Umejifunza nini kwenye biashara kutoka JF 2017? Weka hapa

Umejifunza nini kwenye biashara kutoka JF 2017? Weka hapa

October man

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2017
Posts
3,635
Reaction score
5,012
Salamu wana jf Kama tunavyoinasibisha Jamiiforums kama shule kwahivyo tumejifunza mengi hususani katika nyanja za biashara na ujasiriamali, nikianza mimi

Nimejifunza vingi ila kimoja wapo ambacho ndonakifanya sasa hivi ni kuwa na nidhamu na pesa hivi navyoandika uzi huu naandika uku nasave 700/= ambapo ilibidi nitumie 1000/= kwenye chakula ila nimebana hiyo kwa kununua chakula ambacho ni cheap kinabana matumizi, hapo mwanzo nilikuwa sina nidhamu hata kidogo kwa siku nilikuwa natumia hata 3000/= mpaka 4000/=

Muda mwingine kwa kula tu na muda mwingine kutumia vitu ambavyo havipo kwenye ratiba kama kununua nguo bila kuwa na ratiba nayo kwa sasa hivi nina uwezo wa kutumia 1300/= kwa siku si kwamba nina shinda na njaa ila naweza hivyo kwa kutojali quality ya chakula bali quantity yake mfano

Kwa mazingira nayoishi hasahasa usiku mtu unakuwa huna njaa sana kwaiyo unaweza kula wali mchana arafu usiku ukala ata mkate wa 1000= ambao unaweza kuula kwa siku tatu usiku tu na ukawa umeshiba fresh tu ila siku ukiona mambo sio unatumia 2000/= ambapo mchana wali 1000/= na usiku wali 1000 /=

Kwahiyo kwa sasaivi nimepunguza vitu na vyakula luxuries nilikuwa Karanga za mayai zinanimalizia pesa sasahivi nimeziepuka na pia soda nimeziepuka ninamalengo yakufanya hivi sio kwamba nafanya tu

NB: Naishi campus kwahiyo ni kwa siku unakula milo miwili si mitatu kwa wanaishi campus wanajua

Weka chochote hapa ulichojifunza hapa kutoka jamiiforums focus kubwa ikiwa kukuretea maendeleo
 
Chanzo Kikuu cha Habari maishani mwangu..

Uchambuzi wa hoja na uwasilishwaji wa maoni binafsi

Kikubwa watu wengi humu hatuuelewi uongozi Ulipo Madarakani
 
Jf imeniingiza kwenye ulimwengu wa kusoma vitabu. Bila jf nisingejua vitabu vingine natumai mwaka huu ni wa vitendo na sio blah blah.
 
Back
Top Bottom