mkaskaz
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 606
- 865
Binafsi, mwaka 2020 nimejifunza yafuatayo:
1. Kujitegemea hasa kiuchumi. Kuweka mipango thabiti ili kuepuka kuanguka. Mfano hai, mie binafsi ninajua nikianguka huenda nisiweze kuinuka tena kwa haraka. Hivyo niko makini haswaa katika eneo la uchumi ie mapato na matumizi, uwekezaji, nk. Pia, ninamuomba Mungu.
2. Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na vyanzo angalau viwili vya pesa.
3. Unapotaka kuanzisha jambo lako, kelele za kukatishwa tamaa huwa ni nyingi. Ukizisikiliza hutakaa utekeleze mipango yako. Utabaki ulipo.
4. Usimwamini mtu YEYOTE. Ni rahisi mno kwa wanadamu yeyote yule kukubadilikia.
5. Unavyozidi kufanikiwa ndivyo idadi ya marafiki inavyozidi kupungua & at the same time maadui kuinuka.
6. Afya ni mtaji namba 1. Kuna kipindi niliumwa mambo yote yakarudi nyuma. Tangu wakati huo huwa ninamshukuru Mungu kwa kila wakati anaonipa kuwa mzima, lakini pia ninahakikisha ninaepuka vihatarishi vya afya ie kulewa, kuvuta, na vyakula hatarishi (vyenye sukari au mafuta mengi), nk pamoja na kufanya mazoezi angalau mara moja1.
7. Nimejifunza kwamba Maisha ndo haya. Hakuna mengine. Nimejaribu kujiweka mbali na mazingira yanayoniumiza moyo, kutabasamu, kulinda amani yangu, na kutenda wema kwa wengine kadri ninavyoweza bila kutegemea malipo.
NB: Kwa kifupi, haya ni mambo niliyoyaishi 2020. Yapo mengi, lakini ningependa kujifunza kutoka kwa wengine pia. Ahsanteni.