Umeicheki IRIS? Hizi ni facts 10 usizozijua kuhusu series hiyo

Umenikumbusha... ngoja niitafute pamoja na Athena yake ili niziangalie kwa mfuatano!
 
Kiukweli IRIS 1&2 ni 'konyoo',,, ni moja series bora kuwahi kuziona

Maudhui kwa ujumla ya ile series ni kuonesha namna gani South Korea na North haziwezi kuja kuwa kitu kimoja kwasababu kila mara viongozi wa hayo mataifa wakijaribu kukaa meza moja kutafuta muafaka inashindikana kutokana na kikundi hatari cha IRIS chenye nguvu na ushawishi ndani na nje ya nchi zao kinavyohujumu mipango na mikakati yao

Kikundi hiki cha IRIS ambacho kimeundwa na watu wenye pesa kimejaa watu waliobobea kwneye ujasusi, mapigano nk kinawapa upinzani mkubwa sana idara za usalama wa Taifa wa mataifa haya mawili

Hio sio series ya kukosa hata kidogo
 
Dah nmeichek vipande kadhaa tu nikijua nitapata nzima muda wwte ila sijafanikiwa, naweza kupata wapi hii seriese pamoja na zingine za kikorea???
 
Kuna ile scene wanavamia mall magaidi naona magaidi wa Kenya walicopy walipovamia Westgate mall.Ni series moja Matata sana
 
Pamoja na kuwa shabiki mkubwa wa kdrama hii drama sijawahi kuiangalia. Sababu kuu iliyofanya nisiangalie ni haya masimulizi ya watu yanayoelezea iliishaje. Mimi nikishaambiwa tu kuwa drama inaishaje huwa hamu ya kuangalia inaisha kabisa....ya nini nipoteze muda na mb zangu wakati najua kabisa mwisho wake? Labda nikute inarushwa kwenye kituo cha televisheni
 
Jumong ilipelejea kuangalia hizi series za kikorea, tokea hapo nimeangalia series na drama nyingi sana za kikorea mpaka zingine nimezisahau.

1. City Hunter
2. Iris 1&2
3. Athena
4. Six dragon [emoji236] fry
5. Dong Yi
Love story in Harvard
 
Inji hii bhana inakataza kufanya maigizo yoyote yawe ya luninga au sauti yanayoendana na majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama. Kufanya ivo ni kosa kwa mujibu wa sheria ya usalama wa Taifa nimesahau ni sheria namba ngapi na ya mwaka gani. Kuangalia bongo muvi heri waninyonge. Licha ya vikwazo vya technolojia wanayotuma watu wa hongo muvi lakin bado sheria za nchi zinawabana sana hata kufanya ubunifu walau kulingana na mazingira yaliopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…