Umesajili Pikipiki yako? Mwisho wa kusajili ni 31st March

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Wapendwa wana Jf
Naona watu wengi wamekuwa wanaongelea magari na kusahau kundi kubwa la wajasiriamali waliopo kwenye pikipiki;
Napenda kukumbusha kwa wale wamiliki HALALI wa pikipiki kuwa mwisho wa kusajili ni tar 31 March 2015.
Epuka usumbufu kasajili sasa.

  • Unatakiwa kuwa na kadi halisi ya Pikipiki na kitambulisho rasmi cha kwako.

Binafsi naona hili wazo la kusajili pikpiki ni Jema kwani pamoja na kurasimisha Pikipiki kutofautisha zile za Biashara na zile za Binafsi (Private)
WATAWEZA KUBANI ZILE ZA WIZI KWANI ZITABAKI BILA KUSAJILIWA KWA KUKOSA KADI RASMI (ORGINAL)
Naamini hili likifanyika kwa usahihi bila rushwa ya kusaidiwa kusajili kutabakia mamia kama sio maelfu ya Pikipiki zilizo ibiwa kwan watashindwa kuzisajili.

Tutamani kungekuwa na ubao/mbao za kuandika namba za pikipiki zilizo ibiwa na kukamatwa kwenye vituo vya Polisi ili wenye pikipiki waweze kuzitambua.
Walio ibiwa Pikipiki wengi hubaki wameduwaa mitaaani bila kujua kuwa kuna Pikipiki zimepatikana/pia hujiuliza, kama zikipatikana hazitangazwi kabisa au zinatangazwa kidogo sana kama danganya toto...huwa zinakwenda wapi???
 
Hao TRA wa ache kutisha watu hakuna mwisho wa kusajili pikipiki una poems eti mwisho wa kusajili ni tar fulani..wakati kila siku watu wananunua pikipiki mpya na kuzi sajili
 
Wapendwa wana Jf
Naona watu wengi wamekuwa wanaongelea magari na kusahau kundi kubwa la wajasiriamali waliopo kwenye pikipiki;
Napenda kukumbusha kwa wale wamiliki HALALI wa pikipiki kuwa mwisho wa kusajili ni tar 31 March 2015.
Epuka usumbufu kasajili sasa.

  • Unatakiwa kuwa na kadi halisi ya Pikipiki na kitambulisho rasmi cha kwako.

Binafsi naona hili wazo la kusajili pikpiki ni Jema kwani pamoja na kurasimisha Pikipiki kutofautisha zile za Biashara na zile za Binafsi (Private)
WATAWEZA KUBANI ZILE ZA WIZI KWANI ZITABAKI BILA KUSAJILIWA KWA KUKOSA KADI RASMI (ORGINAL)
Naamini hili likifanyika kwa usahihi bila rushwa ya kusaidiwa kusajili kutabakia mamia kama sio maelfu ya Pikipiki zilizo ibiwa kwan watashindwa kuzisajili.

Tutamani kungekuwa na ubao/mbao za kuandika namba za pikipiki zilizo ibiwa na kukamatwa kwenye vituo vya Polisi ili wenye pikipiki waweze kuzitambua.
Walio ibiwa Pikipiki wengi hubaki wameduwaa mitaaani bila kujua kuwa kuna Pikipiki zimepatikana/pia hujiuliza, kama zikipatikana hazitangazwi kabisa au zinatangazwa kidogo sana kama danganya toto...huwa zinakwenda wapi???

Ya kwangu ilikuwa imeibiwa kwa mtu, vijana wa kazi wakaniletea nikanunua, nikaingia mtaani nikachongesha kibao cha namba feki, ikawa inapiga biashara ya bodaboda jijini Dar, wakati ilikuwa imeibiwa huko Tarime ~ Mara...! Je naweza saidiwa ktk hili?
 
Mkuu mrangi ni kweli kuwa pikipiki zinanunuliwa kila siku, na tar 31 march ndo mwisho wa usajili na pikipiki zote mpya zitakuwa na namba mpya zilizosajiliwa tayari na zile ambazo hazina uhalali ndo hizo zitashindwa kusajiliwa.
 
Last edited by a moderator:
Utasaidiwaje sasa?Wakati kadi unayo cha muhimu ni kadi original.
 
Wameongeza miezi mitatu tena, mwisho wa kusajili hizo motor cycle ni june, 2015.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Hivi gharama halali ya kusajili ni sh.ngapi! ? Kutokana naona kila mtu analipia anavyojua
 
Wameongeza miezi mitatu tena, mwisho wa kusajili hizo motor cycle ni june, 2015.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums

wajinga sana hawa tra wao wanajua kila mtu anaishi mjini ndio maana huduma za kusajiri zinatolewa makao makuu ya mikoa na sio wilayani sijui ni kwa nini? yani mtu asafiri kutoka mafia mpaka dar kwenda kusajiri pikipiki kwa nini wasinge peleka hiyo huduma huko huko mafia? TRA mna zingua kwa dizaini hiyo pikipiki nyingi hazito sajiriwa na zitapiga kazi kama kawaida!
 
Ndio wameongeza muda hadi june badala ya march mwaka huu! Hapo bado ni kwamba muda hautoshi? Miezi mitatu tena sio mbaya.

Kuhusu bei ya kusahilia inategemea na kadi ulizonazo, kama una kadi original na number plate ni yellow unalipa 40k

Kama ni kadi original na number plate ni white unalipa 47k ya usajili plus 200k kila mwaka.

Back
Top Bottom