Hebu tuchukulie kwamba, wewe ni mzazi, iwe ni wa kike au wa kiume. Halafu una binti mkubwa ambaye amefikia umri wa kuweza kushiriki tendo la ndoa. Siku isiyo na jina, unamfuma akiwa na vidonge vya majira. Hebu niambie, ungefanya nini?
Unamkalisha chini kwa utaratibu tu, halafu unamuuliza kwa nini anavyo na kwa nini anavihitaji. Unamweleza athari za kungonoka akiwa angali mdogo hivyo. Unampa moyo kuwa mustakabhai wake una nuru na asifanye mambo ambayo yanaweza kumzimia hiyo nuru.
Mwambie pia hivo vidonge kuanza kuvinywa mapema hivo, vinawez a mletea uvimbe kwenye kizazi,na kupunguza chance yaa kupata mtoto, pia mkumbushe kuanza kufanya mapenzi mapema kunaweza sababisha cancer ya mlango wa uzazi, ila la muhimu ajikinge sababu kuna ukimwi utaweza mmaliiza, anatumia vidonge coz hajikingi
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.