Hakuna jamii yeyote Duniani ambayo kuna usawa kwenye kila kitu. Hata hapa Marekani watoto wa George H Bush wamekuwa maarufu na kuwa Governors na mmoja Raisi kwasababu babu yao alikuwa tajiri, baba akawa tajiri akaweza kuwasomesha shule nzuri sana na kuwapa elimu bora. Hii haina maana kwamba hawa watoto ambao wamekuja kuwa Maraisi wanavipaji kuliko wengine lakini wameweza kupata fursa ambazo ni ngumu kupata mtoto wa masikini.
Hii hipo sehemu nyingi sana. Yule mtoto wa Kikwete ingewezekana asiwe lawyer kama angezaliwa Mtwara vijijini kwa familia masikini lakini haibadilishi ukweli kwamba mtoto wa Kikwete kamaliza Chuo Kikuu cha Dar law school. Na kwakutumia hili huwezi kusema mtoto wa Kikwete ambaye kamsomesha ni sawa tu na yule ambaye hajapata elimu kijijini kwasababu wana vipaji vya kuzaliwa sawa!
Kwa namna hii huwezi kuacha kutangaza shule na matokeo kwasababu tu wanafunzi wengi wa shule hizo na walimu wanapitia magumu sana kulinganisha na wengine.
Mimi mfano nilisoma Ilboru O-level wakati tulivyokuwa Ilboru watoto wa kutoka Arusha School walikuwa wanatuzidi mwanzoni kwasababu ya mazingira yao lakini sisi tuliongeza jitihada na kulingana na hata kuwapita. Huwezi kutumia kisingizio hiki kuacha kutangaza ukweli. Sasa ina maana tutaanza kupeleka watoto kusoma Udaktari ambao hawajafaulu? Au kuendesha ndege ambao hawajafaulu kwasababu kama hizi?
Wabunge wamekuwa kama vilaza anadanganya eti utaratibu wa kupima na mitihani haupo popote. Si kweli. Shule zinapimwa na mitihani hapa USA ndiyo hivyo. Sasa tutaanza kupima watu kwa background! huu ni uongo.