Umenipata Msiba!!

Umenipata Msiba!!

mmmh!mkuu bdo,kuna uhusiano kati ya kufiwa na ukubwa!!!mbona mimi bado mdogo sana na nimefiwa pia!!

kuvumilia (kuichukulia hali nzito kama ya kufiwa na kuizoea)ni ukubwa, hata kama u mtoto na baadaye ukakubaliana na matokeo hayo ni ukubwa (ukomavu), wengine wanashindwa kuvumilia wanaenda kupiga ramli (utoto)! pole sana Kigarama
 
Last edited by a moderator:
nilitaka kujua tu!!natamani ungekuwa unanipenda na mimi hivyo!!!
oh! tafuta sababu ya kupendwa........... umeona mama kafanya nini mpaka nikasema nampenda? anajali sana, na hii nimeiona muda mrefu. kiukweli kabisa nampenda mno
 
oh! tafuta sababu ya kupendwa........... umeona mama kafanya nini mpaka nikasema nampenda? anajali sana, na hii nimeiona muda mrefu. kiukweli kabisa nampenda mno
mmmmh!!ok,uwe unafuatilia post zangu kuanzia leo,nitakuwa naamkia kabla ya post!!shikamoo!!vipi hiyo haiwezi kuwa sababu tosha ya kunipenda!!!ha ha ha ha!
 
mmmmh!!ok,uwe unafuatilia post zangu kuanzia leo,nitakuwa naamkia kabla ya post!!shikamoo!!vipi hiyo haiwezi kuwa sababu tosha ya kunipenda!!!ha ha ha ha!
kama utakuwa unaniamkia mimi, naanza kukupenda rasmi
 
Nimezamishwa kinani, kwenye lindi la huzuni,
pakushika sipaoni, mwenzenu ni simanzini,
Nina uchungu moyoni,limenikuta jamani,
Umenipata msiba.

Mwana kukuza nyumbani, na vyuoni masomoni,
Nikamfunza kanuni, za kuishi maishani,
Za kuheshimu jirani, na wakubwa majiani,
Ametoweka.

Kama mvuke wa chai, mwanangu amenihini,
umemtoka uhai, sijui nifanye nini,
Leo mfu siyo hai, amelala kitandani,
Kifo kimemzingira.

Nyumba yote ni vilio, waja hawasikizani,
Alikuwa kimbilio, la kwangu na majirani,
Kweli mola atakalo, hutokea dunia,
Mwanangu nakulilia.

Najipangusa machozi, ni mkiwa wa wakiwa,
Lilikuwa pandikizi, mwenye tabia muruwa,
Leo hii hajiwezi, hakuna analotambuwa
Umenipata msiba!!

kamtwaa manani, ale mleta duniani
Bado hujabaini, kuwa sote tunjiani?
Itowe shaka moyoni, kaburi si duniani
Sijitie msibani, wawachie makuhani.
 
Pole Kigarama! Afu nowdayz naona umejikita sana kule pande za Siasa eti eeh ?
 
Lord have mercy!
Mungu wa rehema na upendo, awafariji kwa namna aijuayo mwenyewe. Hata ndimi elfu hazitoshi kuwapooza kwa hili. Pole sana baba.
 
NAKUTAKIA SUBIRA.

Pole kwa huo msiba, ndugu yetu kigarama
Kufiwa si jambo haba, uhai ukisha hama
Twaomba kwa mola toba, akupe nyingi hekima
NAKUTAKIA SUBIRA, KIPINDI HIKI KIGUMU

Mola akupe subira, kwa msiba kukufika
Akukinge na hasira, najua wataabika
Ujae wewe busara, kwa mola ameshafika
NAKUTAKIA SUBIRA, KIPINDI HIKI KIGUMU

Kwa mola namuombea, mwanao katangulia
Na sisi twakingojea, kifo kitatufikia
Hakuna wa kukikwepa, za kwako zikiwadia
NAKUTAKIA SUBIRA , KIPINDI HIKI KIGUMU

Kifo hakizoeleki, najua wako uchungu
Na wala usihamaki, yote ni kazi ya mungu
Mola ni mwingi wa haki, ardhi na kwenye mbingu
NAKUTAKIA SUBIRA, KIPINDI HIKI KIGUMU

Makazi mema peponi, mwanao twamuombea
Adhabu za kaburini, zisije msogelea
Na wala usiwe duni, kwa mola amerejea
NAKUTAKIA SUBIRA, KIPINDI HIKI KIGUMU

Beti sita nasimama, huu msiba mzito
Umepoteza amana, mtoto sawa na "kito"
Twaomba kwa maulana, amuepushe na moto
NAKUTAKIA SUBIRA, KIPINDI HIKI KIGUMU



SINDANO MWANA WA GANZI (SMG)
KIJIJINI TONGOLEANI
TANGA
 
Back
Top Bottom