Sasa kinachokufanya ukeshe humu JF unaongea siasa ambazo huna mchango wowote nini? Au stress? Wenzako tumeanza kupiga kura 1995 Gairo huko, Mgombea Ubunge wa CCM akiitwa Shaweji baada ya kufariki Sk. Chiduo na mpinzani wake akiwa Kibibi Senyagw wa NCCR MAGEUZI! Hadi leo tunapiga kura ndio maana unaona mambo yanaenda!Kwa mara ya kwanza nilikidhi vigezo vya kupiga kura mwaka 2005, hata hivyo sikuwahi kupiga kura mpaka mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kulipovuma sana wimbi la mabadiliko, tangu wakati sijawahi kushiriki uchaguzi mwingine wowote tena baada ya kugundua kura yangu haibadilishi chochote. Hii inamaanisha katika chaguzi tisa (za serikali kuu na za mitaa) za nchi hii (pamoja na wa mwaka huu) nimeshiriki uchaguzi mmoja tu.