Umeme na Nishati: Tatizo sugu Tanzania

Tunaweza kwenda mbali zaidi tukaiga ...Singapore, Taiwan, China etc (hawa tulikuwa nao sawa wakati fulani)...au unasemaje 🙂

Kama tulikuwa sawa kwa nini wametuacha tena kwa mbali tu....? Najua utasingizia sera mbovu...
 
Kama tulikuwa sawa kwa nini wametuacha tena kwa mbali tu....? Najua utasingizia sera mbovu...

Ndio swali la kujiuliza sisi kama taifa. Lakini jingine ni kuwa kwa kuona wenzetu tuliokuwa nao level moja wakati fulani wamesonga mbele inaamanisha kuwa inawezekana...........

Challenge inabakia kwetu sisi kama taifa kama tunahitaji kufika huko waliko wenzetu au kuendelea na status quo.
 

Of course it's possible but you need to have what it takes in order to make it happen.....something which is lacking...
 
Of course it's possible but you need to have what it takes in order to make it happen.....something which is lacking...

Kwa sisi watanzania sidhani kama tumewahi kujiuliza 'what it takes to make it happen'......nadhani mwendo wetu ni wa zimamoto (firefighting). Tukiona wakenya wanapata mapato mengi kwenye utalii basi na sisi tunakwenda CNN na UK kutangazwa kuhusu utalii wetu. Hatujaangalia kama hoteli tunazo za kutosha na ku-encourage watu wajenge zaidi, tumetrain watu wengi with good qualification kufanya kazi kwenye tourism industry, miundombinu husika iko vizuri etc ......
 


inanishangaza sana hii nchi ku bajeti $200m kwa ajili ya vitambulisho na $60m kwa ajili ya umeme. Huu ni upumbavu wa hali ya juu au ni hela ya uchaguzi mkuu ujao.
Vitambulisho vimeshidwa kuzuia madrid bombings, na mambo mengine mengi na nchi nyingi zinavipinga, je tz vitatusaidia nini?

Vitambulisho havitasaidia kitu tz kwa ajili ifuatayo:
1. Asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima na wanaishi vijijini, mkulima akitoka nyumbani habebi wallet anabeba jembe kwenda shambani kwa hiyo itakuwa ni kwa matumizi ya watu wa mjini.

2. Tanzania haina polisi wa kutusha kwenda kwenye eneo la tukio haraka je hao polisi wa uhamiaji watawatoa wapi kwa ajili ya vitambulisho na kama nia yao ni kusimamisha ujambazi, watumie hiyo hela kuajiri polisi wnegi na sio vitambulisho.

3. Watanzania wengi ni maskini sana kama mtu anaweza kupata passport ya dili kwa data za mtu mwingine itashindikana id ya mtu mwingine ( mnaokaa ngambo mtanielewa kuhusu kufogi ilivyo rahisi hasa kwa matu maskini). Ulaya watu wanafogi sana id za watu na huku watu hawana njaa kama bongo.

Umeme ni muhimu sana

1. Hiyo hela inatosha kununua jenerata mpya za zaid 20omw (sio dowans na haitachukua mwaka mmoja kufika kama dr tanesco anavyotudanganya). Itakuja kwa kipindi cha miezi sita kama rostam alivyoileta dowans.

2. Kama kukiwa na umeme wa uhakika wawekezaji watakuja wengi , kwa hiyo ajira itapatikana, ujambazi kupungua na serikali kupata hela kupitia kodi. Wawekezaji hawapendi kwenda kwenye nchi ambazo hazina umeme.

Mawazo yote yanakaribisha
 
Naomba niurudishe huu mjadala tena kwa kuipima Tanesco na kinachoendelea kuhusiana na nishati ya umeme.

Mama unazungumzia Stieglers Gorge ambayo iko kwenye bonde a mto rufiji. Bwawa la umeme likijingwa hapa, litakuwa na uwezo mkubwa wa kuitosheleza Tanzania marudufu, takriman MegaWati 2100.

Kwa mujibu wa Tanesco, uwezo wa mabwawa tuliyonayo na mitambo mingine tunayoitumia ya gesi na diseli, ni Megawati 939.


Lakini bado Tanesco na wizara ya Nishati haijaweza kutoa Tathmini nzuri kutuambia kuwa Tanzania tunahitaji umeme wa kiasi gani kwa mwaka.

Kuna mipango kibao ya kujenga na kuzalisha umeme iwe ni mabwawa au makaa ya mawe, ukipiga mahesabu ya haraka, utakuwa kuwa gharama za mipango hii mipya ni sawa na gharama za kuijenga Stieglers ambayo ni dola Billioni 2.


Jumla ya hii miradi hapo juu in Us $1.3 billion, sasa ukiongezea pesa tulizopoteza kwa kuwalipa IPTL, Richmond an Dowans, unakuta kuwa tuna pesa nyingi za kuweza kuwa na mradi kabambe wa kuzalisha umeme wa kututosha bila kutoka jasho.

Hata kama tukiacha tumia hizi pesa za miradi hii hapo juu, angalia pesa tulizofuja BOT, Ndege, Rada na Kiwira, jumla si chini ya US $ 1 billion!

Swali linakuja, je tuna dhamira ya kweli kupata ufumbuzi wa kudumu au tunaendelea kuziba viraka na kujihujumu kwa kutumia miradi midogo midogo isiyo ya maana.

ukiendelea kusoma mipango ya Tanesco, kuna jambo ambalo linajifunua wazi na sina uhakika kama hili limepandwa kwa makusudi au ni ukweli.

Kwa mujibu wa Tanesco kama jedwali la kwanza hapo juu linavyoonyesha, Dowans ndio walikuwa wazalishaji wa umeme wa mitambo iliyoletwa na Richmond. Na hii ni tangu Disemba ya 2006! Lakini ni Rais Kikwete akihojiwa na waandishi wa Nipashe January ya 2007 aliyesema Msabaha angejinyonga kwa kuingia mkataba na Richmond.

ni vipi basi kama nukuu inavyoonyesha hapa chini kuwa Tanesco ilishajua kuwa Richmond imeiuzia Dowans mitambo?

Si dhumuni langu kuendelea na mdahalo kuhusiana na Dowans, lakini ni kujiuliza ni vipi Tanzania na Tanesco zinashindwa kuwa na mipango imara ya kuzalisha umeme kwa kisingizio kuwa hatuna pesa, huku tunazo nyingi na tunazimumunya kwa ujinga?
 
Hivi hiyo mitambo ya Dowans/ RDC waliitoa wapi........kwa anayejua please
 
Hivi hiyo mitambo ya Dowans/ RDC waliitoa wapi........kwa anayejua please

supposedly some where in either North Carolina if not South Carolina. We need name of manufaturer, model and year they were made!
 
Nchi ikiingia kizani sijui itakuwa kwa muda gani makampuni mengi yatasimamisha uzalishaji, kupunguza kwa kiasi kikubwa utendaji wake wa kila siku. Hili litasabiasha baadhi ya makampuni hayo kupunguza wafanyakazi aua kufunga kabisa viwanda vyao na matokea yake kodi zinazokusanywa na serikali toka makampuni na viwanda hivyo na wafanyakazi waliojiriwa huko yatapungua sana na kuathiri bajeti ya serikali na mipango yake mingi (kana wana mipango yoyote inayoeleweka na Watanzania). Tukikosa vitambulisho kwa maoni yangu tutakuwa tumeokoa shilingi bilioni 200 kama nchi tumeweza kuishi miaka 48 sasa bila vitambulisho na hakukuwa na matatizo yoyote yale, lakini tukikosa umeme hata kwa miezi sita tu athari zake ni kubwa mno.
 

Kaka kuhusu Stiglers huu ulukuwa uzembe wa hali ya juu. Kuna kigogo mmoja wa TANESCO enzi zile alikwamisha huu mradi ambao tayari serikali ya Sweden ilikuwa tayari kufinance. Kuna jamaa UDSM aliandika Thesis huu mradi na ameeleza mengi sana.

ALSTOM ndio scandle ya kutisha. Mitambo imefungwa na hadi mkataba unaisha haikutumika hata kutengeneza umeme wa nyumba moja. Hata hivyo tuliwalipa all the charges. Nasikia hata mitambo yenyewe ilishafunguliwa na kuhamishiwa Dar na "wenyemali"... Yaani hapa ndio kuna aibu kubwa lakini kwa kuwa haihusishi sana siasa/maslahi ya makundi CCM huoni moto ukiwaka "BUNGENI"....

Kama nilivyosema hapo kabla tuwe makini sana na hawa MASIHA FEKI ambao wanachofanya ni kuendelea kuendelea kuhalalisha MFUMO FISADI na kuwadanganya watanzania kuwa wanapambana na MAFISADI. Hii ni vita ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya CCM ambayo nia pekee ni kuendelea kulinda uhalali wa tabaka tawala. Hata Mwalimu alikosea aliposema kuwa upinzani mzuri utatokea CCM. Huu utakuwa upinzani mzuri kwa maslahi ya TABAKA HILI LILOSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA WATANZANIA lakini kamwe skwa WATANZANIA haswa wale walalahai(MiddleClass) na walala hoi(DOWNTRODDEN)

omarilyas
 
Nyani,

Wala usione aibu, sema wazi tukusikie, "ndivyo tulivyo", wavivu w kufikiria, wavivu wa kufanya kazi, waoga wa kuingia gharama, tuliokosa ubunifu na zaidi mwamko wa uzalendo=Kutegemea misaada!


Ubunifu utatoka wapi wakati mmefungia nje mainjinia, ninyi mangwini ndio mnatoa maamuzi ya kiinjinia!! Kaaaazi kweli!
 

Ndugu,

nimetoka kuperuzi kwenye kitabu cha Kjell Havnevick cha Tanzania: The Limits to Development from above na kuna reference nzuri sana kuhusianian na Stiegler Tanzania: The Limits to Development ... - Google Book Search

kisha kuna mwanamama Ann Dannaiya Usher ambaye anaandika kuhusu bwawa la Pangani kwenye kitabu chake Dams as Aid Dams as Aid: A Political Anatomy of ... - Google Book Search

Wote hawa wawili ikiongeza na Manongi http://iodeweb1.vliz.be/odin/bitstream/1834/531/1/Wetlands103113.pdf utaona kuna uzembe wa hali ya juu wa sisi wenyewe na hata wafadhili wetu waliotusaidia kwenye hii miradi.

Hapo ndipo utajua kuwa misaada mingine haikuwa na manufaa hata kidogo.

Lakini swali bado linarudi kwetu, ni lini tutakaa chini na kuja na program ya muda mrefu ya Nishati ili tuweze kuwa wazalishaji mali hodari na makini? Using Gordon Brown words of high value product and services, the question becomes when can we the People of tanzania implement high value vision and execute high value plans using high valued leadership and high value labor?

Hili la Umeme linanikera sana, the fact that Tanesco wanakiri kuwa umemem huu unafikia only 11% ya Taifa inaonyesha kuna kasoro za hali ya juu!

source Tanesco.com
 
Si dhumuni langu kuendelea na mdahalo kuhusiana na Dowans, lakini ni kujiuliza ni vipi Tanzania na Tanesco zinashindwa kuwa na mipango imara ya kuzalisha umeme kwa kisingizio kuwa hatuna pesa, huku tunazo nyingi na tunazimumunya kwa ujinga?

Kaka ni muhimu sana kuendeleza mdahalo huu wa sekta ya umeme Tanzania. Bado kuna NetGRoup issue haina majibu, bado kuna ufisadi wa ALSTOM haujapatiwa majibu, bado kuna UFISADI wa enzi wa IPTL hauana majibu...Huu ndio wakati wa kuwaamsha watanzania walionza kusisinzia tena baada ya kuanguka kwa KINARA WA UFISADI na hizi kesi zinazoendelea....

GE walikuwa moja ya sponsors wa LEON SULLIVAN SUMMIT ya Arusha. Kwa kushirikiana na USAID walifanya presentations na lobbying makini kuliko washiriki wote waliokuwepo hapo. Mimi nilishtuka sana kuwaona hapo na haswa baada ya kusikia jinsi wanavyopigia mchepuo suala la REGIONAL ENERGY POOL STRATEGIES kama ilivyo huko west africa. Kwangu mimi hii ilikuwa ni strategy ya kuingia katika mpambano wa uhodhi wa TANZANIA energy potentials kati ya Uncle SAM na makamarade wetu CHINA. Hii ikitilia maanani kuwa serikali ya Marekani ilifikia kutishia kusimamisha utekelezaji wa msaada wa MCC kama serikali/bunge hawajapitisha sheria mpya ya umeme ambayo ingeruhusu sekta binafsi kushindana sawa na TANESCO katika maeneo yote yaani utengenezaji, usambazaji na igawaji kitu ambacho kilikuwa kinapingwa na wengi wa wabunge wetu.

omarilyas
 
Kaka Omar,

nilikuwa na maana ya thread hii isiwe ni kujadili Dowans maana kuna thread karibu 6 zinajadili suala la Dowans na Tanesco.

Hapa mimi nimedhamiria ni kuongelea suala zima la umeme na nishati Tanzania.

Tukirudi kwemye mfano wako wa GE, mwaka juzi nafikiri Tanzania ilitembelewa na Kibosile mmoja mkubwa wa GE. Huyu jamaa Mhabeshi ni EVP ambaye yuko based South Afrika. Nilitegemea basi labda Tanesco, Ewura au wizara wangejigonga gonga wapewe hata subsidised pricing ya Mitambo, lakini nafikiri kama kawaida yetu, focus yetu ilikuwa ni vipi tutapata mlo!

No wonder procurement za Tanzania zinapitia middle men wa ajabu na si directly to the manufatures. i would rather see a State operated company procuring on behalf of Serikali everything and not uzabuni kwa kina Gire au Vithlani.

Hivi wale commercial and trade attachee wetu walioko kwenye balozi zetu nchi za nje kazi zao ni nini?
 
To answer your question Umeme ni muhimu kuliko vitambulisho... PERIOD!!!!!!!!
 
To answer your question [precisely] Umeme ni muhimu kuliko vitambulisho... PERIOD!!!!!!!!
 
Rev Kishoka, naomba nianze kwa kukupongeza kwa kuanzisha thread nzuri (as always) ambayo inataka kupata larger picture na si firefighting na frivolous details kama kawaida yetu.
Naomba nitoe mfano thread "ni kweli mpaka uolewe utoe tigo" ilivyokuwa active kwa wiki nzima na post 400 na kitu! Lakini hapa unakuta watu wanabaki clued to a word or sentence you wrote. Lakini inabidi uwe mvumilivu, hii ndo demokrasia.

Getting to your topic kwa nini tunashindwa kutatua suala la Nishati na kwa nini ni tatizo sugu, mimi nadhani kuna mchangiaji (kumradhi sioni post yake kwa haraka) amezungumzia system mbovu. My friend Nyani amebisha, lakini ukweli ni kwamba it is a matter of system. If you enter a system, you try to adapt and swim with the current. unfortunately system nzima ni mbovu. Kibaya zaidi system hii haiko straightforward , ina mabonde na milima na kuna kona kibao za kukata. Lakini the larger picture is that Tanzanian public system was built on the wrong fundamentals. it was build around a strong presidency, who nominates (not elect and not approved by parliament) his ministers, the principle secretaries, District commissioners, regional commissioners etc. Sasa kama watendaji hawa ni political appointmees, huwezi kutegemea kuwa wataleta decision yoyote ya kutetea wananchi, siku zote watatetea mtu aliyewaweka madarakani and that is the president. This was the system that Mwalimu left for us (true he did inherit partly from colonizers but it was convenient for him to keep it and thus exert control over all areas of authority) na tunaendelea nayo bila kuhoji.
Hivyo system is weak, there is no accountability na everybody is busy kissing a$$ of the powerful.
Tatizo lingine ni lack of innovative lateral thinking - hii ni kutokana na kuwa family and education system yetu ina discourage any thinking and initiative, let alone lateral thinking. We are just handed down information and we have to take it and spew it back the way that we are told.
Sasa unafikiri kuna watu kule Tanesco ambao wako katika leadership level who a) understand the problem including the source b) have worked out the solution long and short term c) are brave enough to stand up and give proper advice d) [upper management] have guts to implement it
Hapa kila mtu anajua Dr Idris is the boss he has the ear of the president (her was appointed by JK, he did not earn it in an open process, he was not vetted by the parliament)
kila mtu anaelewa that this man has a vested interest in buying Dowans nobody dares question or cross him. So they are told "find alternatives that don't work, because we have to buy Dowans equipment" so they obediently do it. They are told to 'upgrade their system' and cease LUKU services, they do it. That is why my dear friend Nyani gets exasperated and says Miafrika ndivyo tulivyo. Because we lack initiative. And even though we philosophize the reason, the truth is we do have a problem!

Nadhani nimeshaandika sana, na nitaendeleza mjadala huu baadaye kidogo na kutoa maoni yangu as to what shoud be done. Not from a technical point of view as I will not pretend to understand anything about energy policies and engineering, but in a more broader sense, to improve they way we handle such problems (it is not a crisis any more because it is persistant!) like the energy shortage.
 
Mkuu, mi naungana mkono kabisa wabnafsishe tu hii sekta, sis tumeshinwda kujiendesha. umewahi kusikia eti TBL inasema hawana chupa za kutosha hivyo kuna uhaba wa bia nchini? Au kwamba wanafanya system upgrade hivyo hawatauza soda kwa siku 10? Cha muhimu mchakato huu wa ubinafsishaji ufanyike kwa uwazi na kusimamiwa na wataalam. Lakini pia ifanyike kama kwa TBL kwamba asilimia kubwa tuuziwe wananchi maana sisi ndo wadau wenyewe, then tutaenda katika hizo general meetings na kuwawashia moto menejmenti!
Lakini shirika la Umma... no thank yee! No more! Ni ukiritimba, inefficiency na ufisadi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…