Umekariri number ngapi za simu kichwani mwako?

Raymanu KE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
8,611
Reaction score
16,118
Najua wanawake especially wasichana wapo vizuri Sana kwenye hili.Hawa viumbe Wana uwezo wa kukariri number za simu kama Mia hivi kwenye vichwa vyao bila shida yoyote.Yaani anaweza akakutajia hizo number off- head bila kurefer popote.

Kimbembe kipo kwetu wanaume Sasa.Binafsi siwezi kariri number zaidi ya 5 kwenye kichwa changu.Imagine nimekariri number 4 tu kwenye kichwa changu.Ya maza, dada yangu mdogo,ya rafiki yangu mmoja na ya mchumba wangu.Baasii!

Aibu inakujaga pale mtu anapokuja kuniomba number ya dingi wangu afu kwa Bahati mbaya niwe Sina simu.Hiyo number walae ataenda kutafuta kwingine maana hapo nitakuwa nimechemka siwezi msaidia kbsa.Naye baba yangu najua hajakariri number zangu kichwani mwako.

Shida nyingine kubwa Sana Ni pale mtu anapoenda sehemu ya mbali na nyumbani afu kwa bahati akakutwa na tatizo kubwa ambalo linahitaji kutatuliwa na watu wa nyumbani.Ukute mhusika Hana simu na Wala hajakariri number yoyote hata Moja ya watu muhimu tuseme wazazi,ndugu jamaa na marafiki.Huyu Sasa maybe atokee msamaria mwema tu amsaidie Vinginevyo......

Jamani especially wanaume tujitahidini katika kukariri number za simu za watu walio muhimu Sana kwetu( wazazi,ndugu na marafiki) bila ya kufanya reference kwenye simu zetu.Hili litatusaidia Sana coz kuna muda tutazikosa simu zetu mikononi mwetu.

Ahsanteni.
 
Mimi hata ya kwako ukinipa mda huu naikariri.
Ni kitu ambacho sikipendi ila huwa inatokea.
 
Mimi hilo huwa halinishangazi kinachonishangaza password za mitandao huwa nasahau ila sijawahi kusahau password za maswala ya helahela mfano PayPal huwa ni nadra sana kuitumia inaweza chukua hata miezi ya kutosha ila password yake inakujaga vizuri tu..😂

Hela tamu nyie asikuambie mtu!.
 
Nina no 2 nimekariri moja, hiyo nyingine imegoma kukaa kichwani.

Nyingine nilizokariri ni za wazazi na ndugu yangu mmoja basii
 
Nina no 2 nimekariri moja, hiyo nyingine imegoma kukaa kichwani.

Nyingine nilizokariri ni za wazazi na ndugu yangu mmoja basii
Acha uvivu mkuu, jitahidi ukariri japo number 50
 
Siku ukipatwa na tatizo afu uwe hauna simu mikononi mwako utafanyaje mkuu?
 
Mama,mdogo wangu na binti yangu wa kaz aliyenilelea my first born
 
me binafsi sina desturi ya kusave no kwenye phone naonaga uvivu hatari so nacho fanya ni kukariri inavyoishia.

mfano ya dem wangu inashia na 84 ko nikiona simu imepigwa inaishia 84 najua huyu ni fulani
mpka ni save no yko basi mvua itakua imenyesha cku hyo.
no nilizo save ni chache mno, kuzikariri ni shida kwangu
 
Kichwani kwangu nna namba zifuatazo:
1. Ya mke wangu
2. Ya mama yangu mzazi
3. Ya mama mkwe
4. Ya dada yangu
5. Ya mdogo wangu wa kiume mmoja, wa pili toka mwishoni
6. Ya mtoto wangu wa kiume
 
huko kama mimi aisee ila sema siku wametu rahisishia
 
Ukiachana na zangu ..Nimekariri ya Dada angu na Mdogo wangu wa mwisho.
 
Siku ukipatwa na tatizo afu uwe hauna simu mikononi mwako utafanyaje mkuu?
Hakuna mahali nimeandika sijakariri namba ya mtu mkuu naachaje kukariri dunia ambavyo haiaminiki hii..😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…