Umemfumania na vidonge vya majira.

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu tuchukulie kwamba, wewe ni mzazi, iwe ni wa kike au wa kiume. Halafu una binti mkubwa ambaye amefikia umri wa kuweza kushiriki tendo la ndoa. Siku isiyo na jina, unamfuma akiwa na vidonge vya majira. Hebu niambie, ungefanya nini?
 
Unamueleza ajilinde, maana ukimwi ni hatari zaidi ya mimba.
 
Unamkalisha chini kwa utaratibu tu, halafu unamuuliza kwa nini anavyo na kwa nini anavihitaji. Unamweleza athari za kungonoka akiwa angali mdogo hivyo. Unampa moyo kuwa mustakabhai wake una nuru na asifanye mambo ambayo yanaweza kumzimia hiyo nuru.
 
Kwanza anaelewa madhara ya mimba hilo nampongeza,pili awe makini na ukimwi na awe mwaminifu.
 
binti mkubwa wa umri gani??????/

20???
30???????
 
Mwambie pia hivo vidonge kuanza kuvinywa mapema hivo, vinawez a mletea uvimbe kwenye kizazi,na kupunguza chance yaa kupata mtoto, pia mkumbushe kuanza kufanya mapenzi mapema kunaweza sababisha cancer ya mlango wa uzazi, ila la muhimu ajikinge sababu kuna ukimwi utaweza mmaliiza, anatumia vidonge coz hajikingi
 
Watoto wa siku hizi. Mimi na umri huu hata sijuhi hivyo vidonge vinafananaje. Kazi tunayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…