Umeshawahi kukutana na mtu aliyepandisha jini/ mwenye majini? Tupe uzoefu wako

Kaka yangu alimwacha mke wake wa kijijini akaoa wa mjini, binti wa kizaramo. Binti anapandisha mashetani, eti anataka cheni na pete za gold. Kaka akamnunulia, baada ya wiki mbili majini yanataka tea simu enzi hizo imetoka S9 Samsung. Akampiga mateke na mabao, majini yakakoma
 
Kama unawasiliano nae mwambie anirushie majini yake PM

Harafu chief ile story yako ya baba mkwe iliishia wapi?
 
Nimeshuhudia sana matukio ya watu wakipandisha majini ila kuna tukio ambalo sitolisahau, kuna siku mida ya jioni nimekaa zangu kibarazani nyumbani kwa rafiki yangu mara ghafla kwa nyumba ya mbele na nilipokaa(kwa rafiki yangu pia) namuona binti anatoka nje na kanga moja (bila kufuli) huku akionekana ametoka kuoga. Nilipoona vile tu nikajua wazi huyu kapandisha akiwa bafuni maana nilikuwa namfahamu na najua kuwa ana hilo tatizo la kupandisha jini,sasa mtihani ukawa nafikiria naendaje kumzuia na hali ile ya kanga moja maana kumzuia kwake pale lazima tu utumie sana nguvu na lazima umkumbatie ndio utaweza kumzuia na kibaya alikuwa anaelekea sehemu yenye kiwanja ambapo kuna watu wengi maana watu walikuwa wakicheza mpira(cha ndimu). Basi ikabaki namuangalia tu nafikiria nifanyaje na sikutaka kuwaambia watu pale wanisaidie kumkamata maana hadi muda huo watu waliyokuwepo pale hawakuwa wanamzingatia hivyo hawakuwa wakijua kibachoendelea.

Basi mpaka nakuja kufanya maamuzi ya kuwaambia kwao yule binti keshafika uwanjani huko kwenye watu wengi hivyo kilichotokea ni kwamba alidharirika sana yule binti wa watu maana kadri alivyokuwa anazuiliwa zile purukushani basi ndio alikuwa anazidi kukaa uchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…