Sasa nchi itaendeshwaje bila Kodi? Tukupe basi nchi uongoze bila kukata Kodi....tupunguzeni malalamiko, mwishowe turudi tulikotoka kwenye vitisho na hofu.
Siwezi kukataa, Ila hakuna Mambo yenye manufaa yanayofanywa Kwa hizo Kodi?Kodi zinazoishiwa kuibiwa au maccm kutanua kwa raha zao? 😳😳😳
Siwezi kukataa, Ila hakuna Mambo yenye manufaa yanayofanywa Kwa hizo Kodi?
Vipi kesi ya mbowe, ni zaidi ya utekajiIla hajawahi teka mtu.Ana nafuu kidogo.
Anaandika malisa GJ
Fikiria unanunua umeme wa 45K, serikali inalamba 11K kupitia makato mbalimbali, na wewe unaambulia umeme wa 34K tu. Fikiria wewe ni mtumishi, umekatwa PAYE, umekatwa HESLB, umekatwa NSSF. Zote hizo unaichangia serikali. Halafu kile kidogo unachobakiza ukienda kujaza mafuta serikali inakula karibu TZS 700 kwa lita. Ukinunua umeme ndo kama hivi.
Ukinunua sukari, chumvi, mafuta, kote huko wanakulamba kodi zenye kuumiza. Bado hujamtumia pesa mama yako mgonjwa kijijjni ukutane na bwana tozo.
Sasa badala ya kuwaza namna ya kutatua changamoto kama hizi zinazomuumiza mwananchi, tunawaza uchaguzi wa 2025 na maumbile ya wagombea. What the hell with maumbile? Awe mwanamke au mwanaume it doesnt matter, muhimu tunataka kiongozi anayeweza kushughulikia matatizo yetu.
Kama mtu hawezi kushughulika na matatizo ya watu wake, uanaume au uanamke wake unatusaidia nini?
View attachment 1940340
Kwa upande wangu sioni tulipopishana sana na nchi nyingine za kiafrika baada ya Uhuru Hadi Leo. Na nadhani tulibugi tulipochagua siasa za kijamaa plus neo colonialism iliyopo duniani...naona hatuko mbali na tulipotakiwa kuwa.Wewe kama Mtanzania niambie baada ya miaka 60 ya maccm madarakani kwanini Wafanyakazi, Wakulima, Wahitimu wa elimu ya juu wote wanalalamika? Watanzania tuna chochote cha kujivunia baada ya kuwa huru kwa miaka 60!? Ni kipi hicho?
Kwa upande wangu sioni tulipopishana sana na nchi nyingine za kiafrika baada ya Uhuru Hadi Leo. Na nadhani tulibugi tulipochagua siasa za kijamaa plus neo colonialism iliyopo duniani...naona hatuko mbali na tulipotakiwa kuwa.
Nakiri tuna tatizo katika uongozi, tuna viongozi walotanguliza maslahi Yao mbele kuliko nchi...Ila Kwa upande wa Samia, Mimi nimechagua kumpa muda, nitamuhukumu Kwa kigezo cha muda kuwa amefanya nini....sio kwa jinsia yake, Uzanzibari wake wala UCCM wake.
Lakini tunaweza kulinganisha ukubwa wa nchi ya Rwanda na hii ya kwetu? Sisi tunafyatuana, population ya kutosha, Tena Population iliyodekezwa na ujamaa isiyotaka kulipa Kodi na inayoona inaonewa kufata Sheria...Tumepishana tuchukulie Rwanda pamoja na kuwa simpendi Kagame kwa kuwa ni dikteta ná muuaji wa wapinzani wake lakini katika kipindi kifupi amenyanyua sana vipato vya Wafanyakazi na Wakulima na hata kuwavutia waliohamia ughaibuni kurudi kwao kwa maelfu ili kuchangamkia ajira zinazolipa vizuri. Nchi yao ni safi sana utadhani uko majuu kwenye nchi zilizo safi. Na mafanikio hayo ni ya miaka 24 au tu baada ya kuuana 1994z. Samia KISHASHINDWA ndani ya miezi minne tu. Hana jipya hasa ukitilia maanani alikuwemo kwenye Serikali tangu 2015. Amebaki kufanya viroja tu lakini uongozi umeshamshinda.
Tumepishana tuchukulie Rwanda pamoja na kuwa simpendi Kagame kwa kuwa ni dikteta ná muuaji wa wapinzani wake lakini katika kipindi kifupi amenyanyua sana vipato vya Wafanyakazi na Wakulima na hata kuwavutia waliohamia ughaibuni kurudi kwao kwa maelfu ili kuchangamkia ajira zinazolipa vizuri. Nchi yao ni safi sana utadhani uko majuu kwenye nchi zilizo safi. Na mafanikio hayo ni ya miaka 24 au tu baada ya kuuana 1994z. Samia KISHASHINDWA ndani ya miezi minne tu. Hana jipya hasa ukitilia maanani alikuwemo kwenye Serikali tangu 2015. Amebaki kufanya viroja tu lakini uongozi umeshamshinda.