Umeme wafika Kisiwani Chole kwa mara ya kwanza toka uhuru

Umeme wafika Kisiwani Chole kwa mara ya kwanza toka uhuru

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
1,984
Reaction score
3,695

uhuru​

dar24.comJul 21, 2024 5:14 AM
f51a195849e5dd60d2cec8ab637ae27c

Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, Mkoa wa Pwani limefanikiwa kufikisha Umeme katika kisiwa cha Chole kilichopo Wilayani Mafia, ambacho hakijawai kuwekwa Umeme tangu uhuru kwa kuupitisha chini ya Bahari.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati Meneja wa TANESCO mkoa wa Pwani, Eng. Cosmas Mkaka akikagua mradi huo, Mbunge wa Jimbo la Mafia ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amshukururu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha za kukamilisha mradi huo.
4f649b9e4846e74d0d2c8b7286348c03

Amesema huduma hiyo ya umeme katika kisiwa hicho utarahisisha shughuli za Maendeleo kwa Wananchi wa Wilaya ya Mafia.
Naye Meneja wa TANESCO Mkoa wa Pwani, Mkaka amesema mkakati wa TANESCO ni kufikisha Umeme katika visiwa vingine viwili vya Jibondo na Juwani ili kukamilisha uwekaji wa Umeme katika vijiji vyote 23 wilayani Mafia kabla ya kufikia mwaka 2025.
a2a9c852cd7eb7495e8b92dde9e80dc4


Alisema urefu wa nyaya za Umeme za mradi huo ni mita 1170 utanufaisha kaya zaidi ya 1000 na mradi huo wa Umeme katika visiwa hivyo vidogo vya kisiwa cha Mafia mkoani Pwani kwa gharama ya bilioni 3.2.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Juma Salum amesema kufika Umeme katika visiwa hivyo ni faraja kubwa kwa Wananchi.

©Dar24
 
Umeme umefika vijana washinde wanacheza ps 🤣🤣🤣

Kusema kweli umeme m naonaga ni kama basic right, mtu kutokuwa na umeme kunadumiza akili sana, mtu hachek hata tv, haangalii habari, hawez tumia simj mtandaon kupata habari na maarifa mengine,

Tanesco ongezeni juhudi
 
Back
Top Bottom