Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Migogoro mingi ya mirathi kwenye familia hutokea pindi mhusika anapofariki dunia, huku akiwa hajaacha wosia.
Wosia ni maandishi au kauli inayoachwa na mtu anapokuwa hai ni namna gani angependa mali zake zigawanywe kwa warithi wake pindi atakapofariki dunia. Kuna aina mbili za wosia ikiwemo wa maandishi na wa mdomo ambazo zote zina vigezo vyake katika kukubaliwa kama ushahidi pindi muandikaji atakapokuwa amefariki.
Kwa wosia wa mdomo huu hutolewa pale muhusika hajui kusoma wala kuandika au amepoteza uwezo wa kuzungumza.
Pamoja na umuhimu wa wosia, bado imeonekana kwenye jamii haijachukuliwa kwa uzito na hivyo kuchangia kuwepo kwa migogoro ya kifamilia pale mwenye wosia wake anapofariki.
Hilo linaonekana katika jamii, kwani miaka ya karibuni kumeibuka migogoro ya kugombea mali za marehemu, jambo linalochangia kuongezeka kwa kesi nyingi za mirathi.
Kwa mujibu wa taarifa za Kituo cha Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke (IJC), tangu kuanzishwa kwake miezi sita iliyopita, mashauri 2,911 ya kesi za mirathi yamefunguliwa kituoni hapo ambayo yanahusisha Mkoa wa Dar es Salaam pekee.
Kutokana na hilo kunakuwepo pia na uhasama miongoni mwa familia au kutumia muda mwingi katika kufuatilia kesi hizo badala ya kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Hata majibu yanapotoka ya kuupa ushindi upande mmoja huwa hawakubaliani nayo na kushuhudiwa kuwepo kwa visa mkasa ikiwemo kufanyiana vitendo vya ukatili kama mauaji.
Mbaya zaidi matukio ya aina hii yameonekena zaidi kuwaathiri wanawake, kwani kwa utamaduni wetu mmiliki wa mali ni mwanaume na ndio maana shida zinakuwa nyingi anapotangulia kufariki mwanaume.
Mambo haya pia yamechangia kusambaratika kwa familia na baadhi watoto kulazimika kukimbilia mitaani hasa pale mama anapokuwa hana uwezo wa kuwalea au ndugu walioachiwa kuwafukuza na kurithi mali za ndugu yao.
Ofisa Sheria wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Janeth Mandawa anasema vipo vigezo vianavyopaswa kuzingatiwa katika uandikaji wosia ikiwemo uwe umendikwa kwa kalamu ambayo haitaweza kufutwa na mtu yoyote na kukaribisha mianya ya kubadilishwa.
Kigezo kingine ni tarehe na sahihi ya mtoa wosia kuonyesha lini aliaacha huo wosia, utaje nani ni warithi na orodha ya mali na namna gani zimegawanywa.
“Jambo lingine ni lazima uwe umeshuhudiwa na mashahidi wawili kwa wosia wa maandishi na mmoja anaweza kuwa ndugu na mwingine mtu wa karibu ambaye muandika wosia atamchagua. Wosia wa wa kauli mashahidi lazima wawe wanne---wawili ndugu wa karibu na wawili watu anaowaamini.
“Pia katika wosia huo, mtoa wosia anapaswa kutaja jina la nani anapaswa kuwa msimamizi wa mirathi na wakati mwingine kusema au kuandika wapi akazikwe,” anasema Janeth.
Nani anapaswa kuandika wosia
Mtu yoyote aliyefikisha umri wa utu uzima, Janet anasema anaruhusiwa kuandika wosia yaani kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Janeth anasema ili wosia uwe na sifa unapaswa kutolewa bila ya vitisho, muandikaji akiwa na akili timamu na bila kulazimishwa.
Janeth anasema kuna umuhimu wa kuacha wosia kwa kuwa muhusika anapata nafasi ya kuchagua nani warithi na pengine kuna ambao wasingekuwa warithi halali kutokana na sharia, lakini wakarithi kupitia wosia.
“Pia itasaidia katika kesi ya mirathi kujua wanasimamia misingi gani kutokana na staili ya marehumu aliyekuwa akiishi.
“Mfano muislamu, mkristo, sheria za kimila na zile za watu waliokuwa wakiishi maisha ya kawaida inayoitwa sheria ya kiserikali ya mwaka 1865. Kwa kufanya hivyo katika uendeshaji kesi ya mirathi inasaidia kufuata maelekezo ya kile mtoa wosia alichoacha hasa kunaopotokea mvutano wa kisheria,” anafafanua Janeth.
Utaratibu wa kuacha wosia
Kuhusu utaratibu wa kuacha wosia, mwanasheria huyu anasema muhusika anapaswa kuandaa orodha ya wosia wake, kuandaa orodha ya mali zake, jina la msimamizi wa mali zake na hata kuandaa wapi atazikwa.
Katika hili anasisitiza wosia ni siri ya mtu na kueleza moja ya faida inaweza ikatokea katika orodha ya warithi labda ulimwandikia mali nyingi akataka kumtoa uhai muandika wosia mapema ili arithi mali.
“Ni vema wosia huo ukashuhudiwa na wanasheria na pia hairuhusiwi kumuacha mrithi halali isipokuwa kama kuna sababu za msingi,” anasema Janeth.
Anazitaja sababu hizo ni pamoja na mrithi kutomtendea wema mtoa wosia ikiwemo kutaka kumuua, mrithi kutembea na mwenza za mtoa wosia. Jambo lingine ni labda mrithi alishapewa mali akazitumia vibaya au mrithi hakumsaidia katika tabu au ugonjwa na sababu nyingine ambazo mtoa mirathi anapaswa kuziandika.
Wapi pa kuhifadhi
Wosia unaweza kutunzwa kwa wakili aliyesajiliwa na mwenye ofisi, rafiki unayemuamini, katika nyumba za ibada ambako kuna sheikh, padre au mchungaji unayemuamini.
Hata hivyo, Janeth anasema mbali na huko kwa sasa hilo linawezekana kufanywa Rita na jambo hilo lilianza tangu mwaka 2008 ilipopitiswa sheria ya kuwaruhusu kufanya hivyo.
“Rita tuliruhusiwa kisheria kutunza wosia baada ya kugundulika huenda kuhifadhi kwa watu binafsi nao kama binadamu wanaweza kupatwa na majanga ikiwemo kufariki, lakini kwa Serikali utakuwa pale milele,”anasema Janeth.
Kuhusu gharama za kuhifadhi, anasema kwa mtu mwenye mali chini ya thamani ya Sh200 milioni kuandaa ni Sh20,000 na Sh20,000 kutunza, mali zikiwa ya zaidi ya thamani ya Sh200 milioni kuandaa ni Sh 30,000 na Sh30,000 kutunza na zikiwa zaidi ya thamani ya Sh500 milioni, kuandaa ni Sh50,000 na kutunza ni Sh50,000.
Akitoa takwimu za walioandika wosia tangu Rita ilipoanza kazi hiyo mwaka 2008, anasema wameshaandaa na kutunza wosia 986.