Umesoma shule ya boarding(bweni) wewe?

Umesoma shule ya boarding(bweni) wewe?

Nimesoma boarding advance ambapo skonga kwetu palikuwa na o'level pia so ilikuwa board form one to six tena mixture. Ambacho sitasikisahau ni pale wasichana wawili warembo wa kidato cha nne walipokamatwa kwa wizi mkubwa. Kati ya vitu walivyoiba ni t shirts zaidi ya 70,chupi za kutosha za wenzao, viatu pea nyingi mno!!,sidiria, sketi,mashati,soksi na vingine vingi!!! Waliletwa assemble na kila mmoja kukiri kosa hilo!! Cha ajabu walikuwa makauzu hata soni hawakuona looh!!!! Ilikuwa hatari

si kweli!!
 
Nakumbuka skuli kwetu umeme ukikatika mida ya night utasikia watu wakipiga kelele NO GAP EMERGED
 
ebwanaeeeeeehh!!!!..... sitokaa nisahau hiki kisanga!!

nakumbuka ilikuwa ni fainali ya uefa, kati ya MAN U na BARCA, mwaka 2011!!!!!!

nakumbbuka siku hiyo tulitoroka skuli pipo kibao!,,, huku tukiwa na wasiwasi na ticha mnoko (huyo ticha alikuwa akikukamata una kosa hata la kusahau kumsalimia!!!,, jua wewe una stiki kama nane matakoni... chezea kahororo wewe!!)

basi siku hiyo tulisepa usiku kwa tahadhari kubwa sana, katika mishe mishe za kumkwepa mnyama!!!! (huyo ticha!),, mara ghafla, kwa msaada wa mwanga wa pikipiki, tukamwona mbele yetu!!! just hatua kama 15!!!

hahahaaaaa!!!! nakumbuka jamaa yangu mmoja alikimbilia kwenye mji wa mtu na kujikuta yuko sebuleni!!!

...... sitosahau hii ishu!!.......

kahororo for life!
 
Basi akili zenu ndogo sanaa mbona tumeenda club na onetumepata ingekuwa nyie mnafanya hivyo kama sisi wenye vipaji mngepata four na zero hahaha

ndugu yangu darasa la saba nilifaulu kwenda kibaha lakini nikaopt kwenda seminari nikiamini seminarini kuna malezi ya aina nne intellectual,pastoral,spiritual and discipline formations na hayo ndo malezi yaliyonijenga mm....hongera kwa kuwa ulikuwa ukienda disco mimi muda huo nilikuwa kanisani nasali nikijiweka karibu zaidi na muumba na hakika ndie yeye muumba alietuwezesha tukapata hizo one na si kwa juhudi zetu.......
 
haya ngoja nianze,
Siku ya wali na nyama ilikuwa ni siku ya furaha sanaa, raha ni ile siku ya kwenda disco kwa marwasaw kama huna uniform nzuri lazma uazime ili ukienda disco usije ukakosa demu
Nakumbuka adhabu ya kukata kuni kipimo cha cubic metre moja. Wali tulikuwa tunaita cheche. Siku ya disco kila mwanafunzi alijitahidi kununua mafuta ya mgando yenye manukato yaliyojulikana kwa jina la YOLANDA. Kuna kiranja mmoja wa chakula alikamatwa na kilo 8 za nyama alikuwa anataka kupeleka town ili kuipiga bei,baada ya wk 1 alifukuzwa shule. Wanafunzi walikuwa wanavamia mashamba ya kijijini na kuiba mazao kama vile miwa, mihogo, mahindi n.k. Kidato cha pili walikuwa wanawaonea sana kidato cha kwanza kwa kuwacharaza bakora usiku wakiwa usingizini. Kwa leo inatosha.
 
Kuna siku mdada wakijijni alikua kalewa basi bhana akajichanganya akaingia Bweni la Boys.. Ilikua sa 1 usiku na umeme umekata.. Ilikua raaaaaaaha
 
nilisoma shule ambayo tulikuwa na uoga wa Mungu na tulijua nn kilitupeleka shule,tulikuwa tukisali,tulijifunza kilimo na hasa maadili na hakika hatukuwa na cfa za ajabu kama za kwako ww...

Pamoja sanaa mtumishi endelea hivyohivyo
 
KIMUKI kwa anaiyeijua????wakati muafaka wa kutoka na mbuni,ha ha ha ha wapi PETER TINO,KILOKA,.......,nakumbuka kiongozi mmoja alimgonga mbuni mmoja juu ya mikate ya wanafunzi jikoni(agghaaaaaaaa!!!!) akakamatwa na kumwagwa fasta,yaani ni uchafu kwa kwenda mbele.
 
Wakuu naomba tukumbushane vituko,mikasa,na mambo mbalimbali uliyokumbana nayo wakati unasoma shule ya sekondari ya bweni(boarding),
Nakumbuka tulikuwa tunakula ugali umepoa kinoma mida usiku kwenye saa sita au saba hivi baada ya kutoka msuli...alafu nguna ilikuwa inatunzwa uvunguni no kufunikwa wala nin panya wanakatiza juu yake ila hatuugua hata siku moja.....Mungu kumbe anawapenda wanafunzi.............:smile:
 
mtwara girls tuliitwa Vinyoya, Chidya boys tuliwaita Mbwa mwitu coz shule yao ipo milimani
 
ndugu yangu darasa la saba nilifaulu kwenda kibaha lakini nikaopt kwenda seminari nikiamini seminarini kuna malezi ya aina nne intellectual,pastoral,spiritual and discipline formations na hayo ndo malezi yaliyonijenga mm....hongera kwa kuwa ulikuwa ukienda disco mimi muda huo nilikuwa kanisani nasali nikijiweka karibu zaidi na muumba na hakika ndie yeye muumba alietuwezesha tukapata hizo one na si kwa juhudi zetu.......
huna lolote wewe muongo mkubwa,seminary gani hio?kama mlifunzwa discpline mbona kila siku unapigwa ban kwa matusi yako,tambaa zako acha kuongopa
 
Nakumbuka tulikuwa tunakula ugali umepoa kinoma mida usiku kwenye saa sita au saba hivi baada ya kutoka msuli...alafu nguna ilikuwa inatunzwa uvunguni no kufunikwa wala nin panya wanakatiza juu yake ila hatuugua hata siku moja.....Mungu kumbe anawapenda wanafunzi.............:smile:
mwanafunzi hafi,hata akifa haozi,hata akioza hanuki,hata akinuka ananukia marashi.

Huo ndo ulikua msemo wa kujipa moyo kabla hujala bila kunawa na wakati huo kipindupindu kilikua kinatisha.
 
Special diet haswa ukiandikiwa E.D lakini makiranja ya bwalo yalikuwa magumu kukubali.
kipindi hicho mkitoka class mchana baada ya chakula inafuata self reliance,kufanya kazi yeyote iwe usafi,kwenda shamba,kupalilia etc,nilikua special duty yani mda huo mimi niko ofisini English department ,wazungu walikua wanaleta misaada ya vitabu kazi yangu ikiwa ni kuviregist na kuvipa namba,ndipo nilipoupatia ulevi wa kusoma novel.
 
Back
Top Bottom