Umeicheki IRIS? Hizi ni facts 10 usizozijua kuhusu series hiyo

Umeicheki IRIS? Hizi ni facts 10 usizozijua kuhusu series hiyo

Moja kati ya Series ya kikorea iliyochezwa vizuri, nyingine ni GIANT, EAST OF EDEN & GOODBYE MR BLACK.
 
Kama sikosei hii ndo drama yangu ya kwanza ya kikorea
 
Pamoja na kuwa shabiki mkubwa wa kdrama hii drama sijawahi kuiangalia. Sababu kuu iliyofanya nisiangalie ni haya masimulizi ya watu yanayoelezea iliishaje. Mimi nikishaambiwa tu kuwa drama inaishaje huwa hamu ya kuangalia inaisha kabisa....ya nini nipoteze muda na mb zangu wakati najua kabisa mwisho wake? Labda nikute inarushwa kwenye kituo cha televisheni
Hebu itafute hiyo series hutojutia kuingalia, humo kuna kila kitu in human knowledge to know.
 
Nakumbuka mara ya kwanza kuona tamthiliya ya Iris ilikuwa ni ITV pale mwaka 2013 kama sio 2014 kipindi hicho hata smartphone sina.

Nilivyoiona tu mara ya kwanza sijui ilikuwaje lakini tangu hapo sikuacha kuifatilia mpaka episodes zote 20 zilivyoisha.Nakumbuka nilikuwa nachelewa kulala siku alhamisi na ijumaa saa 22:00 mpk 23:00 ili tu nione Kim Hyun Jun ameishia wapi.

Kiukweli Iris ndio imenifanya mpaka leo mimi niwe shabiki wa Korean dramas na ndio maana leo nimeamua kuweka hapa facts 10 ambazo inawezekana huzifahamu kuhusiana na drama hii ambayo iligharimu takribani 16M USD ili kuikamilisha :

1. Kim Hyun Jun ambaye ndo alikuwa "steringi" kwenye series alikuwa analipwa takriban Tzs milioni 200 kwa episode moja. Tukumbuke episode zilikuwa 20! Huku Choi Seung Hui yeye alilipwa takriban Tzs million 40 per episode!

2. IRIS Ilitengenezwa na Taewon Entertainment moja ya kampuni kubwa sana nchini Korea. Na IRIS haikushirikisha kituo chochote cha TV wakati inatengenezwa. Producers walitaka chaneli kama SBS, MBC na KBS 2 vishindane dau atayeshinda ndie atakayepata haki ya kuonesha IRIS. Of course KBS 2 ndio ilishinda na IRIS ikaanza kuoneshwa October 14 mwaka 2009.

3. IRIS pia shooting ilifanyika kwenye nchi tatu. Walianza kushoot Japan pale Akita March 10 2009 kisha wakaenda Budapest huko Hungary ( rejea episode ya 2) na kumalizia principal photography huko Seoul South Korea.

4. Kim Tae Hee ambaye kwenye series ameigiza kama Choi Seung Hui ilibidi ajifunze martial arts kidogo ili aweze kufit kwenye series hasa kwenye upande wa action hii scenes. Pia kwenye series waigizaji walikuwa wanafanya Stunts zao wenyewe.

5.Bajeti ya series nzima ilikuwa ni takribani 16M USD. Kupelekea Iris kuwa mojawapo ya tamthiliya za kikorea zilizogharimu mkwanja mrefu.

6. IRIS pia imezalisha watoto au series nyingine kama IRIS 2 starring Jang hyuk ambao ni muendelezo wa IRIS 1 japo actors ni tofauti na ATHENA starring Soo Ae. Ukiachana na hizo series mbili pia kuna movie inaitwa IRIS THE MOVIE ambayo hii ina utofauti kidogo na series.

7. Wengi wanasema IRIS imeisha vibaya maana haijulikani nani alimuua Kim Hyeonjun. Lakini aliyemuua Kim ni AGENT RAY sniper hatari sana kutokea kwenye kikundi cha Iris. IRIS 2 imeelezea vizuri tukio hilo.


8. Kuna ile scene kwenye Episode ya 19 ambapo Kim Hyun Jun na Choi Seung Hui wanapigana na magaidi wanaotaka kulipua Seoul, barabarani. Sasa ile scene ilifanya barabara ya Seoul karibu na Gwanghamun plaza ifungwe kwa masaa 12. Kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa 1 usiku ili tu kushoot hiyo scene.

Serikali ya Seoul City ilivyoulizwa ikasema imeruhusu jambo hilo kwani itasaidia kukuza utalii hapo mjini Seoul.

9. Katika hali ya kushangaza kidogo kituo cha TV kiitwacho TBS kutokea Japan kilinunua haki za kuonesha series hiyo kwa USD Million 4.2.

Baada ya kununua series hiyo ili ionyeshwe huko Japan ilifanya dubbing huku waigizaji wakubwa huko Japan kama Tatsuya wakiingiza sauti zao na ofcourse walivyoanza tu kuionesha ratings za watazamaji zilipanda sana.

10. IRIS ni mojawapo kati ya series ambazo ziliangaliwa sana huko Korea ikiwa na audience share ya wastani 30% kitu ambacho kipindi kile ilikuwa ni nadra sana kutokea

Yes! Najua uzi ulikuwa mrefu kidogo ila hayo ni machache tu kwa leo.



Wasaalam. View attachment 1774087View attachment 1774088View attachment 1774090View attachment 1774091View attachment 1774092
Naomba kujua mtu aliemtambua Mr Black kwenye hii series
 
Series Kali hiyo nakumbuka bibie alilia pale sterling alipouawa Iko so emotional.
 
Sorry kama nipo nje na maafa, Hivi kati ya IRIS na Descendants Of the Sun, ipi kali niangalie
 
Back
Top Bottom