UMASIKINI

UMASIKINI

MGOGO27

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2016
Posts
459
Reaction score
218
UMASIKINI WAKO NI NINI?

-UMASIKINI unanzia Kwenye kupuuza unapoambiwa UKWELI na kuhisi anaekwambia sio saizi yako,lakini

-UMASIKINI mkubwa ni Kukubali wewe ni masikini,lakini

-UMASIKINI mkubwa zaidi ni Kujilinganisha na aliyekuzidi UMASIKINI,lakini

-UMASIKINI mbaya ni kumchukia Aliyekuzidi Akili au Mali au Elimu(ayeweza zaidi yako),lakini

-UMASIKINI mbaya zaidi ni kukataa kujifunza kwa Aliyekuzidi na kukataa kwenda na wakati,lakini

-UMASIKINI kiwango cha Changalawe ni Kupanga juu ya kesho(future)za wengine bila kujua kuna Mungu, lakini

-UMASIKINI wa kiwango cha Lami ni Kuhisi Unaonewa kwa Jambo lisilo haki yako na kuhisi unakubalika bila kipimo rasmi(kununua watu),lakini

-UMASIKINI kiwango cha fly-overs ni Kujisingizia Utajiri,Ukuu(kununua heshima)wakati hauheshimiki wala haufikiliwi na watu kiwango hicho!

Huo ni UMASIKINI hata kama una mahela kibao kwenye mabenki

By
Mathias Raymond Nyakapala
 
Back
Top Bottom