Umesoma vitabu gani mwaka 2020?

Umesoma vitabu gani mwaka 2020?

Habari wakuu? Ni mwisho wa mwaka. Tutafakari usomaji wetu wa mwaka huu. Vitabu vingi nimevijua kupitia michango ya members humu.

Mi nimesoma vitabu vichache tu, sikuwa na usomaji mzuri.

1. Screw business as usual cha Richard Branson.

Anaeleza jinsi biashara zinaweza kubadilika na kuweka jamii kwanza badala ya faida kwanza. Anasema biashara zinazoweka faida mbele zitapotea. Anaeleza pia jinsi misaada inavyopaswa kubadilika na kulenga ujasiriamali unaotatua matatizo ya kijamii badala ya kuwapa tu watu vitu. Kina mifano mingi kutoka Africa. Nilienjoy kukisoma.

2. Surveillance valley: The secret military history of the internet cha Yasha Levine.

Kitabu kizuri sana. Kinaeleza jinsi internet ilivyoanza na jinsi toka mwanzo ilikuwa ni chombo cha upelelezi.

3. David and Goliath cha Malcom Gladwell. Hiki sikukimaliza. Kilikuwa kimepondwa sana kwenye reviews lakini nilienjoy mpaka nilipofikia. Anazungumza mambo yanayofanya underdogs wa-shine.

4. The country of the blind cha HG Wells.
Jamaa anaenda nchi ya vipofu watupu.

5. The pearl cha John Steinbeck.

Jamaa masikini anapata lulu kubwa sana.

6. Hichhiker guides to the galaxy. Bado nasoma hii series ya vichekesho. PAULA unamkumbuka Bowerick wowbagger the infinitely prolonged?

7. Adili na Nduguze cha Shaaban Robert. Nimeisoma tena hii hadithi.

8. Njama cha Musiba.

9. Naandika Novel ipo kama 90%. Naona kama iko poa sana.

Vipi wewe, umesoma vitabu gani mwaka 2020?
1. The Richest Man in Babylon - George Samuel Ckason
2. Think and Grow Rich - Napoleon
3. 6 Golden Rules of Building wealth
4. The Power of Self Discpline
5.Millionare Mindset course
6. End of Days - Sylvia Brown, Lindsay Harrison
7. Afica's Hidden History - Credo Mutwa
8. 1st Council of NICEA - Dean Dudley
9. Religions Exposed - Philmore Akhenaten Carter
10. Currency Trading for Dummies - Brian Dolan
 
Mkuu umenunua hard copy au umesoma softcopy.kuna kitabu nimekicheki kinagonga laki moja mwe nikaamue nipotezee.Vitabu hard copy ni ghali sana.
Nilivutiwa na OSHO, jamaa alikuwa ana library kubwa sana Nadhani hakuna mtu mwenye library kubwa kama ile.Jamaa alikuwa anajua sana mambo ya werevu
Ukisoma sana vitabu unakuwa unajua kila kitu, af wanaokuzunguka wanaanza kukuona kama unajua kila kitu, unawashinda hoja kisha wanakubatiza jina.
Mkuu

Mimi huwa nasoma softcopies, ukiangalia katika Titles hapo juu hakuna hata kimoja utakachokikuta bookstores za Bongo labda uagize Amazon

Hivyo vitabu ni ghali sana huko Duniani, Mfano kitabu cha Breakthrough Advertising bei yake ni zaidi ya Million. Sina uwezo huo 😂

Na kuhusu hilo swala la kubatizwa majina ni kweli, vitabu vinakujengea uwezo wa kuwa na uono mpana sana tofauti na wale wanaokuzunguka, ikitokea ukawa muelewa wa mambo mengi sana wengine wanaanza kukuita Muongo

I remember nishaitwa a man who knows more than Google, hii sio compliment Bali wananisadifu kwamba mimi ni Muongo 😂😎

Tujenge mazoea ya kusoma vitabu!
 
Hiki the monk who sold his ferrari kinanipigia sana kelele. Kila kona nakutana nacho. Huwa naogopa vitabu vya hivi(self help). Nisaidie summary yake, labda ntakijaribu.
Doooh....Kitafute ukisome..Mimi Nilinunua 2500 TU online nikasoma kwa simu...Ni kizuri..kinafikirisha.
 
Mkuu

Mimi huwa nasoma softcopies, ukiangalia katika Titles hapo juu hakuna hata kimoja utakachokikuta bookstores za Bongo labda uagize Amazon

Hivyo vitabu ni ghali sana huko Duniani, Mfano kitabu cha Breakthrough Advertising bei yake ni zaidi ya Million. Sina uwezo huo 😂

Na kuhusu hilo swala la kubatizwa majina ni kweli, vitabu vinakujengea uwezo wa kuwa na uono mpana sana tofauti na wale wanaokuzunguka, ikitokea ukawa muelewa wa mambo mengi sana wengine wanaanza kukuita Muongo

I remember nishaitwa a man who knows more than Google, hii sio compliment Bali wananisadifu kwamba mimi ni Muongo 😂😎

Tujenge mazoea ya kusoma vitabu!
Mzee hii kitu "Breakthrough Advertising by Eugene Schwartz" plz my email is samsonibahati@gmail, I will exchange some books too
 
Hivi Screenshot_2022_0813_154105.jpg
 
Back
Top Bottom