Umesoma majengo sec 1988-2010?

Daniel Mjema

Member
Joined
Jul 23, 2007
Posts
77
Reaction score
84
Ndugu zangu,
Shule ya sekondari Majengo iliyopo mjini Moshi itaadhimisha Jubilee ya miaka 25 mwezi Oktoba 2011. Ili kupamba maadhimisho haya imeonekana ni muhimu wanafunzi wote waliomaliza katika shule hii kati ya 1988-2010 wawepo siku hii muhimu kwa historia ya shule hii. Wewe kama ni mmoja wa waliomaliza katika shule hii tafadhali sana tunakuomba uwasiliane na Mwenyekiti wa muda wa wanafunzi waliomaliza majengo secondari kwa simu namba 0715 432243 au email danielmjema@yahoo.com AU danielmjema@gmail.com ukitoa taarifa muhimu ya lini ulimaliza majengo, kwa sasa uko wapi na unafanya nini na kama unathibitisha ushiriki wako. Maadhimisho haya hayatanoga pia kama wale waanzilishi wa shule kwa maana waliomaliza 1988 hawatahudhuria. Tafadhali mjulishe na mwenzako.
Karibuni
 
Tuko pamoja kaka nimemaliza hapo FORM 6, 2004 ni shule nzuri nilifundishwa elimu na nidhamu hapo ya hali ya juu! BR,LIYMO mr Lago, mushi B ,lyatuu ,viongozi shupavu wamenifanya niwe mpiganaji mzuri tu. I LOVE MAJENGO SEC !
 
KISS THE GROUND!!!

Wow, I didnt know this...nimesoma hapo bwana A-level 2005-2007.
I enjoyed chakula cha waalimu (ukiwa kiongozi,lol)...
...most of all I loved the Library, I could stay in there asubuhi mpaka jioni! Santimes yule bibi alikuwa ananifukuzaga! dah..

Sadly, I wiill not make it for th celebrations..nitakuwa porini..but on that day i will surely remember to say a prayer for the school..tutakuwa pamoja kiroho!!!
PAMOJA SANA...
 
Dah, umenikumbusha mbali mkuu. Nimesoma majengo form 1-6. Dah, nawakumbuka sana kina Lyatuu, Mlay, Prof Makundi, Mr. Sendoro(RIP), Mr James, Papaa Kichawele.. Duh, ntakuwepo.
 
Du, hata mimi ni mdau nilimaliza hapo form 4 mwaka 1993, nawakumbuka bother Pius Kihuru, Lyatuu, Kandia, nimewasahau wengi. Tutakuwa pamoja.
 
dah yani hamuwez amini leo thru fb 2lipanga 2kutane 2liomaliza pale o level mwaka 2001,maeneo ya coco beach,majengo noumer,unakumbuka msosi wa walimu eh,esp maharage yaliyoungwa matamuuu,namzika mwl james na mushi b
 
Nawashukuru wote mliocguswa na tukio hili ambalo litatokea tena baada ya miaka 25 mingine ijayo. Nawaomba mnitumie email danielmjema@yahoo.com AU danielmjema@gmail.com au ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwenda namba 0715 432243 au 0754 432243 ukitaja jina kamili, ulimaliza lini na sasa uko wapi ili tuandae taarifa itakayosomwa siku hiyo na kuwekwa pia kwenye website ya shule. Naomba ushirikiano wenu ili siku hiyo tukumbushane kila mmoja kwa staili yake anavyokumbuka alikopita hadi sasa.
 
Hongereni sana Majengo Sec.Alumni... japo mm sikusoma Majengo lakini nimeipenda hii spirit..sii vibaya mkipeleka tangazo Radioni...kwani wasikilizaji ni wengi... Japo pia Umeme unaweza kuwa kikwazo...
 

Peleka habari pia Facebook kaka..kuna group ya Majengo kule...this is great news.
Mimi pia naruhusiwa kukutmia habari hata kama sitokuwepo!??
 
Nimefurahi coz Mj Sec tupo wengi jf,nami pia nilisoma Majengo sec A-level(2005-2007).Namkumbuka sana brother Peter limo na usemi wake ''kiss the ground'' mwalimu Januari ambaye alisadikika anavuta 'bangi' mwalimu fitris,mwalimu magembe na wengine wengi.
 
Tupo pamoja wakuu nimemaliza 6 mwaka 2006, ninawakumbuka sana walimu hawa Br Lyimo mkuu wa shule, Mr. Makundi, Mr. Maghembe, Mr.Mlay, Kichawele, Lyiatuu, Mr. James, Mr. Minja Mr. Sendoro (RIP)etc.
 
Ctosahau cku niloambiwa nipge pushap na brother peter lymo in 2009 kpnd npo 6...wl neva 4get Majengo sec na mambo ya kutoboa fens
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…