Hebu tuchukue hatua moja na kuliangalia hili jambo la nishati kwa mtazamo mwingine wa ki-ngwini!
Nitaanzia na Zanzibar. Zanzibar, mpaka leo wanafanya wateja na watumwa wa Tanesco kwenye suala hili la umeme.
Je mahitaji ya Umeme Zanzibar kwa ajili ya nyumba, maofisi na viwanda ni kiasi gani? Tukishajua mahitaji hayo, kuna uwezekano wa Zanzibar kujitutumua na kuwa na mitambo yao ambayo ni huru kutoka Tanesco kujizalishia umeme na hivyo kuondokana na Ukiritimba wa Tanesco?
Kama Zanzibar matumizi yao ni 250 MW, wakinunua mtambo wa MW 500, umeme wa ziada kuunganishwa kwenye gridi ya Taifa na zaidi unaweza kusaidia kupanuka kwa matumizi ya Umeme Zanzibar na hivyo kuhakikisha kila nyumba ina umeme madhubuti na viwanda kuweza kuongezeka hivyo kukuza uchumi na kuawa huru ki-nishati?
Je suala la Zanzibar kuwa na mfumo huru wa Umeme ni lazima lipate baraka ya Serikali ya Muungano au SMZ ina uwezo tosha kupitia fungu lake lenyewe kujizalishia umeme huru ya kufuatilia makubaliano yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na mfumo wa Umeme Tanzania?
Kama Zanzibar wataweza kujitoa kwenye utegemezi huu wa Tanesco kujipatia na kujizalishia umeme na wao wakawajibika kwa EWURA na hata mfumo wao kuweza kuzalisha na kuchangia kwenye Gridi ya Taifa, hatuoni kuwa kutakuwa na manufaa katika maendeleo yetu kama Taifa na kuondokana na mikorogano tuliyonayo na lawama kuwanyanyasa Zanzibar?
Nikirudi Bara, tuna wilaya takriban 130. Je ukiondoa miji mikubwa kama Dar, Moro, Arusha na mingineyo ambayo kuna viwanda, je mahitaji yetu na nyumba zinazotumia umeme ni kiasi gani?
Ni nyumba ngapi katika wilaya ya Hai ambazo zinatumia umeme wa Tanesco na si vibatari? Je wilaya ya Kondoa, Bahi, Manyoni, Nzega na Kigoma Vijijini?
Je umeme uliopo ambao ni wa Diseli ambao tunajua kwa takwimu za Tanesco ni 34 MW
ISOLATED DIESEL POWER STATIONS
Total installed Capacity 33.8 MW
Available generation varies from month to month, but in 2006 it averaged 17.5 MW.
TANESCOs isolated diesel power stations which are not connected to the national grid system are located at Mtwara, Lindi, Songea, Masasi, Tunduru and Kilwa Masoko. Other townships are Mpanda, Kigoma, Mafia, Ikwiriri, Ngara, Biharamulo, Liwale and Njombe.
Most of the diesel power stations are aged and urgently require running spare parts to improve their operational performance. Some of the power stations need upgrading and major rehabilitation to meet the growing consumer demand in the townships.
tunaweza kuongeza kwa kubadilisha na kutumia mitambo ya umeme wa upepo na jua?
Tunaweza kuwekeza Umeme nchi nzima n akuondokana na Tanesco kama tukiruhusu kwa nia ya kweli kuwepo kwa ushindani wa ufuaji umeme na usambazaji.
Mathlani na hili ni poendekezo langu ni kwa kila wilaya kuwa na uwezo binafsi wa kuzalisha si chini ya megawati 20 za umeme kutumia umeme wa Upepo.
Mapendekezo yangu ni kwa Wilaya hizi kuchukua hatua kupitia vyama vya ushirika, bodi za biashara na wananchi wenyewe kuwa wamiliki na wazalishaji wa umeme huu. Mtaji wao unawezekana kupatikana kwa kutoa Bond au Treasury Bill ya miaka 10 pale BOT, na wakanunua mitambo ya umeme wa upepo na Jua au hata kama ni wa gesi ya makaa ya mawe (kiwira will be the supplier) au Jatropha (nitaliongelea hapo chini).
Ikiwa kila wilaya inaweza kuzalisha umeme mwingi na waziada, kama nilivyozungumzia suala la Zanzibar hapo juu, basi kila nyumba, shule, ofisi, hospitali, zahanati zitakuwa na umeme na uwezekano wa kuwa na viwanda kuongezeka na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta ya Diseli katika kuzalisha.
Kitendo hiki cha kusambaza umeem na kuhakikisha umiliki ni wa wananchi wenyewe kwa kuuziwa na kununua hisa katika mradi, kitakuwa ni kitendo cha kishujaa na cha msingi katika kuleta utatuzi wa muda mrefu kwa tatizo sugu la umeme. Umeme wa ziada ambao hautatumika, basi utaunganishwa kwenye gridi la Taifa na kuuzwa kwa wale wenye kuhitaji umeme mwingi zaidi.
Nimeongelea Jatropha hapo juu na hasa ukizingatia kuwa sasa hivi, kuna wawekezaji wengi wa nje ambao wanakuja Tanzania kununua na kukodisha ardhi ili wazalishe mmea wa Jatropha ambao ni chanzo cha mafuta yanayoweza kutumika badala ya mafuta ya uarabuni.
Kwa sasa hivi na bei za mafuta kushuka duniani, Jatropha inaonekana kama ni biashara ambayo haitalipa.
Lakini sisi tuna nafasi basi kulima Jatropha kwa wingi, na kuizalisha kuwa mafuta ya viwanda na kutumika kuzalisha umeme na kuachana na matumizi ya Dizeli.
Pendekezo langu ni kuhakikisha kuwa tuna ukulima stadi wa Jatropha ambao hautatuletea tatizo la njaa kutokana na wakulima kuacha kulima mazao ya chakula au mazao mengine ya biashara ;pamba, tumbaku n.k.
Tutumie nyenzo za ndani iwe ni SUA, TBS au TPDC na UDSM kuweza kuwa na uzalishaji wa kusindika Jatropha na kuzigeuza kuwa mafuta ya kuendesha mitambo.
Hili si kwamba litatupunguzia gharama za kuagiza mafuta pekee, bali litatoa ajira kwa wajasirimali na wawekezaji wa ndani, ukianzia na wakulima mpaka viwanda vy akuzalisha mafuta. OKwa uziada tuu, machicha ya Jatropha yanaweza kuwa ni mbolea au chakula cha wanyama kama Ng'ombe, Kuku, Kondoo, Mbuzi hata Nguruwe na Farasi.
Hivyop basi tukiweza kuwa na Tanzania yenye umeme thabiti na wenye kusambaa kila kona, basi hatua zetu za maendeleo zitasonga mbele na hizi mbio za kuhujum nchi ambazo zilianza nyakati zile za majenereta ya petroli kwa kila nyumba na sasa hivi mkorogano wa IPTL, Kiwira, Richmond an mengineyo ambayo hatuyafahamu, yatapungua.