Umeshawahi kujiuliza wewe ni nani?

Umeshawahi kujiuliza wewe ni nani?

Mkiitwa nifah mnakuja zaidi ya mmoja iweje sasa wewe uwe nifah.

Mimi niko tofauti, unique...naamini hakuna wa kufanana nami.
Hata wewe pia, labda kama ukiwa hujielewi.
 
Swali hili ni la miaka mingi, na watu wengi, ila jibu bado, na yawezekana lisipatikane. Angalia jamaa wa enzi hizo walivyolikabili swali hili BBC Radio 4 - A History of Ideas

Asante kwa Link nzuri.

Pia nadhani ni swali la muhimu sana. Naamini ni swali la zamani sana. Mwanadamu unapojikuta katika experience ya kujitambua sana unaanza wewe ni nani, Ni swali ambalo ni fumbo na kila mmoja anatakiwa kujitambua.

Tukitazama kuzaliwa na kufa kama sehemu ya maisha tunajifunza kuwa kuna vitu au hali za milele na kuna hali za muda mfupi, kuna ambavyo tunaviacha na hakuna kitu cha kifizikia tunachoondoka nacho. So hapo utajifunza kuchuja utambulisho wako.

Then, tukijifunza katika kujichunguza utaona kuwa tofauti kati ya wewe na mimi ni ufahamu wako. And ufahamu ndio unaacha mwili baada ya kufa. Hata kwa wanaoamini maisha baada ya kifo au hukumu baada ya kifo watakubali kuwa huwezi kuhukumiwa kama hauna ufahamu hivyo ufahamu wako unabeba mengi na ndio sehemu isiyoshikika katika sehemu zako zote za kifizikia na zisizo za kifizikia.

So, tukichunguza sana tunajifunza kitu fulani katika fumbo hilo.
 
mimi ni mimi

Ni kweli wewe kama ni wewe, lakini tambua kuwa kuna Oneness katika ulimwengu. Wewe ni mimi na mimi ni wewe lakini at the same time I Am That I am. Unapomkosea mwanadamu mwenzio unakuwa hujamkosea yeye bali umejikosea wewe kwani yeye ni sehemu yako wewe. Unavyoona kila mtu yuko kivyake kama wewe ni Illusion/Uongo/Mtihani. Ndio maana tunafundishwa mtendee mwenzio ambacho unapenda utendewe, kwa sababu unajitendea wewe. Unaposaidia mtu unajisaidia wewe, unapomuumiza mtu unajiumiza wewe bila kujua. Utakuja kujua
baada ya maisha yako umuhimu wake lakini kwa sasa ni kama mtihani kwako.

Hivyo inakupasa kuepuka ubinafsi.
 
Hili swali nilikua najiuliza sana kipindi nikiwa mdogo.Hasa nikikaa sehemu tulivu isiyo na kelele yoyote.Hadi nikawa najikuta najishangaa mwenyewe!
Lakini siku hizi kila nikijaribu nashindwa sijui kwanini!

Wow, asante sana. Hata mimi nilianza kujiuliza hili swali. Nilipokuwa naona watu wanazikwa najiuliza kuwa na mimi ipo siku nitazikwa, je mimi ni nani? Kwanini nauacha mwili wangu? Kuna muda unaamua kutafuta sehemu tulivu na kuanza kuvuta taswira ya maisha na kujikuta unaona kuwa kuna mengi ya kufahamu zaidi.
 
mtoa post nimemwelewa..... na ukitaka umwelewe zaidi you have to be genius and deep thinker
Truly. Nashukuru sana kwa kunielewa. Naamini fumbo hilo utalifumbua/umeshalifumbua katika maisha yako. Ubarikiwe sana.
 
Hiyo ni Yoga meditation steps.
Naona wameshamchanganya huyu. Nimetembelea mataifa mengi yanayofanya hiyo kitu naona wao wanafanya na Budha akiwa mbele.
Hata hapa hotelini Champ De lamar, Port Luis, Mauritis naona sanamu ya Budha.

Wanaweza wakawa wameweka statue ya Buddha kwa lengo la kama pambo na wengi wanapenda statue ya Buddha katika meditation kwani inawakumbusha kuwa watulivu na kukuonyesha mfano wa Lotus Pose katika mkao.

Buddha hana uhusiano na Yoga kwani alifundisha Meditation tu na sio Yoga japokuwa katika safari yake ya kujifunza kujitambua aliwahi kujifunza mpaka Yoga lakini alipenda Meditation zaidi. Yoga ina foundation kubwa sana katika Hinduism zaidi ya Buddhism. Lakini zote zina lengo moja.
 
The whole message ambayo ndio key ya hizi conversation sijaelewa where should I stand to identify my self
 
Sasa mkubwa, ntawezaje kukuelezea mimi ni nani wakati hautaki maelezo?
[/CENTER]
Wewe sio maelezo mengi unayotumia kujieleza kwa maana kuwa wengi wanajielezea na kujitambua kwa kazi zao, muonekano wao, hali zao, Vitambulisho vyao, jinsi media zanavyowaambia wao ni nani n.k hivi vyote sio sahihi kwani tunakufa na kuviacha. Utambulisho huu una muda na muda wake ni katika maisha yako tu ya hapa duniani, hivyo inahimiza kutafuta utambulisho wako wa kudumu ambao hauna mwisho.
 
Ni kweli wewe kama ni wewe, lakini tambua kuwa kuna Oneness katika ulimwengu. Wewe ni mimi na mimi ni wewe lakini at the same time I Am That I am. Unapomkosea mwanadamu mwenzio unakuwa hujamkosea yeye bali umejikosea wewe kwani yeye ni sehemu yako wewe. Unavyoona kila mtu yuko kivyake kama wewe ni Illusion/Uongo/Mtihani. Ndio maana tunafundishwa mtendee mwenzio ambacho unapenda utendewe, kwa sababu unajitendea wewe. Unaposaidia mtu unajisaidia wewe, unapomuumiza mtu unajiumiza wewe bila kujua. Utakuja kujua
baada ya maisha yako umuhimu wake lakini kwa sasa ni kama mtihani kwako.

Hivyo inakupasa kuepuka ubinafsi.

Kuna kitu unataka kukieleza ila hakielezeki hivyo tunakua hatukuelewi
 
The whole message ambayo ndio key ya hizi conversation sijaelewa where should I stand to identify my self
Look deeply within you, Ask your self "who am I?" Then every identity that come to the mind, observe it and criticize it if it have limitation of time and space. The whole concept is to eliminate all the negative identity we have learnt from the society, parents (who didn't spend time to find the truth), and to find our true identity that last and not taken by wordily end/death.
 
Back
Top Bottom