Mpigamsuli
JF-Expert Member
- May 24, 2012
- 3,885
- 582
- Thread starter
-
- #121
sisi tulikuwa buzy tukitafuta one...hatukuwa na huo upuuzi..
kwann co wote mliopata hizo one...sisi mbona wote tulipata one..
Teh mkuu mie mboyzia banaa..............ulisoma Milambo wewe!!!
Nimesoma boarding advance ambapo skonga kwetu palikuwa na o'level pia so ilikuwa board form one to six tena mixture. Ambacho sitasikisahau ni pale wasichana wawili warembo wa kidato cha nne walipokamatwa kwa wizi mkubwa. Kati ya vitu walivyoiba ni t shirts zaidi ya 70,chupi za kutosha za wenzao, viatu pea nyingi mno!!,sidiria, sketi,mashati,soksi na vingine vingi!!! Waliletwa assemble na kila mmoja kukiri kosa hilo!! Cha ajabu walikuwa makauzu hata soni hawakuona looh!!!! Ilikuwa hatari
Basi akili zenu ndogo sanaa mbona tumeenda club na onetumepata ingekuwa nyie mnafanya hivyo kama sisi wenye vipaji mngepata four na zero hahaha
umesomea wapi mkuu?
Nakumbuka adhabu ya kukata kuni kipimo cha cubic metre moja. Wali tulikuwa tunaita cheche. Siku ya disco kila mwanafunzi alijitahidi kununua mafuta ya mgando yenye manukato yaliyojulikana kwa jina la YOLANDA. Kuna kiranja mmoja wa chakula alikamatwa na kilo 8 za nyama alikuwa anataka kupeleka town ili kuipiga bei,baada ya wk 1 alifukuzwa shule. Wanafunzi walikuwa wanavamia mashamba ya kijijini na kuiba mazao kama vile miwa, mihogo, mahindi n.k. Kidato cha pili walikuwa wanawaonea sana kidato cha kwanza kwa kuwacharaza bakora usiku wakiwa usingizini. Kwa leo inatosha.haya ngoja nianze,
Siku ya wali na nyama ilikuwa ni siku ya furaha sanaa, raha ni ile siku ya kwenda disco kwa marwasaw kama huna uniform nzuri lazma uazime ili ukienda disco usije ukakosa demu
nilisoma shule ambayo tulikuwa na uoga wa Mungu na tulijua nn kilitupeleka shule,tulikuwa tukisali,tulijifunza kilimo na hasa maadili na hakika hatukuwa na cfa za ajabu kama za kwako ww...
Nakumbuka tulikuwa tunakula ugali umepoa kinoma mida usiku kwenye saa sita au saba hivi baada ya kutoka msuli...alafu nguna ilikuwa inatunzwa uvunguni no kufunikwa wala nin panya wanakatiza juu yake ila hatuugua hata siku moja.....Mungu kumbe anawapenda wanafunzi.............:smile:Wakuu naomba tukumbushane vituko,mikasa,na mambo mbalimbali uliyokumbana nayo wakati unasoma shule ya sekondari ya bweni(boarding),
Eb kumbukaNimesahau..
Pamoja sanaa mtumishi endelea hivyohivyo
Pamoja sanaa mtumishi endelea hivyohivyo
huna lolote wewe muongo mkubwa,seminary gani hio?kama mlifunzwa discpline mbona kila siku unapigwa ban kwa matusi yako,tambaa zako acha kuongopandugu yangu darasa la saba nilifaulu kwenda kibaha lakini nikaopt kwenda seminari nikiamini seminarini kuna malezi ya aina nne intellectual,pastoral,spiritual and discipline formations na hayo ndo malezi yaliyonijenga mm....hongera kwa kuwa ulikuwa ukienda disco mimi muda huo nilikuwa kanisani nasali nikijiweka karibu zaidi na muumba na hakika ndie yeye muumba alietuwezesha tukapata hizo one na si kwa juhudi zetu.......
mwanafunzi hafi,hata akifa haozi,hata akioza hanuki,hata akinuka ananukia marashi.Nakumbuka tulikuwa tunakula ugali umepoa kinoma mida usiku kwenye saa sita au saba hivi baada ya kutoka msuli...alafu nguna ilikuwa inatunzwa uvunguni no kufunikwa wala nin panya wanakatiza juu yake ila hatuugua hata siku moja.....Mungu kumbe anawapenda wanafunzi.............:smile:
kipindi hicho mkitoka class mchana baada ya chakula inafuata self reliance,kufanya kazi yeyote iwe usafi,kwenda shamba,kupalilia etc,nilikua special duty yani mda huo mimi niko ofisini English department ,wazungu walikua wanaleta misaada ya vitabu kazi yangu ikiwa ni kuviregist na kuvipa namba,ndipo nilipoupatia ulevi wa kusoma novel.Special diet haswa ukiandikiwa E.D lakini makiranja ya bwalo yalikuwa magumu kukubali.