Umati wajitokeza kutia nia kwenye Ubunge na Udiwani kupitia CHADEMA, nafasi zimejaa kabisa

Hii ni Taarifa kutoka kwa John Mrema ambaye ni mkurugenzi wa Itifaki wa Chadema, Ikumbukwe kwamba Chadema iliweka utaratibu kwa wanachama wake wote wanaotaka kugombea nafasi hizi kujitokeza mapema kutia nia kwenye chama chao ili usaili ( Vetting ) juu yao uanze mapema, lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa viongozi kuwafahamu kiundani Wagombea hawa kabla ya kuwapa nafasi za kugombea.

Nafasi zote za ubunge na udiwani kwenye majimbo na kata zote nchi nzima, hakuna mtia nia ambaye yuko peke yake, yako majimbo ambayo kuna watia nia ya ubunge kuanzia watatu hadi watano!

Kwa aina ya siasa za Tanzania za sasa Umati huu wa watia nia wa Chadema una maana gani?

# TUENDELEE KUNAWA MIKONO ILI KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA .

Kwa hiyo John Mrema kakufuata wewe na kukupa hizi taarifa na wewe umeona uweke hapa JF? Je, nitakuwa namekosea nikisema wewe ndio John Mrema? Je, nitakuwa nimekosea nikisema JF imenunuliwa kihalali na Chadema? Je, nitakuwa nimekosea nikisema kwamba hiyo ndio sababu kubwa michango na thread nyingi huhamishwa kwa maelekezo ya John Mrema?
 
Kwani kutoa taarifa jf limekuwa kosa ?
 
Hiki ndio kimekimbiza wabunge mamluki na wachovu kama akina Lijuakali
 
Nilitamani sana kwenda kumtoa Mh. Luhaga Mpina! Ana bahati sana mambo ya kianzio hayajaniendea vizuri!
 
kwa jinsi alivyochoma nyavu za watu ingekuwa rahisi tu
Yaani naona kama nimekosa bahati aiseee! Ni mwepesi mno, CHADEMA tunatakiwa tupate mtu sahihi tu huku, hakuna cha maana alichokifanya jimboni kwake miaka leo 15 na uwaziri juu!
 
Hii ni Taarifa kutoka kwa John Mrema ambaye ni mkurugenzi wa Itifaki wa Chadema, Ikumbukwe kwamba Chadema iliweka utaratibu kwa wanachama wake wote wanaotaka kugombea nafasi hizi kujitokeza mapema kutia nia kwenye chama chao ili usaili ( Vetting ) juu yao uanze mapema, lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa viongozi kuwafahamu kiundani Wagombea hawa kabla ya kuwapa nafasi za kugombea.

Nafasi zote za ubunge na udiwani kwenye majimbo na kata zote nchi nzima, hakuna mtia nia ambaye yuko peke yake, yako majimbo ambayo kuna watia nia ya ubunge kuanzia watatu hadi watano!

Kwa aina ya siasa za Tanzania za sasa Umati huu wa watia nia wa Chadema una maana gani?

# TUENDELEE KUNAWA MIKONO ILI KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA .
Kwahiyo tunanawa mikono tuu bila karantini?
 
Hulka ya kibinadamu kabisa. Kutia nia ni kuonyesha kuna tumaini fulani. Je, hilo tumaini ni la mtu binafsi, jamii au kikundi ndiyo cha msingi.
 
Back
Top Bottom