Umejifunza nini 2020?

Umejifunza nini 2020?

mkaskaz

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
606
Reaction score
865
Binafsi, mwaka 2020 nimejifunza yafuatayo:

1. Kujitegemea hasa kiuchumi. Kuweka mipango thabiti ili kuepuka kuanguka. Mfano hai, mie binafsi ninajua nikianguka huenda nisiweze kuinuka tena kwa haraka. Hivyo niko makini haswaa katika eneo la uchumi ie mapato na matumizi, uwekezaji, nk. Pia, ninamuomba Mungu.

2. Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na vyanzo angalau viwili vya pesa.

3. Unapotaka kuanzisha jambo lako, kelele za kukatishwa tamaa huwa ni nyingi. Ukizisikiliza hutakaa utekeleze mipango yako. Utabaki ulipo.

4. Usimwamini mtu YEYOTE. Ni rahisi mno kwa wanadamu yeyote yule kukubadilikia.

5. Unavyozidi kufanikiwa ndivyo idadi ya marafiki inavyozidi kupungua & at the same time maadui kuinuka.

6. Afya ni mtaji namba 1. Kuna kipindi niliumwa mambo yote yakarudi nyuma. Tangu wakati huo huwa ninamshukuru Mungu kwa kila wakati anaonipa kuwa mzima, lakini pia ninahakikisha ninaepuka vihatarishi vya afya ie kulewa, kuvuta, na vyakula hatarishi (vyenye sukari au mafuta mengi), nk pamoja na kufanya mazoezi angalau mara moja1.

7. Nimejifunza kwamba Maisha ndo haya. Hakuna mengine. Nimejaribu kujiweka mbali na mazingira yanayoniumiza moyo, kutabasamu, kulinda amani yangu, na kutenda wema kwa wengine kadri ninavyoweza bila kutegemea malipo.

NB: Kwa kifupi, haya ni mambo niliyoyaishi 2020. Yapo mengi, lakini ningependa kujifunza kutoka kwa wengine pia. Ahsanteni.
 
Nilichojifunza akiba ni muhimu snaa tena sana, kingine aisee tusiogope kukopa ili kufanyia kitu cha muhimu maana kudaiwa hakuuwii kingine usingoje upate pesa nyingi ili ufanye kitu kikubwa Anza na kile ambacho unaisi unaweza kukipata na Anza nacho iwe kuliima, kujenga, kufanya biashara na mengineyo kikubwa uwe umeanza kile ulichodhamiria, kingine nyuchi zinatufilisi sana tupunguze hasa Kwa Sisi vijana maana kuacha au kuwa na mmoja hatuwezi chamwisho ukipata rafiki atakaye kushauri mazuri aisee tembea naye bega Kwa bega
 
Umenena bro mbunye zinturudisha nyuma xn mie nkifkiria kwa hii 2020 huenda nmetumia ata mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kula, kusafir, kulala na mavaz ya hawa viumbe daaaaah 2021 naacha kabisa
......eeee mwenyez mungu nisaidie.
 
Nilichojifunza akiba ni muhimu snaa tena sana, kingine aisee tusiogope kukopa ili kufanyia kitu cha muhimu maana kudaiwa hakuuwii kingine usingoje upate pesa nyingi ili ufanye kitu kikubwa Anza na kile ambacho unaisi unaweza kukipata na Anza nacho iwe kuliima, kujenga, kufanya biashara na mengineyo kikubwa uwe umeanza kile ulichodhamiria, kingine nyuchi zinatufilisi sana tupunguze hasa Kwa Sisi vijana maana kuacha au kuwa na mmoja hatuwezi chamwisho ukipata rafiki atakaye kushauri mazuri aisee tembea naye bega Kwa bega
Nyuchi zinakufilisi kweli kweli ila poa tuu wacha tuzike pesa kwenye papuchi ...sii ndio starehe namba moja hapa duniani.
 
Back
Top Bottom