Mambo vipi wadau.
Kitambo sana sijapost pahala hap. Ila niwape pole Mikia Fc kwa kupoteza mechi dhidi ya Morrison FC. Halafu ile freekick ya jamaa imewafanya Viongozi wa Simba wampigie simu Razak Abalora usiku wa Manane. Kwamba ajiandae msimu ujao avae zi wao.
Anyway tuachane na hayo.
Leo nimekuja kuwauliza wadau wa soka la kibongo. Kuwa mmejiandaaje na aibu itakayoletwa na Simba SC kwa mara nyingine tena kwenye tasnia ya soka la Bongo. maana iyo mechi ya jumapili ilibidi Yanga SC waondoke na mabao kama 3 kwa Nunge hivi.
Jamaa wana uchochoro wa ajabu sana uani kwao, hadi najiuliza kwa ubovu wa Yanga SC hii, wanapataje ushindi mzuri kiasi kile. Mikia inabidi mjitafakari kwa mara nyingine tena.
Licha ya ukweli kwamba msimu uliopita mlikuwa na kikosi kizuri zaidi ya cha msimu huu, na bado mliweza kupokea vipigo vya mabao matano matano. Je hivi kwa kikosi hiki dhaifu cha msimu huu mnapanga kufanya nini huko CAFCL kama sio kuendelea kutiana aibu na watu wakaidhalau ligi ya Bongo.
Mimi binafsi naiona kadhia iliyo karibu na kope zangu. kilichotokea nyuma kitajirudia tena na tena msimu ujao wa klabu bingwa.
Uchebe alikuwa na nafsi kubwa ya kuibadilisha timu yenu, Mo akajifanya nae ni mtaalamu wa soka akamsepesha. Huyu naye kishingo ndio usiseme kitu, hata mechi anazoshinda unakuta naye wamemuwekapo kagoli kamoja ka ushkaji.
Muandae pa kuziweka sura zenu, nionacho ni kwamba baadae kidogo ataikimbia timu baada ya vipigo vya kudharirisha Taifa, atajiweka pembeni pia kwa kuona anachokiweka hakiendani kabisa na anachokipata.
Byreeee!
View attachment 1382000View attachment 1382001View attachment 1382002
Hongera kwa Posti yako Nzuri.Nilidhani Mimi ndiyo nimeandika Hii Post.
Hakika umenena, Mo ndiyo Mwenyekiti wa Bodi, Mo ndio Kocha Mo ndio anaamua nani abaki nani asibaki, and the worst he is too immature yani hana akili lakini anajitia anaakili.
Tangu zile post zake za kujiuzulu hakika huyu jamaa namfananisha na Bocco Haram.
Uchebe alikuwa kocha Mzuri, aliandika Taarifa ya Utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 ; taarifa yake ilitaka kikosi kisivinjwe lakini waongezwee baadhi ya wachezaji kuja kutia nguvu.
Mo akaleta u much know, Akashindwa kumbakisha Okwi, Niyonzima na wengineo, Uchebe alimaindi baada ya kuona report yake Mo kaifanya toilet paper.
Akaja na Wabrazili , na Msudani wake. Akaimaliza timu kwa Kumleta kishingo. Mo ndio mchawi Simba na vijisenti vyake vya masimango.
I swear to my ass; Simba Hii haitofika kokote kwenye michuano ya Kimataifa, ingawa wenyewe wanajiamini wana kikosi kipana; lakini mjinga mpe cheo , time will tell na watatolewa na timu ndogo hatua za awali kabisa.
Una plan ku compete na As Vita, Mazembe kwa beki ile ya walevi ? Kwa kipa gani ? Itawachukua not less than 5 years kupata kikosi cha mwaka jana; si mnamsujudia huyo Muhindi;
Timu haina beki ya maana wala kipa wa maana kwa mwaka mzima sasa; timu haina kocha mwenye mbinu na mkakati ; hivi Kishingo ana kazi gani , au yule matola madevu anayeingiza vidole puani Muda wote ( Nose Pick). kishingo ameletwa na Mo kocha ambae Hana background y’a maana ;he is not even competent. Angalia Mazembe; bench lote limetoka ; Yaani unamtoa Uchebe una muacha Udevu Matola Nose Pick , are you guys serious?
Yaani SSC ya leo tukiileta As Vita pale taifa , kwa beki yao na yule pazia la kipogolo linalokaa pale golini zitapigwa nyingi sana.
Mimi naomba wachukue kombe; mara Hii Mo lazima ajiuzulu Maana ana expectation kubwa sana sisi watoto wa mjini tunamcheki tu kwa Sababu tunajua hakuna timu, tumeona Mpira wa Azam , Tumeona mpira wa Yanga.
Upumbavu wa Yanga jana ni kuihofia Simba lakini jana mwananchi alitakiwa atie goli zaid yaa mbili: Sisi tupige Soka, tuwaache wao watumie Muda mwingi kuuza sura social media. Na maviti yao ya Kifahari, sisi tumekaa Kwenye udongo na tumewafunga na tutazidi kuwafunga maana udhaifu wao umeshajulikàna.
Na kombe wachukue lakini wajiandae na matokeo hatua za mwanzo kabisa Out.