Umesoma vitabu gani mwaka 2021?

Nmemaliza mwaka with this book by Curtis Jackson aka 50 Cent ni kizuri sana aina ya uandishi aliyotumia will make you read it non stop ameelezea maisha yake na mziki challenges alizopata,mkasa wake wa kupigwa risasi tisa na bado akainuka,pia kina principles nzuri za maisha ambazo alitumia mpk kufika hapo alipo, yan nlivosoma hichi kitabu ndo nimegundua mziki Marekani unalipa sanaa ndo maana Wasanii wa mbele kuwa na expensive things ni kawaida this book is great
 
Apple store haipo bado. Na kwenye android ni Tz na Kenya tu.
Asante sana. Mimi navitafuta sana vitabu vya Shaaban Robert nisome. Ninacho cha Kusadikika. Na vingine pia nilishavisoma ila nataka tu kuvirudia. Zamani sekondari walikuwa wanavitumia kwenye fasihi. Sijui kama siku hizi bado vinatumika lakini mimi nadhani ili kumuenzi Shaaban Robert ilitakiwa vitumike ili kila mtanzania amsome. Vina fasihi nzuri sana na mafundisho yake ni mazuri. BTW nime-note wewe ni mpenzi wa vitabu. Kuna kitabu cha Trevor Noah kinaitwa Born Crime umeshakisoma? Kama bado basi jitahidi ukisome. Pia kuna kitabu kinaitwa ''I heard you paint houses'' kinaelezea kisa cha kweli kuhusu kupotea kwa Jimmy Hoffa, aliyekuwa kiongozi wa vyama vya wafanyakzi USA. Nacho ni kizuri mno. Na movie yake ipo inaitwa ''The Irishman'' (2019)
 
Shaaban yupo vizuri sana. Ni mtu anayestahili tuzo za kimataifa. Kwenye app vipo vitabu vyake vitano(nilivyoorodhesha). Bahati mbaya ndiyo inapatikana Tz na Kenya kwenye android. Born a crime nimekisoma maana Noah namkubali sana, kitabu kizuri.

Nilicheki movie ya The Irishman. Inaonekana kuna mambo mengi sana yalikuwa yanamzunguka huyo bwana(Pacino). Kitabu hicho nimeshaweka kwenye list ya mwakani. Shukrani sana.
 
Kuna kipindi nilipata passion ya kusoma vitabu sijui iliyeyukia wapi, BTW nilifanikiwa kusoma
1. Rich dad, poor dad
2. Think big
3. The Monk who sold his ferrari
4. As a man thinketh
5. Power of subconscious mind
5. How to win and influence people ( sikumaliza)
6. Fools die ( sikumaliza ) .... na vingine vingi nimegusa kidogo
 
Hivyo vitabu vya Kiswahili unavipata wapi on line?
 
Mwaka huu nimeamua kusoma vitabu vya Simulizi binafsi za watu (Autobiography na biography) zaidi na vingine tofauti vichache. Vitabu nilivyosoma ni;

1. Muhammad Ali his life and times- by Thomas Hauser


2. My life- by Bill Clinton


3. Jackal - Carlos the jackal


4. The Man of Honor (Joseph Bonano) - by Sergio Lalli


5. Autobiography of Martin Luther King Jr- by Clayborne Carson


6. Mob Star The Story of John Gotti- by Gene Mustain



7. It's all about Muhammad (Prophet Muhammad)- by F. W. Burleigh


8. King David- by Steven L. Mackenzie


9. Michael Jackson- by J. Randy Teraborreli


10. Emperor's of Rome- by David Potter


11. The World dangerous secret societies- by James Jackson


12. The Tipping point- by Malcolm Gladwell





View attachment 2054130
 
Hivyo vitabu vya Kiswahili unavipata wapi on line?
Sehemu mbalimbali. Kuna vichache kama viwili vitatu nilivipata Kindle. Vingine nilinunua Mkuki na nyota( vya Shaaban na Kezilahabi). Vingine niliagizia Abebooks, vile vya zamani kwaajili ya app. Cha Bulicheka nilikipata duka la vitabu Peramiho.

Kuna hawa wachapishaji watawa wa Peramiho na Ndanda, wana vitabu adimu sana.

*Kumbe ulisema online, Kindle vipo vichache maana waliacha kuweka vitabu vya kiswahili. Pia kuna app kama UWARIDI, Sim Gazeti na hiyo maktaba, unaweza okoteza.
 
Hivyo vya on line unaweza kunisaidia? Please
 
Hivyo vya on line unaweza kunisaidia? Please
Kwenye hii maktaba app(by pictuss), karibu vitabu vyote vya kiswahili nilivyoorodhesha hapo vipo. Kasoro hivyo vitatu vya Kezilahabi. Ukipakua hiyo app unasoma bure, na unasoma hata ukiwa offline.
 
Sijui ni Tawasifu! Tawasifu gani kali zaidi hapo?
 
Nimesoma vitabu zaidi ya 50; vyengine hivyo ambavyo umeviweka, ila When breath becomes air hiki ni kitabu kizuri mno. Mbinu niliotumia ni kusoma vitabu zaidi ya vitatu kwa wakati mmoja. Nikimaliza chapter ya kitabu hiki badae naenda chengine.
 
Nimesoma vitabu zaidi ya 50; vyengine hivyo ambavyo umeviweka, ila When breath becomes air hiki ni kitabu kizuri mno. Mbinu niliotumia ni kusoma vitabu zaidi ya vitatu kwa wakati mmoja. Nikimaliza chapter ya kitabu hiki badae naenda chengine.
Mkuu tumemiss nyuzi zako, vichwa vyetu vimemiss madini yako ya upande wa kiroho.
tilmikha
 
Sijui ni Tawasifu! Tawasifu gani kali zaidi hapo?
Karibia vyote! Lakin nimependa zaidi
1. Muhammad Ali- Nimeweza mjua zaidi ya kumuona anapigana ngumi, alikuwa philosopher and orator, a proud of black race. Pia kujua yaliyokuwa yanaendelea kambini wakati anajiandaa na mapambano yake makubwa.
2. Michael Jackson- Nimekuja kumjua jamaa vizuri, a selfish person, who liked to blame others for his problems ( Kama ambavyo anamlaumu baba yake kuwa alikuwa anampiga na kumtania kuwa ana pua kubwa, kuwa ndio sababu kubwa ya yeye kuchonga pua.. uongo mtupu!, Au watu wanavyolaumu wazungu kuwa ndio waliomdanganya abadili rangi .. uongo mtupu! Ni yeye mwenyewe, sema siku zote amekuwa mjanja kuwaaminisha watu). Inaelezea maisha toka utotoni mpaka kufa. Utamjua vizuri
3. Martin Luther King Jr- Mchango wake kwa negroes ni mkubwa sana
4. King David- Utaona vitu vingi kwenye biblia vimeandikwa uongo ili kukamilisha propaganda flan iliyokusudiwa na watu walioandika biblia.. lakin pia jinsi biblia yenyewe inavyojicontradict
5. Muhammad- Historia yake na maswali utajiuliza kuhusu hizi dini na imani ( mfano hapo watu wanapoenda kuhiji Hilo jiwe la kaaba, ni mahali wapagani walikuwa wanahiji miaka maelfu kabla hata hajazaliwa Muhammad, ilikuwaje mahali walikuwa wanahiji wapagani pawe sehemu takatifu?) Unazipata zile za ndaani kabisa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…