Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Kwa mara ya kwanza nilikidhi vigezo vya kupiga kura mwaka 2005, hata hivyo sikuwahi kupiga kura mpaka mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kulipovuma sana wimbi la mabadiliko, tangu wakati sijawahi kushiriki uchaguzi mwingine wowote tena baada ya kugundua kura yangu haibadilishi chochote. Hii inamaanisha katika chaguzi tisa (za serikali kuu na za mitaa) za nchi hii (pamoja na wa mwaka huu) nimeshiriki uchaguzi mmoja tu.