Umenena Ukweli Ben pol

Umenena Ukweli Ben pol

heaven on desert

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
1,025
Reaction score
393
Msanii wa R&B Ben Pol amewasifia wasanii wenzake wa Bongoflava kuwa wana uwezo mkubwa kuliko hata wasanii wa nchi zilizoendelea kama Marekani kwa uwezo wao wa kufanya kazi nyingi zikiwemo utunzi na kuimba wao wenyewe.

Kupitia Twitter Ben Pol ambaye mwaka jana na mwaka huu amehit na ngoma kama Pete na Yatakwisha amesema, "wasanii wa Bongo tuna vipaji vya hali ya juu, mtu unafanya kila kitu mwenyewe na bado unaweza kutunga na kutoa Hits, hii hata R.kelly hawezi."

Ameongeza kuwa kutokana na mazingira ya muziki wa kibongo msanii hujisimamia mwenyewe anapotaka kurekodi, kushoot video
ama kujiandaa na show ilhali wasanii wakubwa mfano wa Marekani huwa na watu wanaosimamia mambo hayo.

Amesisitiza kuwa msanii hulazimika kufanya kila kitu kwasababu hawezi kumudu kuajiri watu wa kusimamia mambo hayo. "Sasa watu hawataki kulipa vizuri, mwishowe tunashindwa kutoa ajira kwa wenzetu wenye utaalam fulani fulani wa marketing n.k."

Wasanii wengi wakubwa katika nchi zilizoendelea huandikiwa nyimbo zao (mashairi na melody) na watu maalum (songwriters) ambao
hutafutwa na record label husika kwa kazi hiyo na wao huingia tu studio kurekodi tofauti na wasanii wengi wa Tanzania (na kwingineko Afrika) ambao hutunga na kuimba wenyewe.
 
Msanii wa R&B Ben Pol amewasifia
wasanii wenzake wa Bongoflava
kuwa wana uwezo mkubwa kuliko
hata wasanii wa nchi zilizoendelea
kama Marekani kwa uwezo wao wa
kufanya kazi nyingi zikiwemo utunzi
na kuimba wao wenyewe.
Kupitia Twitter Ben Pol ambaye
mwaka jana na mwaka huu amehit
na ngoma kama Pete na Yatakwisha
amesema, “wasanii wa Bongo tuna
vipaji vya hali ya juu, mtu unafanya
kila kitu mwenyewe na bado
unaweza kutunga na kutoa Hits, hii
hata R.kelly hawezi.”
Ameongeza kuwa kutokana na
mazingira ya muziki wa kibongo
msanii hujisimamia mwenyewe
anapotaka kurekodi, kushoot video
ama kujiandaa na show ilhali
wasanii wakubwa mfano wa
Marekani huwa na watu
wanaosimamia mambo hayo.
Amesisitiza kuwa msanii hulazimika
kufanya kila kitu kwasababu hawezi
kumudu kuajiri watu wa kusimamia
mambo hayo. “Sasa watu hawataki
kulipa vizuri, mwishowe
tunashindwa kutoa ajira kwa
wenzetu wenye utaalam fulani
fulani wa marketing n.k.”
Wasanii wengi wakubwa katika nchi
zilizoendelea huandikiwa nyimbo
zao (mashairi na melody) na watu
maalum (songwriters) ambao
hutafutwa na record label husika
kwa kazi hiyo na wao huingia tu
studio kurekodi tofauti na wasanii
wengi wa Tanzania (na kwingineko
Afrika) ambao hutunga na kuimba
wenyewe.

Vipi hakumtaja Diamond?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kwakweli Ben pool kaona aseme uongo! Yani kuna msanii bongo wa kumlinganisha na R.kelly hata uimbaji? Huu ni zaidi ya uchizi!
 
Back
Top Bottom