Umeshawahi kukosa huduma au msaada kwa kutokusalimia watu,

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
nikiwa nimetokea zangu kigamboni nikafika ferry kutafuta magari ya gongo la mboto, sikuwa mzoefu sana yanaoopatikana,

ikabidi nisogee kwenye daladala moja hivi iliyopaki ilikuwa ni mida ya mchana, ndani kulikuwa na dereva na kondakta wake,

kufika nakauliza, eti gari za gongola mboto zinapaki wapi,? wote wakawa wananitazama tu,

nikarudia tena kuuliza kondakta akataka kunijibu, dereva akamkatiza, kwani ameona watu hapa, angeona si angesalimia,

nikawa mnyonge muda huohuo naona gari za gongo la mboto kumbe zenyewe hazikai zikifika tu ni mwendo wa kugombania na kugeuka,

toka siku hiyo ikawa mwanzo na mwisho kutokusalimia watu njiani,
 
JUTAAA kuzaliwa Tanzania JUTAAA nakwambia JUTAAA.
Kenya tu hapo Nairobi ukimsalimia mtu anaweza kukuitia polisi bongo ni ny'a sana 😓
 
Miaka ya nyuma nilienda shuleni kuchukuwa cheti Cha O-level. Nilfunga bahasha kwenye baiskeli nikawa nikiendesha speed. Kuna wazee niliwakuta tunafahamiana, Kati yao kulikuwa na mmoja ana mgogoro wa shamba na familia yetu, alikuwa anang'ang'ania shamba letu.

Nikaona hakuna haja ya kusalimia, nikawapita kwa kasi kufika mbele nikagundua nimedondosha bahasha yenye cheti! Nikaanza safari ya kurudi taratibu kwa mguu huku nikiangalia barabarani kwa umakini kama nitaona bahasha.

Ghafla nikakutana wa wale wazee halafu lile zee lililokuwa Lina mgogoro wa shamba na familia yetu ndilo limeshika cheti changu anakisoma huku anawaambia wenzake "watoto wote wa huyu mwanamke (mama yangu) Wana akili Sana darasani.

Nikaanza kwa kuwasalimia na kuwabembeleza wanipe Ile bahasha. Lile zee likakazana kusema "ulitupita pale bila kutusalimia hivyo hatukupi hii bahasha, kwanza nachana hichi cheti" nilutamani nimuuwe.

Wenzake ndiyo wakawa wanamzuia asikichane, baadae Sana akanipa ila kwa mbinde sana cheti kikiwa kimekunjika-kunjika kama mchicha wakati muda mfupi uliopita kilikuwa kipya.

Tangu siku ile nikawa nikipita barabarani nasalimia hadi mbwa.
 
😅😅😅😅Aisee
 
Iliwahi nitokea ya kutosalimia kondakta nikamuuliza tu gari flani zko wapi? ,akanielekeza station tofauti makusudi wakati naelekea mdada flani muuza chakula alikua maeneo ya pale wanajuana akanifata akanambia dogo uwe unasalimia ,then akanisaidia station sahihi...Tangu siku hiyo lazma nianze kumsalimia mtu ata mtoto mdogo😅😅
 
JUTAAA kuzaliwa Tanzania JUTAAA nakwambia JUTAAA.
Kenya tu hapo Nairobi ukimsalimia mtu anaweza kukuitia polisi bongo ni ny'a sana [emoji29]
Ha ha nimewahi fanya kaz na Wakenya, asubuh anawakuta straight anauliza shida yake hakuna salamu. Ilibidi tuwazoee tu wale jamaa
 
Na ndo sehemu zilizoendelea zilivyo.
Huku bongo ujamaa mwingi alafu hauna maana eti nikusalimie wewe Lavit kwa kuogopa kupatwa shida na usinisaidie 😂😂😂

Shida ya nyokweee
 
Iliwahi nitokea ya kutosalimia kondakta nikamuuliza tu gari flani zko wapi? ,akanielekeza station tofauti makusudi wakati naelekea mdada flani muuza chakula alikua maeneo ya pale wanajuana akanifata akanambia dogo uwe unasalimia ,then akanisaidia station sahihi...Tangu siku hiyo lazma nianze kumsalimia mtu ata mtoto mdogo😅😅
😅😅😅😅😅
 
Back
Top Bottom