Umekula tunda gani leo?

Umekula tunda gani leo?

Ni tunda la msimu kula tani yako..hakuna shida kiafya lakini kiimani tunafundishwa kuwa na KIASI kwenye kila kitu...Madhara mengine labda kuvimbiwa[emoji23]
😁😁Hapo kwenye imani niko vizuri sijavimbiwa Doctor! Na Bado mwili unadai niendelee kula tu ila meno hayana ushirikiano kabisa😬. Thank you
 
Kwa hakika kama kuna mtu kati yetu asubuhi ya leo kala tunda lolote lile basi ni wale waliolala zile hotel zenye bed n breakfast full course. Wengine wetu kwa uchache mno ni wale wafanya diet na kwa uchache zaidi wale wanaotambua umuhimu wa matunda mwilini kiafya. Wengi wetu humaliza mpaka wiki bila kula hata kipande kimoja cha tunda lolote.

Wengi huwa hawali matunda mpaka waandikiwe na daktari kama sehemu ya tiba. Kwao kula tunda ni sehemu ya anasa na kupoteza pesa..

Matunda yana faida kubwa mwilini kiafya kuliko hata nyama. Matunda ni sehemu muhimu ya tiba. Matunda ya uwezo wa kukujenga kiafya na kukukinga na maradhi mengi. Ni afadhali mara mia ukala matunda ya buku kuliko kula mchemsho wa buku 2 Matunda ni tiba ya magonjwa mbalimbali.

Matunda ni sehemu muhimu ya tiba mbadala na ujenzi wa mwili imara na wenye nguvu.
Baadhi yetu hupendelea shurubati zaidi kuliko matunda yenyewe. Ni sawa pia lakini shurubati isiyo halisi inakuwa imechanganywa na vionjo vingine hivyo kupunguza kwa kiasi fulani nguvu ya kutenda.

Huu ni ushauri wangu kwako pamoja na kunywa maji mengi na kupangilia milo yako lakini usisahau kitu hiki muhimu sana TUNDA. Jitahidi kupata kipande cha tunda kwenye kila mlo wako..kuna siku utanikumbuka na kunishukuru kimoyomoyo
Je, umekula tunda gani leo?

Mimi nimekula tunda la kati pale. Ni tamu sana hilo tunda.
 
Ahsante kwa ushauri mzuri na kutukumbusha! Je ukila nanasi lile kubwa zima ni vizuri kiafya ama nimejioverdose? Maana nimekula hadi meno yanauma hapa[emoji16]
Kipande tu FS, labda kama unakula matunda tofauti..pata kipande cha nanasi, kipande cha embe, ndizi moja/kipande nk....pia kula sana mbogamboga, usisahau bamia na nyanya chungu kwa afya ya naniliu[emoji39][emoji39]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] we upo ka mm uwa naligonga peke angu mpk amu iniishe ila nikimaliza mimeno yote miganzi
šŸ˜‚šŸ˜‚Yaani sijaamini kama ndiyo namalizia kipande cha mwisho cha nanasi zima kubwa! Lilikua poa sana tatizo meno sasašŸƒā€ā™€ļø
 
Kitu Cha tikiti[emoji525]
Tikiti maji na nguvu za kiume

Tafiti za karibuni zinasema karibuni zinaonyesha kila wanaume watatu mmoja na ana tatizo la kupungua kwa nguvu za kiume na dalili zinaonyesha idadi itaongezeka mara mbili miaka ya karibuni.

Kwa bahati nzuri madaktari na watafiti mbalimbali wameendelea kufanya utafiti juu ya suluhisho la tatizo hili kwa njia salama zisizo na madhara mengine baadaye.

Tikiti maji linasemwa kuwa ni mkuyati wa asili pia kama lilivyo parachichi. Kwenye tikiti maji kuna vitu hivi vitatu mhimu sana kwa afya ya mapenzi navyo ni ā€˜lycopene’, ā€˜beta-carotene’ na ā€˜citrulline’ ambavyo husaidiwa kuweka mishipa ya damu katika hali ya utulivu.

Tikiti maji ni viagra ya asili inayoweza kutumika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa watu wa jinsia zote mbili bila kukuacha na madhara yoyote mabaya.

Kwenye tikiti maji hasa mbegu zake kuna kitu kingine kinaitwa ā€˜L-arginine’ ndicho ambacho huhusika na kuongeza nguvu za kiume. Mbegu za tikiti maji zimeonyesha matokeo mazuri katika kuimarisha nguvu za kiume hata kwa wazee kabisa.

Unachohitaji ni kula tikiti maji kila siku sambamba na mbegu zake na hutakawia kuona tofauti.

Faida nyingine 27 za tikiti maji kiafya

Asilimia 92 yake ni maji
Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili
Huponya majeraha
Hukinga uharibifu wa seli
Huboresha afya ya meno na fizi
Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
Hubadilisha protini kuwa nishati
Chanzo cha madini ya potasiamu
Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la juu la damu
Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
Huondoa sumu mwilini
Huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake
Tunda zuri kwa mwenye Kisukari aina ya pili
Husafisha figo
Huzuia na kutibu kansa mbalimbali
Tunda zuri kwa mwenye ugonjwa wa moyo
Huzuia na kutibu pumu
Hutibu tatizo la kufunga choo
Hufanya ngozi ing’ae
Huhamasisha kuota nywele
Husaidia kupunguza uzito
Huimarisha mifupa
Husaidia kuponya vidonda na majeraha
Huzuia madhara yasitokee katika seli
Huzuia ugonjwa wa baridi yabisi ya moyo (heart stroke)
Hutibu kiseyeye (scurvy)
 
Kipande tu FS, labda kama unakula matunda tofauti..pata kipande cha nanasi, kipande cha embe, ndizi moja/kipande nk....pia kula sana mbogamboga, usisahau bamia na nyanya chungu kwa afya ya naniliu[emoji39][emoji39]
Ahsante Eli ntazingatia hayo ila umesema bamia na nyanya chungu ni kwa afya ya nini?.. sipendi mabamia! Ila nyanya chungu poa šŸ¤”
 
Kuna hawa jamaa...
Wanaweka Kila
šŸ‡šŸˆšŸ‰šŸŠšŸ‹šŸŒšŸšŸŽšŸšŸ’šŸ“šŸ…šŸ„„šŸ„‘šŸ„• aina ya tunda ndani ya ' conterna'šŸ± sahani ndogo za mfuniko
Wanauza tsh 1000 ,2000

Huwa napiga conterna' zangu mbili na jagi la maji ..
 
Mganga Mshana atakupa dondoo za faida za bamia na mlenda kwa afya ya naniliu[emoji39][emoji39][emoji39]
Bamia ni mboga maarufu hapa Tanzania, na watu wengi wamekuwa wakiichukulia mboga hiyo kama ya watu wenye uwezo mdogo kiuchumi. Sasa leo yafahamu magonjwa yanayoweza kutibika kwa kula bamia.
[https://www]
1-Pumu.

Bamia ina Vitamin C ambayo inawafanya watoto wanaougua ugonjwa wa pumu, kupumua vizuri wanapotumia bamia. Nusu kikombe ya Bamia iliyopikwa huwa ina miligramu 13 ya vitamin C.

2-Msongo wa mawazo (Depression).

Bamia ni mboga bora zaidi kwa wale wanaoshambuliwa na msongo wa mawazo, unywaji wa kikombe kimoja cha supu yake huimarisha nguvu ya ufanyaji kazi wa ubongo.

3-Hupunguza Chorestol mwilini.

4-Bamia unasaidia kumarisha kiga ya mwili na mfumo wa uonaji mwilini.

5-Bamia inasaidia kutibu tatizo la kukosa choo.

6-Bamia inatibu vidonda vya tumbo.

Bamia husaidia kuweka utumbo kuwa na hali nzuri hivyo kupunguza uwezakano wa kuugua vidonda vya tumbo kwani inasaidia kusawazisha asidi mwilini.

7-Kuimarisha afya ya nywele.

8-Inasaidia kusawazisha sukari mwilini kwa wale wanaougua ugonjwa wa kisukari.

9-Inasaidia kutibu magonjwa mbalimbali ya zinaa kama Kisonono, kaswende n.k .

10-Ni kinga dhidi ya utamiamlo (Unene uliopitiliza).

Faida hizi ni kwa mujibu wa majarida mbalimbali ya afya duniani, na bamia inatajwa kuwa ni moja ya mboga za majani zenye faida nyingi zaidi duniani.
 
Back
Top Bottom