Umepataje namba yangu!!!?

Umepataje namba yangu!!!?

Namwambia nitakujulisha namba nimeitoa wap, kisha naendelea na mazungumzo
 
Moja kwa moja kwenye mada...hilo swali ni gumu sana kwa vijana domo zege(mostly) na wapenda kutelezea ganda na ndizi.

Unakutana na binti mkali haswaaa ila kumuomba contacts inakua mtihani. Unapitia kwa rafiki zake, wanakupa namba zake ila unapewa SHARTI moja tu kwamba usimtaje...

Haya sasa unamfata inbox...baada ya salam na kujitambulisha sanaa...anakuuliza swali "nani kakupa namba yangu?"
Unaanza kujiuma uma weeee.
Jamani wazoefu wa haya mambo watupe majibu mazuri ya hili swali tata bila kumtaja aliekupa namba.

Baadhi ya majibu:
1. Niliiona kwenye profile yako facebook(tuna assume yupo fb)
2. Ilikua kwenye group la whatsap...lazima tu awe kwenye magroup aiseee
3. Mtu umpendae huwezi kukosa mawasiliano yake[emoji16] n.k
Jamani wazoefu wa haya mambo ongezeni sababu tuwaokoe madomo zege humu

Njia bora ni kusingizia kakupa namba yeye mwenyewe, hapa lakini lazima uwe umesha bonganae kiasi.
FB, WhatsApp huko kote anaweza akawa hayupo au anatumia namba zingine.
 
Heheeee wazee wa ganda la ndizi.

Kumbe we ulitaka aseme; Eeee wajua, eee wajua, niliiii niliii pata insta, kumbe huko hayupo. Nani bwege hapo?? Nadhani jibu la kwanza ndo sahihi. Akiondoka yu aenda akiwaza jibu lako, nawe unampigia tena kwamba, unaomba lunch na yeye Sehemu
 
Back
Top Bottom