[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]Asante mkuu kwa kutuhamasisha,, ila chakuongezea hapo tunda linaliwa kabla ya kupiga menu kubwa. Maana ukila baada ya msosi kuna enzymes zinakuwa zimeshaachiwa ambazo kuzuia uyeyushaji wa vitamin C. Kwa hiyo unaweza kukosa hiyo vitamin ya muhimu kabisa inayopatikana kwenye matunda. Kwa hiyo basi tupige tunda angalau nusu saa kabla ya kupiga menu!
Ninakula machungwa sana, kila siku.Kwa hakika kama kuna mtu kati yetu asubuhi ya leo kala tunda lolote lile basi ni wale waliolala zile hotel zenye bed n breakfast full course. Wengine wetu kwa uchache mno ni wale wafanya diet na kwa uchache zaidi wale wanaotambua umuhimu wa matunda mwilini kiafya. Wengi wetu humaliza mpaka wiki bila kula hata kipande kimoja cha tunda lolote.
Wengi huwa hawali matunda mpaka waandikiwe na daktari kama sehemu ya tiba. Kwao kula tunda ni sehemu ya anasa na kupoteza pesa..
Matunda yana faida kubwa mwilini kiafya kuliko hata nyama. Matunda ni sehemu muhimu ya tiba. Matunda yana uwezo wa kukujenga kiafya na kukukinga na maradhi mengi. Ni afadhali mara mia ukala matunda ya buku kuliko kula mchemsho wa buku 2, Matunda ni tiba ya magonjwa mbalimbali.
Matunda ni sehemu muhimu ya tiba mbadala na ujenzi wa mwili imara na wenye nguvu.
Baadhi yetu hupendelea shurubati zaidi kuliko matunda yenyewe. Ni sawa pia lakini shurubati isiyo halisi inakuwa imechanganywa na vionjo vingine hivyo kupunguza kwa kiasi fulani nguvu ya kutenda.
Huu ni ushauri wangu kwako pamoja na kunywa maji mengi na kupangilia milo yako lakini usisahau kitu hiki muhimu sana TUNDA. Jitahidi kupata kipande cha tunda kwenye kila mlo wako.. kuna siku utanikumbuka na kunishukuru kimoyomoyo
Je, umekula tunda gani leo?
Duh mkuu hiyo kitu sijawahi sikia ndio kwanza nasikiaIll lisikupe shida ya meno,liwekee chumvi kiasi
Sawa mkuu ngoja mida nipandishe zangu sokoni nikachukue nanasi nifanye kama unavyosema hili nione hali ikoje likinishinda nitalipika kabisa mixka naweka na viungo alafu ntakula kama mboga[emoji14][emoji14]Please jaribu iko poa sana..ukishamenya nanasi liloweke kwenye chombo chenye maji yenye chumvi kiasi kama dakika 5,10 kisha kula
Yan acha tu ila ngoja nijaribu nione testi yake mana kila siku tunajifunza japo tumemaliza shuleChumvi tena si utaharibu taste ya nanasi jamani achana na huo ushauri mkuu[emoji3]
Hadi huo ulozi ni uumbaji jamani?? Huo ni binadamu mmejiongeza bana. Ila kweli😀😀Vyote chini ya jua ni uumbaji wake[emoji3]
Duh[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Sawa mkuu ngoja mida nipandishe zangu sokoni nikachukue nanasi nifanye kama unavyosema hili nione hali ikoje likinishinda nitalipika kabisa mixka naweka na viungo alafu ntakula kama mboga[emoji14][emoji14]
Ni nzuri sana kuliko sana yenyewe na utaifurahia na hutoiachaDuh mkuu Iyo kitu sijawai sikia ndio kwanza nasikia
Ndo pale husemwa elimu haina mwisho,ukishakata vipande ukiona tabu kuliloweka kwenye maji chumvi basi chukua chumvi nyunyuzia nyunyuzia kwa juu kama unavyonyunyuzia kwenye nyama chomaYan acha tu ila ngoja nijaribu nione testi yake mana kila siku tunajifunza japo tumemaliza shule