Umbo la miguu na mpira wa miguu haviendani!

Umbo la miguu na mpira wa miguu haviendani!

babacollins

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
901
Reaction score
212
Mpira una umbo la duara na miguu ina umbo ambalo kiuhalisia haliendani na kuuchezea mpira. Hii ni sababu muhimu kwa watoto wanaopenda soka kuzoezwa mapema kuuchezea mpira kwa muda mrefu.

Kwa Afrika ni timu chache zenye uwezo wa kuwa na timu za watoto ambapo kila moja ana mpira wake kwa ajili ya kumpa muda mrefu wa kucheza na mpira.

Kwa hiyo sio ajabu kuwakuta baadhi ya wachezaji huku kwetu, wakiwa na uwezo mdogo wa umiliki wa mpira na wapo madaraja ya juu.

Hii ni miongoni mwao kanuni muhimu pia katika soka.

Mchezaji kiongozi.
 
Umbo lile kwa mguu ndio sahihi, vinginevyo vingeluwa vichekesho, kukaa na mpira sio kuujua, ball caontrol ya phil jones ni mbovu hafikii walau robo ya erasto nyoni.

Kuna zaidi ya haya unayofikiri wewe.
kwa upande wako upo sawa umezungumzia "usahihi" mimi nazungumzia "kuendena".
 
Ulitaka mguu uwe mviringo,hata ume na uke havifanani ili viwe compartible
😂😂😂 uko sahihi ndio maana nimesema " HAVIENDANI" sio havifanani.

Sio compartible kama ulivyosema uke na uume au kizibo na chupa ndio nilichomaanisha.
 
Mbona kama dizaini unamsema kibudenga na mugalu kijanja?
 
kwa upande wako upo sawa umezungumzia "usahihi" mimi nazungumzia "kuendena".
Upo sahihi, hata ukimchukua mtoto mdogo uanze kumfundisha basic za mpira utagundua mpira na miguu haviko sawa, ila anavyozidi kujifunza ndo mfanano wa miguu kwenye mpira huongezeka, hii ina maana kujifunza mpira tangu mdogo kuna utofauti mkubwa na ukiwa mtu mzima. Nimeshuhudia mtu mzima asiyejua mpira akiukanyaga tu anadondoka.
 
Asante, pia anaezoea kucheza mpira peku siku atakapo pata viatu anaweza kuona ni vigumu kucheza akiwa amevaa viatu lakini baada ya muda huzoea na kuona kawaida tu.
 
Back
Top Bottom