Hahaha kuna siku nimetoka Tabata nakuja Ubungo, kuna watu wana IST mbele wanasua sua nikawapigia horn nyingi na nawawashia taa maana walikua sambamba na roli. waliposogea pembeni niliwaovertake kibati sana, nafika mataa ya External AC ikaanza toa joto, gari inatikisika feni ipo maximum, taa ya coolant inawaka, taa ya overheating ya njano ikawaka dakika 2 mbele ikawa nyekundu, weee.. kwenye bonnet ulitokwa mlipuko sijawah usikia. Nasimama wale wenye IST ndio waliokuja nisukuma nikaweka pembeni pale njiapanda ya Mabibo hostel. water pump ilikua imenifia. aisee nilikonda ndani ya week 1 kupata ile pump.