Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
kumbe kilichowasibu Piacenza ni Mgomo na hali ngumu ya Uchumi!!!
Iko hivi:
Moja ya habari iliyoshika kasi sana ilikua kipigo cha mbwa mwizi kwa klabu ya Pro Piacenza.
Hawa wanashiriki ligi daraja la pili kule Italia maarufu kama Serie C'
Basi bwana hii leo wamefungwa 20-0 na klabu ya AC Cuneo!!!
Wengi tukashangaa japo hatuifahamu vema.
Baadhi yetu wakahisia matokeo yamepangwa!
Hasa wakizingatia Mpaka kufikia mapumziko walishapigwa 16-0!!!
Nilitamani kuandika lakini nafsi yangu ilisita!
Nikasubiri mechi iishe, ikaisha.
Nilipotaka kuandika nafsi yangu ikasita tena!
Nikaona nitizame mawili matatu ya kuihusu klabu Hii!
Nikafungua msimamo wa ligi nikaona jamaa wapo nafasi ya mwisho, nafasi ya 20.
Nikaanza tafakari!
Kustaajabu jamaa wana mechi chache kuliko wenzao!
Wamecheza mechi 19, wenzao wana 25 wengine 26.
Nikatizama zaidi katika hizo 19 wameshinda 5 sare 1 na kupoteza mechi 13.
Nikatizama zaidi na zaidi nikaona wamefunga goli 18 na kuruhusu 56, 20 zikiwa zimeongezeka leo!
Nikastaajabu
Iweje mechi 18 waruhusu goli 36, then mechi 1 waruhusu goli 20.
Si ndo Nikaingia Chimbo!!!!
Ndo kubaini Kumbe wameponzwa na mgomo na hali ngumu ya uchumi!
Wachezaji hawajalipwa mishahara yao!
Mara ya mwisho Wamelipwa agosti 2018
Wakagoma kusafiri!
Benchi la ufundi nalo eti halijalipwa!
Likagoma kusafiri!
Ikawaje?
Ikabidi waende na wale wa timu ya vijana!
Ndio Under 17.
Mechi ikaanza wakiwa wachezaji 7 tuuuuu!
Nikapata shauku zaidi
Ndo nkabaini kumbe hata mechi 3 zilizopita walifungwa bila kucheza!
Ndio, yaani hawakutokea uwanjani
Wakahesabiwa kufungwa 3-0, 3-0, 3-0.
Ilikua dhidi ya Siena, Pro Vercceli na Juventus II
Nikabaini jamaa washakatwa na pointi 8 sababu ya ukata
Unaambiwa kikanuni laiti Leo wasingecheza wangeshushwa daraja!!!
Basi ndo hvyo walianza 7.
Saba wenyewe U17.
Mchezaji wa nane akaingia kipindi cha pili!
Na Huyo unaambiwa hakua na usajili wa kueleweka, wakazozana huko nje wee ndo akaruhusiwa hyo pindi ya pili
Kwenye hao 7 walioanza mmoja ambae alicheza beki ya kati (Central Defender) alikua ni mtaalamu wa Afya wa timu (massaji)
Na yeye hakumaliza mechi aliumia na kutoka zikiwa zimebaki dk 14.
Hata Ulaya Yapo!
Sent using Jamii Forums mobile app