1995_No_Ku_Fake
JF-Expert Member
- Aug 24, 2026
- 1,561
- 3,328
Umeeleza kwa busara kweli.Hamna kitu kinachoumiza kama kuwa na uhitaji mkubwa huku mfuko wako ukiwa mtupu. Unaumwa huna pesa ya matibabu, una njaa huna pesa ya chakula, una ndoto lakini huna mtaji, na una matatizo ambayo huwezi hata kumweleza mtu kwa sababu huna uhakika kama atakuelewa.
Umaskini unaweza kukufanya uishi huku ukihisi kama umeshakufa ndani. Unaweza kukunyima usingizi, kukuvunjia heshima mbele za watu na kukufanya uogope hata kupokea simu kwa sababu hujui utajibu nini kwa wanaokudai.
Kinachouma zaidi ni kwamba watu wengi hawakuchaguliwa kuwa maskini; mazingira, fursa na hali za maisha zimewafikisha hapo. Lakini jamii mara nyingi humhukumu mtu kwa alichonacho mfukoni badala ya kuangalia anapitia nini.
Hata hivyo, umaskini si mwisho wa maisha, wala si kipimo cha thamani ya binadamu. Tatizo ni pale mtu anapokosa hata fursa ya kuanza kujinasua.
Swali langu ni hili:
Je, umaskini ni matokeo ya maamuzi ya mtu binafsi, au kuna mazingira ambayo yanaweza kumfanya mtu afanye juhudi kubwa lakini bado ashindwe kutoka kwenye hali hiyo?
Ningependa kusikia mitazamo yenu ya kweli, si kauli za kusema tu “maskini ni wavivu.”
Kweli mkuu, umaskini si kukosa pesa tu, bali ni maisha yenye masomo mengi ambayo huwezi kuyaelewa mpaka uyapitie mwenyewe. Kuna mambo maskini anayajua ambayo mwenye nacho anaweza asiyaelewe kirahisi.Umeeleza kwa busara kweli.
Umaskini ni somo ndefu kweli yaani
Atanikieleza nazani sitamaliza.
Poverty is a disgrace.I hate poverty
Wewe kuna kitu unajua.Poverty is a disgrace.
Umasikini unaweza kuchangia watu kufanya maamuzi ya hovyo, lakini utahira haupimwi kwa kiwango cha umasikini. Tatizo ni pale mtu anapopata madaraka bila hekima, uwajibikaji na maadili. Hapo ndipo wananchi huanza kulipa gharama za uongozi mbovu.Umasikini ndio chanzo cha utahira
Viongozi wengi wa kiafrika wamelelewa kwenye absolutely povert ndio maana WeHu
Inaonekana umasikini huujui kwa kina na njaa bado unaiskia hujaiishi au kuona mtu mwenye njaa weweUmasikini unaweza kuchangia watu kufanya maamuzi ya hovyo, lakini utahira haupimwi kwa kiwango cha umasikini. Tatizo ni pale mtu anapopata madaraka bila hekima, uwajibikaji na maadili. Hapo ndipo wananchi huanza kulipa gharama za uongozi mbovu.
Kiuhalisia umaskini haupo!
Kuna wahuni wachache walifanya makaratasi yaitwayo fedha yawe ya thamani na tukaaminishwa huo uongo na kuukubali,kumbe ni mchongo wa kimazingara!!!
Na matajiri wanatengenezwa na mfumo TU,kwasasa hakuna tajiri wa kweli anaeonekana asiekwepa kodi,Kodi zenyewe hazilipiki!!
Umaskin na utajiri ni fiction za kimedani hakuna uhalisis kabisa!!