Umejifunza nini kupitia huu wimbo?

Umejifunza nini kupitia huu wimbo?

Dunia haina huruma, kuna muda unahatarisha maisha yako kwa ajili ya wengine lakini hawatoliona hilo. Binadamu wengi tupo vizuri kuhesabu mabaya ya watu na kuhukumu.
Naamini wewe si miongoni mwao, kadhalika na mimi pia.

Lakini kwa binadamu wengi, unaweza ukamtendea mambo mazuri tisini na tisa, tena mfululizo, na akawa anayafurahia sana. Lakini katika awamu ya mia, ukajikuta umemfanyia jambo ambalo hajalifurahia, labda, jambo ambalo kwa tafsiri yake ni baya japo wewe ulimkusidia jema, anaweza akayasahau yale mema yote 99 na akabaki na kumbukumbu ya hilo moja tu asilolipenda.

Watu ni wepesi kutunza kumbukumbu mbaya kuliko nzuri.
 
Back
Top Bottom