Umegundua nini?

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,922
Reaction score
3,559
Habari wakuu,

Katika pitapita zetu za maisha tumejikuta tukienda sehemu mbalimbali kulingana na sababu mbalimbali ikiwamo masomoni,kazini,biashara, utalii nk nk

Kuna wengine wamefanikiwa kuvuka mikoa yao,nchi zao,na hata mabara na wengine hawajawahi hata kutoka nje ya mikoa yao lakini bado kuna vitu ambavyo wamegundua na wanaweza kutujuza pia.

Lengo ni kujaribu kufahamishana mambo kadha wa kadha ambayo pengine si ya kawaida tuliyowahi kuyashuhudia katika mizunguko yetu ili na wengine ambao hawajawahi kufika katika hayo maeneo basi wakaelimika na kpata faida pia.

Mfano nimegundua,
Akina mama/bibi wa Iringa hata kama akiwa anasalimiana na kijana mdogo wa kiume ni lazima wakunje goti.

Madereva na makondakta wengi wa daladala aina ya Dcm jijini Dar ni Wachagga

Wazaramo wanathamini zaidi ngoma kuliko kitu kingine chochote.

Wadau nyie katika tafiti zenu ndogo mmegundua nini?
Karibuni
 
hiyo tafiti ulifanya kwa kipindi gani ? uliwafanyia watu wangapi ? leta analysis inayoeleweka
 
hiyo tafiti ulifanya kwa kipindi gani ? uliwafanyia watu wangapi ? leta analysis inayoeleweka
Mkuu hizi ni tafiti ndogo ndogo ambazo hazihitaji analysis kama zile official ulizozizoea mkuu (Just don't complicate mkuu)
 
Nimegundua akikukataa bila sababu ya msingi ipo siku atarudi "analia"
 
Nmegundua Tegeta ni maarufu kuliko Kolomije
 
Nimegundua akikukataa bila sababu ya msingi ipo siku atarudi "analia"
Mda huo ulishamfuta kabisa kwenye mipango yako.
Kama ulipanga kumfanya mke anakua kimada sasa loh.
 
Mimi katika tembea zangu ndani kabisa ya vijiji vya umasaini,
Nikakutana na mzee mmoja nikamsalimia mzee shikamoo na yeye akajibu musee shighamoo, nikapotezea nikajua atakua anaact , nikakutana na mwingine na yeye hivyo hivyo kumbe wao wanajua ukiwasalimu shikamoo na wao wanajibu shikamoi
 
Nimegundua JF kuna watu ni wazuri wa kuigiza maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…