Beesmom
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 17,202
- 28,732
Hii ndiyo Siri kubwa iliyopo na inayowatafuna wanandoa.Umeoa au umeolewa Kwa harusi yenye mbwembwe kibao huku mmefichiana makucha...kimbembe mmeanza kuishi uliyedhani ni maria mama mtakatifu kumbe ni mwajuma ndala ndefu🤣uliyedhani ni yohana kumbe ni Petro kumkataa yesu mara tatu kabla ya jogoo kuwika.😳
Binadamu hubadilika bhana,tena hubadilika kuwa adui.Sasa watu badala ya kuachana wanaendelea kuvumilia,eti ndoa ya kanisani watu watasemaje au nikimwacha Mali tutagawana.☹️ Wee bhana we...hata ukimwachia vyote ukajinusuru na kesi za mauaji kama mwanza embu mwachie vyote sepa.Nenda kaanze na mkeka.Kwanza kaburini hatuzikwi navyo viache🙄
Watu kuongea ni kawaida,wanaongea yanapita.inakuwa ni kipindi Cha mpigo tu unasemwa wee,wanatulia.
Kuishi na mtu mzima asiyethamini ndoa inahitaji jitihada ya hali ya juu sana.Wewe unajitoa mhanga kuitunza ndoa Yako mwenzio kichwani anawaza hata akiniacha nitapata mwingine.Yaan maana yake alipo bado hajaridhika bado anasafari ndefu.Unamkumbatia hakumbatiki ....mwache aende,usiogope kitu,aibu fedheha tumeumbiwa na ndo maisha yenyewe.Watoto Mungu hulea tu popote ...mbona wengine tumekua ivoivo tu🙄😏🤜