Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 38,283
- 97,793
binafsi jambo nsilopenda kufanyiwa sipendi kulifanya kwa wengine, kuna muda n vyema kuwaelewa watu na mabaya yao kuliko kuhukumu au kuyahesabu.Naamini wewe si miongoni mwao, kadhalika na mimi pia.
Lakini kwa binadamu wengi, unaweza ukamtendea mambo mazuri tisini na tisa, tena mfululizo, na akawa anayafurahia sana. Lakini katika awamu ya mia, ukajikuta umemfanyia jambo ambalo hajalifurahia, labda, jambo ambalo kwa tafsiri yake ni baya japo wewe ulimkusidia jema, anaweza akayasahau yale mema yote 99 na akabaki na kumbukumbu ya hilo moja tu asilolipenda.
Watu ni wepesi kutunza kumbukumbu mbaya kuliko nzuri.
Ndio huwa ipo hivyo unamfanyia mtu mazuri mengi hayaoni ila kosa moja tu unakuwa umeshaharibu yale mazuri yote.