (labda mie niko tofauti) nyie ndiyo walewale mliouza watumwa Uarabuni. ni damu hiyohiyo haijifichi daima dumu,
Tutawapata mmoja mmoja.
Halafu ukisha kuwa kibaraka, unaishi kwa taabu sana, mfano mzuri ni Savimbi(Angola), Mobutu(Zaire ya zamani), Alfonso Dhlakama(Mozambique), juzijuzi tumelizika moja hapo zimbabwe. Angalia wazalendo walivoishi vizuri, Julius,Kaunda,Kenyatta,etc. sielewi ni kwa vipi kijana Mwafrika(jeusi tii) wa leo anatetea Mabeberu ambao tumewashinda kwa gharama kubwa, ajabu zaidi msomi wetu UDSM amekaa mbele ya key board anatoa tamko ''here only work'' to restore the so called hatred nationalised properties.

Samahani sana ndugu yangu,kama nimekukwaza lkn tuna jenga taifa!!!. KARIBU.
 
Sijui ni kwa nini kuna watu wanatamani matabaka yasiwepo duniani. Ninachojua kinachowezekana ni kuzuia matabaka yenye nguvu kuyaonea matabaka yale yasiyo na nguvu.
Ni mitizamo yao mkuu, huwezi wabadilisha, cha muhimu ujue kuishi na watu wenye mitizamo na mawazo tofauti tofauti, kila mwenye imani atatetea anachojua then wanaenda kwenye sanduku la kura. wanachagua, wengi wakishinda wape 5yrs.
 
Ulichoandika hapa kinahusiana na nilichoandika mimi kwenye bandiko langu ulilolinukuu?
 
Propaganda za Mabeberu wa Magharibi hizi ni laini na tamu mnoo, ajabu mpaka leo watu huziamini, White wash ni kitu kibaya sana.
wewe ni lengo la mafanikio ya Mabeberu wa Magharibi,

Babu zetu walipinga sana ujinga huu na uelewa wao mdogo,
Waumini , misikitini na makanisani mliambiwa huwezi kwenda mbinguni kama utapingana na utawala wa mtu anayefanana na Mungu,
Eti wao ni watoto wa Mungu, amewatuma watawale, by the way Yesu ni Mzungu, mtume MSW ni Muarab walewale waliponyonya hamkujua kabisa, wao wana amini mtumwa mzuri ni yule asiyejua kuwa ni mtumwa kama wewe Timiza

Julius Baba Nyerere alipowapendelea akawapa mali za Wazungu kwa kuzitaifisha ili msome na kumiliki,Akawajengea National Housing mpaka leo mwaishi kisasa. mnaona alikuwa na chuki, dhidi ya mnyonyaji wenu walio kupigeni mijeledi wakati mnalima shambani kwa jembe.rejea Kibanga ampiga mkoloni ulisoma hii?

Sasa mwataka nini mmezoea kuchukiwa? Julius alijionea ujinga huu hii mijitu ndo ilivo, akajiondokea kijijiniii!.

Semina zote Tanzania zinazo dhaminiwa na mzungu. anatoa malipo mazuri kwa kila mwana semina, Mswahili mmoja jasho linamtoka anaumia, ana shawishi hela ipunguzwe, eti ''unawapa hela zote za nini, wamekula vizurii na guest house nzuri, halafu uwape hela? hawa washamba hawa kwanza wanashukuru. '' basi hata achukue yeye zimsaidie! no, zinarudishwa kwenye Tasis ya Mzungu zinakaa tu, kwa matumizi mengine.

Hawa ndo type yako,

Unamtetea Ji beberu kiasi cha kujidhalilisha hivi, sababu tu Mwafrika mwenzio asipate, eti atatanua Eheee!. (labda mie niko tofauti) nyie ndiyo walewale mliouza watumwa Uarabuni. ni damu hiyohiyo haijifichi daima dumu,
Tutawapata mmoja mmoja.
Halafu ukisha kuwa kibaraka, unaishi kwa taabu sana, mfano mzuri ni Savimbi(Angola), Mobutu(Zaire ya zamani), Alfonso Dhlakama(Mozambique), juzijuzi tumelizika moja hapo zimbabwe. Angalia wazalendo walivoishi vizuri, Julius,Kaunda,Kenyatta,etc. sielewi ni kwa vipi kijana Mwafrika(jeusi tii) wa leo anatetea Mabeberu ambao tumewashinda kwa gharama kubwa, ajabu zaidi msomi wetu UDSM amekaa mbele ya key board anatoa tamko ''here only work'' to restore the so called hatred nationalised properties.

Samahani sana ndugu yangu,kama nimekukwaza lkn tuna jenga taifa!!!. KARIBU.

Ujamaa umetusaidia nn,mbona tumeshindwa na kurudi kule kule kuwarejeshea tena.Tafuta historia ya kweli acha hii ya darasani iliyochakachuliwa, linganisha South Africa ya kaburu na ya waswahili.Huna Uhuru gani zaidi ya kupandisha na kushusha bendera bendera,hao Viongozi walioleta ujamaa je washawahi pigia mkaa mswaki?,washawahi shonea viraka?,kosa bidhaa? Sukari na sabuni? Washawahi panga foleni kusubiri bidhaa maduka ya ushirika? Mwafrica ana Uhuru gani? Vita vya ukombozi ilikuwa ni hadaaa ya wajanja wachache kuwadanganya wengi ili wapate sapoti ya kuwatoa weupe kisha wakakalia nafasi hizo na kujigeuza wakoloni weusi hata sasa kwa kuwatendea madhila maovu makubwa waafrica wenzao zaidi hata waliyoyafanya wakoloni weupe,kwa kuwaua,kuwafukarisha,kuwaibia waafrica na kwenda kuficha ulaya,Maisha ya waafrica yamekuwa ya hovyo sana baada ya Uhuru. Tumeshindwa kila kitu kuanzia uchumi, demokrasia, Amani,ustaarabu na kila kitu,viwanda, Mashamba,migodi miradi tumeua iliyokuwa ikiajiri mamilioni ya waafrica.
 
Mwambie sasa Tundu Lisu aache ujinga anaoufanya kama kweli unamaanisha na hutak turud huko.

Mapunga mengine haya huku😂😂😂😂😂😂😂😂
Lisu ndo Rais wako wa IMF/WB.
Taabu sana!!!

😈😈😈😈😈😈
 
Acha watu wawe huru mwenye speed ya kuzalisha azalishe kadri atakavochoka na apendae kulala alale atakavopenda.Mwingine nyumba moja inamtosha mwingine mmoja haimtoshi so usimbane mwenye uchu ya zaidi kwa expenses za aliyetosheka.Hulka ya tajiri ni kutokutosheka kwa kuwa na kiu ya kuendelea kutaka zaidi yaani kufungua miradi zaidi kumbuka hii miradi atoajiri wajomba zake ataajili masikini hivo masikini watapata kipato,pia tajiri atakatwa kodi zitakazotumika kutoa huduma muhimu kwa masikini. Ujamaa ni nadharia iliyojikita zaidi kwenye kuwatawala watu kwa kuwafanya wawe masikini ili iwe rahisi kuwatawala maana huwezi mtawala aliyeshiba.Uchumi inatakiwa uwe huru.Ujamaa ni mfumo wa kishetani, mfumo sahihi hata Mungu aliouagiza ni ubepari thus kasema asiyefanya Kazi asile,apendae usingizi atavuna umasikini, apandae kwa nguvu atavuna,mwenye nacho ataongezewa,nk.Hata ukilinganisha masikini ni wengi kwenye ujamaa kuliko kwenye ubepari.Viongozi wote wa kijamaa hawakuishi kijamaa waliishi kibepari
Daaah! weee! mkuu, imenifurahisha sana naona wataka jua kitu wewe;
Sikia bwana kuba Uhuru bila nidhamu ni wendawazimu, hiari yashinda utumwa. na ujamaa haumnyimi mtu fursa zipo mnashindwa kuuelewa sababu ufahamu uko ki Magharibi zaidi,

Propaganda za magharibi zimesimama kwenye uongo, ni ma -x part wa propaganda wale thubutu; hakuna tajiri anayetaka maskini atoke, zaidi ya wao matajiri. sana watampa mahitaji muhimu mazuri tu kama afya na nyumba nzuri za kuishi ili watu wengine kama wewe wautamani Ubepari.
wanatawala kwa kutumia njia kuu tatu;
1) Synthesis.
2) Antisynthesis.
3) Solutions.
Hii ina maana wanaitisha jamii tawaliwa, then wanapinga vitisho hivyo kwa nguvu zote, na watu wameajiliwa kufanya kazi hiyo kwa hela nyingi ndo unao waona leo ni matajiri, hasa hasa Medias,Km TV, Magazeti etc
Baadaye wana tafuta suluhisho, wanajitokeza Watoto wa Mabepari damudamu, wakitumia hizo hela za wa Africa kujifanya wanatetea jamii tawaliwa. mfano WTC ilivo shambuliwa .mchezo unaofanywa Middle East, Lockerbie bombing

Siyo hayo tu sponsors wote wa skirmish war Duniani ni Mabepari, ambao leo unaamini wana uhuru wa kufanya unachotaka. wewe una dhani AL-shabab, Boko haram,ISIS, wanapata wapi silaha, chakula, mishahara,Usafiri. Jibu ni hela za mabepari hizo ndo mungu wako alivo taka uko sahihi kabisa,ndivo alivyo watuma. Lakini siyo Mungu wetu wa ujamaa sawa?

Lengo ni kuimarisha ngome yao ya Magharibi hata ukitaka leo unakuwa tajiri tu.kupitia mgongo wao ila mwisho wako hautakuwa mzuri.si unaona Gaddafi alivo busiana na jack shirack, lakini Gaddafi yuko wapi leo;
Sera zao ziko wazi hawana rafiki wa kudumu, wao ni wao tu. ni wamoja kwisha. wako juu ya sheria mtoto wa kiume wa Thatcher Michael,alikamatwa kwa uharifu Equatorial Guinea, mbona aliachiwa tu. ma Rais wa nchi zote wanawekwa na wao, hivyo vimadini vyenu wanachimba wao,watawapa hela wanayo taka, hamtafurukuta, ebu fikiria stone kaishia kimya kimya na makanikia yake,(alikuwa hajui), maskini, na ni familia hizo za kibepari zina tawala Dunia yoote.isipokuwa nchi za kijamaa.
na huyo mungu wenu wa kibepari mashoga,sagaji,good time rukhsa, pesa iko mtapewa. uhuru wa Dume kutoa nyaa! Jamani wana JF kweli haki? dada zetu wakose mambo? nchi za kijamaa umewahi sikia haya?

Amini usiamini ni familia ishirini tu ndo unadhani ni mabepari wa Magharibi, hivo wanainua mtu mmoja mmoja sana, tena kwa kiwango fulani baaadaye anarudi chini chini kabisa. hata.... U-rais utapata. lakini?.watakuomba mambo...........wakikupenda sana. wale usijiulize maswali anza kulia na uomboleze na familia yako..
 
Nahisi umejifunua mwenyewe ujinga wako. Unaishi "in denial" ndugu yangu
Sasa hii nayo ni sehemu ya kutuelimisha unayoyajua wewe?
Kwa faida yako na wabishi wengine kama wewe, Kenya hawakupoteza miaka 25 katika kujaribu mfumo ambao ulishashindwa duniani kote.
Mfumo upi haujashindwa dunia kote? Unaweza usielewe maana ya mfumo ndio maana unang'ang'ania 'mfumo' kushinda au kushindwa!
Big G ilimsaidia kitu gani mkenya ambaye ni hana ardhi na ni manamba tu kwenye mashamba ya wazungu! Uchumi wa kuzalisha mamilionea wa dola za Marekani zaidi ya 30 kwa mwaka huku maskini wanaourudi kwenye rindi la ufukara milioni na zaidi katika mwaka huo huo? Na mbaya zaidi wengi wa hawa mamilionea wengi wao sio wakenya!

Na kama Kenya hawakupoteza miaka 25, mbona nchi kama Ethiopia ambao walikuwa ni maskini maradufu sasa wanawatimulia vumbi katika upanukaji wa uchumi wao? Unaelewa Ethiopia walipoteza miaka mingapi?
UPE alianzisha mwalimu nyerere, na kuna watu walichaguliwa kutoka darasa la saba kwenda kusomea ualimu. Nao wakaja kufundisha wenzao 😀
Tulipopata uhuru tulikuwa na walimu wangapi wenye diploma tu na hata vyeti? Na kama elimu yetu ilikuwa inapanuka haraka, ulitaka walimu tukawatoe wapi?
Unashindwa kutambua dhumuni la kuwawezesha hata hao wa darasa la sba kuwa walimu. Hata watu wazima (kisomo cha ngumbaru) kilikuwa na lengo lake, lakini wewe hapa unataka kuyafanya haya yawe ndio sababu ya elimu kuvurugika!
 
Back
Top Bottom