Umekula tunda gani leo?

Umekula tunda gani leo?

FAIDA ZA NDIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU

TOFAUTI na vyakula vingine, ndizi zinafaida kubwa sana katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, ndizi zina virutubisho vya aina mbalimbali kama vile, protini, mafuta, kalishiamu, wanga, fosiforas, madini ya chuma, vitamin A,B,C na maji.
Ndizi zina faida zipi katika urembo? Chanzo cha nishati Ndizi zina uwezo wa kumeng’enywa kwa urahisi zaidi, tena zina nishati kubwa, sukari iliyomo katika ndizi ni chanzo kizuri sana cha nishati.
Hivyo naweza kusema kuwa ndizi ikiliwa ipasavyo itakusaidia kujenga mwili na misuli yako kwa ujumla. Husaidia kuondoa chunusi Chunusi ni miongoni mwa matatizo ambayo huwasumbua warembo wengi hususan wanawake.
Je, unafahamu kuwa ndizi mbivu zinaweza kukuondolea tatizo hilo? Kwa kuchanganya ndizi mbivu na maziwa na asali na kisha kuzisaga ili kupata urojo ambao utatumia kupaka kwenye maeneo yaliyoathirika, unaweza kuondokana kabisa na tatizo hilo.
Fanya hivyo kila siku na hakikisha unakaa na mchanganyiko huo kwa muda usiopungua dakika 30 hadi 40, kisha osha na maji ya baridi ikiwezekana yaliyopozwa na jokofu.
Ndizi katika ‘diet’ Ndizi zina nafasi kubwa sana kati kuongeza au kupunguza uzito, hivyo unaweza kutumia ikiwa unahitaji kupunguza ama kuongeza uzito wako.
Kwa wajawazito Ndizi ni chakula kizuri kwa wanawake wajawazito, kwani kina kiwango kikubwa cha ‘folic acid’ ambayo inaweza kufyonzwa kwa urahisi sana na kiumbe kilicho tumboni. Ikiwa mama mjamzito atatumia ndizi mara kwa mara ni wazi kuwa atakuwa mwenye muonekano mzuri na wa kuvutia.

1.
Ni kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, presha, vidonda vya tumbo, saratani ya figo, kukosa choo
Ndizi mbivu ni tunda ambalo linafahamika na kila mtu, lakini sina hakika kama watu wengi wanafahamu umuhimu na faida za tunda hili ambalo linapatikana kirahisi sana nchini. Bei yake ni kati ya shilingi 50 na 150 tu, kiwango cha pesa ambacho kila mtu anaweza kukimudu.
Iwapo ulikuwa hujui umuhimu wa kula ndizi mbivu, leo utalazimika kubadili mtizamo wako na kuziangalia ndizi kama tunda muhimu katika kuupa nguvu na kuulinda mwili wako dhidi ya maradhi hatari ambayo hayana tiba. Watu wa michezo pia wanapaswa kuliona tunda hili kuwa ni muhimu sana katika kuipa miili yao nguvu.

KINGA DHIDI YA SHINIKIZO LA DAMU NA MARADHI YA MOYO
Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi, ndizi ni chanzo kikubwa cha Potassium, madini ambayo ni muhimu sana katika kuweka shinikizo la damu mwilini katika hali yake ya kawaida (Normal Blood Pressure), na ufanyaji kazi mzuri wa moyo. Kwa kuwa ndizi moja ina wastani wa 467mg za madini aina ya Potasiamu na 1mg ya sodiamu (chumvi), ndizi moja tu kwa siku inaweza kukupa kinga ya maradhi ya shinikizo la damu na matatizo ya moyo.
Ukweli kuhusu vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya Potasiamu katika kushusha shinikizo la damu mwilini, umethibitishwa na tafiti nyingi za kisayansi. Kwa mujibu wa jarida moja la masuala ya afya nchini Marekani, zaidi ya Wamarekani 40,000 wa kike na kiume, walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka minne na ikagundulika kwamba watu wanaokula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha madini ya Potasiamu na kirutubisho cha Fiber (Ufumwele), wako katika hatari ndogo ya kupatwa na kiharusi.
Aidha, utafiti mwingine uliofanywa na taasisi moja ya masuala ya tiba ijulikanayo kama Archives of Internal Medicine, ya nchini Marekani, pia ilithibitisha kwamba ulaji wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha ufumwele (fiber) kama vile ndizi, husaidia sana kutoa kinga dhidi ya maradhi ya moyo. Na katika suala hili, zaidi ya watu 10,000 walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka 19.

KINGA DHIDI Y VIDONDA VYA TUMBO
Kwa muda mrefu sana imethibitishwa kwamba ndizi ina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na asidi tumboni hivyo kutoa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo (stomach Ulsers) na kutoa ahueni kwa mtu ambaye tayari ameathirika. Katika utafiti mmoja, ilkibainika kwamba mtu akila mchangayiko wa ndizi mbivu na maziwa freshi, huzuia utokaji wa asidi tumboni inayosababisha vidonda vya tumbo.
Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi juu ya suala hili, ndizi hutoa kinga na ahueni ya vidonda vya tumbo kwa njia mbili. Mosi: virutubisho vilivyomo kwenye ndizi huzipa uhai seli zenye kazi ya kutengeneza utandu ambao hutoa aina fulani ya urojo (mucus) unaotumika kama kizuizi dhidi ya asidi tumboni.
Pili: kuna virutubisho vingine kwenye ndizi ambavyo kwa kitaalamu vinajulikana kama ‘Protease’ ambavyo husaidia kuondoa bakteria tumboni ambao wanaelezewa kuwa ndiyo chanzo cha vidonda vya tumbo. Hivyo kama wewe hujaptwa na vidonda vya tumbo, kwa kula ndizi mara kwa mara unajipa kinga madhubuti na kama tayari umeathirika na vidonda, kwa kula ndizi utajipa ahueni kubwa.

NDIZI KAMA TIBA KWA WENYE MATATIZO YA CHOO
Ndizi ni muhimu sana katika kulainisha na kusafisha tumbo na kumuwezesha mtu kupata choo. Mbali ya kusaidia upatikanaji wa choo kwa wenye matatizo hayo, lakini pia hutoa ahueni kwa wagonjwa wa kipindupindu. Mtu aliyepatwa na kipindupindu hupoteza kiasi kikubwa cha madini ya Potasiamu, hivyo kwa kula ndizi ataweza kurejesha mwilini maidni yake yaliyopotea na kuupa mwili nguvu yake.
UIMARISHAJI WA NURU YA MACHO
Wakati ulipokuwa mdogo, bila shaka uliwahi kuambiwa na mama kuwa mtu akila karoti, atakuwa akiona vizuri. Bila shaka hakukosea, lakini sasa ukiwa mtu mzima unaambiwa kwamba ulaji wa matunda, ikiwemo ndizi, ndiyo kinga hasa dhidi ya matatizo ya kutokuona vizuri uzeeni. Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kwamba ulaji wa matunda kwa wingi kila siku, hupunguza kwa asilimia 36 matatizo ya kutokuona vizuri kutokana na mtu kuwa na umri mkubwa.

KINGA DHIDI YA SARATANI YA FIGO
Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Jarida la Kimataifa la masuala ya Saratani (International Journal of Cancer) la nchini Marekani, umeonesha kwamba ulaji wa mara kwa mara wa matunda halisi, hasa ndizi mbivu, ni kinga madhubuti ya mwili. Zaidi ya wawake 50,000 wenye umri kati ya miaka 40 na 76 waliofanyiwa utafiti, ulionesha kuwa wale waliokula wastani wa milo 2.5 ya matunda na mboga kila siku, walipunguza hatari ya kupatwa na saratani ya figo kwa asilimia 40.
Baadhi ya vitamini na madini yaliyomo kwenye ndizi ni pamoja na Vitamini B6, Vitamin C, Potassium, Dietary Fibre na Mnganese. Hivyo utaona kwamba tunda la ndizi ni muhimu kwa sababu limesheheni vitamini na madini muhimu katika mwili wa binadamu. Kuanzia leo itazame ndizi kama tunda muhimu sana katika ustawi wa afya yako na ni kinga dhidi ya maradhi unayoweza kuyaepuka kesho kwa kula tunda hili kwa wingi leo!
Nimesomaa, mwishoni nimetafuna ndizi... Shukrani kwa andiko hili
 
Suala la Afya bora ni suala la muhimu sana katika Maisha ya kila mmoja wetu na taifa kwa ujumla. Bila afya hakuna furaha,amani wa shughuli yoyote ile ya maendeleo.Afya ndio msingi wa maisha yetu ya kila siku.Siku hizi si ajabu sana kusikia au hata kushuhudia watu wengi wakisumbuliwa na matatizo mengi sana ya kiafya, suala hili linachangiwa na mambo mengi hali ya mazingira au tabia za watu.

Upuziaji wa matumizi ya matunda na mboga mboga unachangia kwa kiasi kikubwa matatizo ya mengi ya kiafya. Matunda ni moja ya zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu binadamu tuliopewa japo tunaidharau licha ya faida yake katika maisha yetu.

Kuna sababu kadhaa za kwa nini watu hawatumii matunda mara kwa mara , baadhi ya hizo ni Kutokujua faida ya matunda kiafya, na Ukosefu wa uwezo wa kumudu gharama za kula matunda mara kwa mara. Ikiwa wewe ni miongoni mwa watu wanaoshindwa kutumia matunda kwa moja ya sababu hizi basi taarifa hii inakuhusu na uyajue matunda yenye gharama nafuu sana wakati huo huo yakiwa na faida tele kiafya kwa mwili wako.

#1.

MACHUNGWA


grapefruit

Haya ni matunda matamu sana ,rahisi sana kupatikana na yenye faida nyingi mno kwa afya yako.Matunda hayab hupatikana kwa wingi bila gharama kubwa mfano kwa wale waliofika Morogoro na Tanga wanajua uwingi wa matunda haya. kama hujui tazama virutubisho muhimu sana viliyomo katika machungwa.

Vitamin C __________________ 93%
Fiber __________________ 13%
vitamini B1 __________________ 9%
Pottasium __________________ 7%
Calcium ___________________ 5%
Na virutubisho vingine vingi sana huku vikiwa na faida muhimu zaidi ikiwemo:

Vitamic C ya machungwa husaidia kuimarisha ulinzi wa Antioxidant na ulinzi dhidi ya magonjwa
Machungwa husaidia kuzuia ugonjwa wa mawe katika figo(kidney stones)
Machungwa huzuia kansa na vidonda vya tumbo
Machungwa husaidia na kuboresha afya ya mfumo wa upumuaji.
Yapo mengi na faida nyingi sana za machungwa …Machungwa sio gharama ,ni rahisi kupatikana yatumie mara kwa mara uone faida yake kwa afya yako.

#2.

NANASI


pineapple.jpg

Nanasi ni tunda maarufu na linalopatikana karibu maeneo yote kwa urahisi.Tunda hili lina virutubisho vya kusaidia ubora wa afya yako.Baadhi ya faida ya nanasi ni;

Husaidia kwa kiasi kikubwa ulinzi wa mwili.
Husaidia seli na tishu mwilini kwa vitamini c iliyomo katika tunda hili suala linalopelekea kujengwa kwa sehemu muhimu ya protini iitwayo COLLAGEN ambayo huimarisha mishipa ya damu,ulinzi wa ngozi,ogani na mifupa mwilini.
Husaidia sana kukukinga na kansa kwa kuupatia mwili wako vitamini A na C zenye uwezo mkubwa wa kupambana na kansa mwilini.
Nanasi ni tunda lenye faida kubwa sana mwilini mwako hizo ni chache kati ya nyingi, hivyo tumia fursa ya gharama ndogo ya matunda haya kwa faida ya afya yako.

#3.

PARACHICHI


avocado.jpg

Parachichi ni tunda rahisi sana kupatikana hasa sehemu za baridi. Watu wanaoishi maeneo haya wana ushahidi juu ya hili.Huuzwa nchi nzima kwa bei ndogo na ya kawaida kabisa huku likiwa na faida kubwa sana kiafya.Baadhi ya virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye tunda hili ni;

Vitamini K __________ 26%
Folate __________ 20%
Vitamini C __________ 17%
Potassium __________ 14%
Vitamin E __________ 14%
Vitamin B5 __________ 14%
Vitamin B6 __________ 13%
Kwa orodha ya virutubisho hivyo hapo juu Parachichi litasaidia sana mwili wako kurekebisha msukumo wa damu, Tunda hili lina 77% ya protini kitu kinachofanya tunda hili liwe mmea wenye protini kuliko mwingine wowote ule.Husaidia macho kuona vizuri zaidi, zaidi husaidia nywere na ngozi yako, Na faida nyingine nyingi sana.Hauna budi kutumia parachichi mara kwa mara.

#4.

PAPAI


paw-paw

Papai ni moja ya tunda zuri,tamu likiwa vilevile linapatikana kwa urahisi na gharama nafuu.Kama ulikuwa hujui faida za papai kwa afya yako ngoja nikuibie siri. Papai ndio tunda lenye utajiri wa madini mengi sana ukilinganisha na matunda mengine pamoja na virutubisho vingine vingi.Baadhi ya faida za tunda hili ni kama vile;.

Husaidia sana kupunguza uzito (weight loss), Ikiwa kila nusu kipande kikiwa na Calories 120.Tunda hili ni la muhimu sana kwenye suala la kupunguza uzito …kama unashida ya uzito usiotakiwa tumia tunda hili mara kwa mara litakusaidia sana.
Husaidia sana kinga ya mwili kwa zaidi ya 200%.Utajiri wa Vitamini C papai lililonao husaidia kinga ya mwili kuwa imara pindi unapotumia mara kwa mara.
Ni tunda nzuri kwa wagonjwa wa kisukari.Papai lina kiwango kidogo cha sukari(8.3 gram kwenye kikombe cha papai zilizokatwakatwa vipande vidogo).Juisi yake ni nzuri sana kwa sukari huku ikiwa na Vitamini nyingi zenye kusaidia mgonjwa wa sukari kuepukana na magonjwa ya Moyo.
Faida za papai ni nyingi sana ,Husaidia kurainisha na kurinda ngozi,husaidia macho kuona vizuri,huasidia mfumo wa usagwaji wa chakula mwilini n.k, hivyo litumie mara kwa mara.





#5.

EMBE


mango

mangos

Tunda hili ni maarufu na rahisi sana upatikanaji wake huku likiwa na bei ya kawaida sana.Maeneo kama ya mubende, kampala, Tommy, kent,mashamba ya Capsicum ,Embu ishiara ,karurumo,Tabora, Tanga, Morogoro, Kigoma, na maeneo mengine mengi sana ya Afrika mashariki, tunda hili hulimwa na kustawi kwa wingi sana. Licha ya hilo bado watu wanapuuza kutumia tunda hili kiafya, Ila wewe unatakiwa ujue faida za tunda hili mfano,

Linasafisha ngozi, linaimarisha sana afya ya macho.
Lina virutubisho venye Antixiodant vinavyosaidia kukukinga na kansa kwenye mwili wako.
Hongeza hamu ya tendo la ndoa na nguvu za kiume.
Kubwa zaidi hukuepusha na ugonjwa wa mshituko wa moyo (heart stroke)
Ni baadhi ya faida chache na muhimu sana kwa ajiri ya mwili wako …. Jenga mazoea ya kula maembe kwenye milo yako na ufurahie afya bora.



#6.

NDIZI


banana.jpgNdizi ni tunda maarufu sana lenye faida tele kwa mwili wako huku likipatikana kwa gharama ndogo na kwa urahisi. Ndizi ina virutubisho vingi venyefaida nyingi sana kwa afya yako ikiwemo.

Potassium ______________ 9%
Vitamin B6 ______________ 33%
Vitamin C ______________ 11%
Protein _______________ 1.3 grams
Fat _______________ 0.4 grams
Na vingine vingi sana kiasi cha kutotaja vyote huku vikiwa na faida kwa mwili wako kama vile,

Kurekebisha kiasi cha sukari mwilini (ndizi ina Kalories 105 pekee).
Inapunguza uzito usiotakiwa (weight loss).
Potassium iliyopo kwenye ndizi Inaboresha afya ya moyo.
Husaidia Insulin na figo kufanya kazi vizuri .
Na faida zingine nyingi sana hupatikana kwa kutumia ndizi mara kwa mara.



#7.

TIKITI MAJI



Tikiti maji naamini ni tunda linalofahamika na watu wengi sana ,Tunda hili licha ya watu wengi kutokujua lakini lina faida nyingi mno kiasi cha kushauriwa kutumika mara kwa mara na wadau mbalimbali wa masuala ya afya. Hizi ni baadhi ya faida muhimu sana za tunda hili

Pamoja na tikiti maji kuwa tamu kwa ladha lakini tunda lina Karolies chache sana (105 Calories), wakati huo huo 92% ya tunda hili ni maji. Kitu hiki kina faida mno kiwenye mwili wako hasa baadhi kazi zile ambazo maji hufanya mwiulini hufanywa na tunda hili.Fibers na Maji ya tunda hili hukupa afya bora wakati huo huo likiwa na calories.
Lina vitamin C , Vitamini A, Vitamin B1, Vitamin B5, Vitamin B6 na virutubisho vingine vingi vyenye faida nyingi sana kama vile , kukukinga na kasa, kuboresha afya ya moyo,Ni tunda zuri sana kwa afya ya ngozi na nywere n.k .
Litumie mara kwa mara uone faida hizi kwenye mwili wako.

#8.

PASSION





Matunda sio tu mazuri kwa harufu nzuri sana yaliyonayo.LA hasha !!!! Tunda hili linafaida kubwa sana kiafya .Tunda hili lina viritubisho muhimu sana kwa afya ya mwili wako mfano,

Energy ____________ 97 kcal
kabohydrate ____________ 23.38 grams
protini ____________ 2.2 grams
Vitamin A ____________ 1274 IU
Magnesium ____________ 29 grams
Madini chuma ____________ 1.6 Milligramu
Na virutubisho vingine vingi sana vinavyokulinda na kansa, shinikizo la damu na shmbulio la moyo, magonjwa ya macho, Anemia, Ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa na matatizo mengine mengi ya kiafya. USIPUZIE tunda hili lina faida sna kwa mwili wako.



#9.

MAPEAZI



Matunda matamu sana na yenye faida kubwa sana kwenye mwili wa binadamu.Tunda hili lina vurutubisho muhimu sana kwa afya kama ifuatavyo;

Fiber ________________ 23%
Copper ________________ 17%
Vitamin C ________________ 10%
Vitamin K ________________ 9%
Takwimu hizi kwa mujibu wa Orodha ya mfumo wa ubora wa vyakula yaani Food Rating System Chart huonyesha matunda haya kuwa %DV ikimanisha kuwa peazi ndio tunda lenye uwiano sahihi sana wa virutubisho kuliko matunda mengine.

Matunda haya husaidia sana mwili wa binadamu kuepukana na magonjwa ya moyo na sukari, Hupunguza hatari ya kupata kansa, na faida nyingine nyingi sana kiafya.

JE WAJUA ?!……… Kwa mujibu wa Shirika la Marekani la udhibiti wa magonjwa U.S Center for diseases control Peazi ndio tunda lenye mzio mdogo kuliko mengine (most low allergy fruit). Unasubiri lini wakati ushafahamu faida ya tunda hili ?! fanya kulitumia walau hata mara kadhaa kwa kila mwezi, Naongea hivi kwa sababu matunda haya hupatikana kwa wingi katika sehemu na sehemu lakini hii haimanishi kwamba hayapatikani.



#10.

TANGO



Hili ni tunda (Cucumber) sio mtandao maarufu wa kijamii wa “Tango meesenger”. Tunda hili lina faida nyingi mno kuliko unavyoweza kufikiria ! Hebu tazama baaadhi yake >>>

Hulinda ubongo ,Tango lina kirutubisho kinachoitwa Fisetin ambacho huupa ubongo afya bora sana, kwa kukusaidia kutunza kumbukumbu,na kuzidisha uhai wa seli mbalimbali kwenye ubongo.
Linakulinda na hatari ya kupata kansa, Tunda hili lina Kirutubisho kinachoitwa Lignans ambacho huweza kukusaidia kuepuka kansa ya maziwa, kibofu, via vya uzazi, vilevile Cucurbitacin ni kirutubisho muhimu sana kwa ulinzi dhidi ya kansa.
Hukupa usafi wa kinywa na hewa toka mdomoni na ulinzi wa kinywa na meno, Tunda hili linao uwezo mkubwa sana wa kuua bakteria wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa na magonjwa ya meno.Hivyo hukuepusha na hatari za bakteria hatari kwa kinywa na meno yako.
Huwafaa sana wagonjwa wa kisukari.Tango likiwa ni tunda lenye Kalories chacche sana (calories 16 kwa kikombe cha vipande vidogo vidogo)….Hii ni habari njema sana kwa wagonjwa wa sukari kufaidi faida mbalimbali za kiafya zinazotokana na tunda hili bila hofu yoyote ya kupanda au kushuka kwa sukari.
Hizi ni baadhi ya faida nyingi za tunda hili ambalo sio adimu ukiamua kulitafuta utalipata kwa urahisi na gharama nafuu ya kuridhisha.Rafiki yangu usipuzie ni muhimu sana kuzingatia faida zake kiafya.

KWA FAIDA YAKO :

MATUNDA NI CHAKULA KITAMU, CHA GHARAMA NAFUU, RAHISI SANA KUPATIKANA. MUNGU ALIWAPATIA BINADAMU MATUNDA KAMA DAWA NA CHAKULA CHAO . NANASI MACHUGWA PAPAI PARACHICHI NDIZI TIKITIMAJI na mengine mengi sana husaidia mno kujenga na kulinda afya ya mwili wako , zingatia haya utaishi kwa afya njema.
 
Mimi kila siku lazima nile kachumbali...karoti na hoho na tangawizi ndani...ni sawa?
 
Bado sija amka maana leo ni wikendi,
Nime kula tu tunda kwa mke wangu natural

HAYO ARTIFICIAL TUNDA ngoja ntaendea gengeni....

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Na bet huu Uzi baadae utabadilika uwe wa kugegedana kimapenzi!
 
Back
Top Bottom