Umejiandaaje na anguko la Uchumi Duniani baada ya Corona

Umejiandaaje na anguko la Uchumi Duniani baada ya Corona

Kipindi baada ya corona kuisha kitakuwa ni kipindi selective sana. ni kipindi ambacho kitachagua biashara sana. kitachagua ni biashara gani iliyokuwa hai iendelee kuishi na ipi ife, kulingana na needs and wants za kipindi hicho.

Mostly the needs business ndizo zitasavive eg biashara za mazao,dawa na food industries, the wants business nyingi zitasuffer sana eg transportation (mashirika ya ndege sanasana), clothes ,utalii na wanaotegemea dini.

Kwa waajiriwa ni vyema kujiandaa maana hali ndiyo mbaya zaidi.naona kipindi ambacho kitazaa matajiri wapya wengi sana.
 
Nilifikiri ni huku kwetu.
huu uchumi wetu wa kienyeji (unplanned) hakuna litakaloharibika
Huenda ikawa ni mtumishi wa serikali ndio maana unaongea hivo, hadi sasa Tza kuna watu hawana kaz hotel zimefungwa na nyingne kupunguza watu, sekta ya utalii ishadorora sasa hadi kufikia Julai unafikiri itakuwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Tanzania tuseme ukweli hii great recession ilishaanza muda kama miaka 2 nyuma watu wengi wapo hoi taabani kiuchumi kampuni kibao zilishasepa hapa bongo na zile zilizobaki hali ni mbaya na corona ndio itazimalizia kabisa mfano. mahotel hoi, utalii ndio kabisa serikali pia hali ngumu hakuna afadhali sanasana hili la corona litatuingiza kwenye hali ngumu zaidi.
 
Ungekuja na uzi wa kueleza athari hizo ni zipi hata kwa uchache, kisha utuulize tunajiandaaje kwa athari hizo nadhani ungetusaidia.
 
these people tanzanians are not seriously.😎😎
 
Kwa Afrika ni ngumu hata kuhisi mtikisiko

Jr[emoji769]
Huo ndio ukweli wenyewe!!! Ila kwa ulaya, ndio huonekana mala moja, huku, anguko lisiwepo huwa kama lipo tu!!!! Na maisha yanasonga, utaambiwa kwenye soko la dunia bei ya mafuta imeshuka, lakini huku, huoni tofauti kubwa!! Utaambiwa kwenye soko la dunia bei ya zao fulani imepanda sana!! Huku bei utakayouzia zao hilo ni, ile ile, tena usishangae ukalipwa pungufu zaidi.
 
Wasalamu wana JF...

Natumai ni wazima na mnaendelea kuchukua tahadhari juu ya virusi hivi vya corona vinavyoitesa dunia kwa sasa.

Je ushawahi kaa ukawaza anguko kubwa la uchumi linalokuja baada ya corona!!?

Hii Corona ni kama upepo tu lakini huu mwaka hatuwezi kukwepa GREAT RECESSION. Kirusi kina athari ndogo sana kulinganisha na economics crisis inayofuata baada ya Corona. Soko la hisa la US mpaka sasa limeanguka kwa 24% in less than 2 months. Makampuni yamefunga, wafanyakazi wapo nyumbani, watu wanapunguzwa ajira, hakuna economic activities

Dunia ni kama imesimama, hakuna mzunguko wa pesa, unemployment rate imeongezeka maradufu, Hakuna uwekezaji, hakuna uzalishaji, hakuna consumer spending. Dunia nzima inaosha mikono tu, uchumi umelala. Kama Corona ikigonga na hali ikawa hivi mpaka June, basi tutashuhudia one of the worst ECONOMIC CRISIS in human history.
Naona umem-copy kaka yako Ontario huko Instagram na kuja kui-paste huku,


Ungemalizia na Copy & Paste from Ontario, au ndo ID yako mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom