Inasemekana kuwa katika Mapenzi na Vita, chochote kinafaa, zikiwemo mbinu safi na chafu, na wala sio kama tunavyotaka iwe kuyaona Mapenzi kama barabara iliyopambwa kwa mawaridi. Hii ni kwa sababu kwanza, kama ambavyo kuna mapenzi, vilevile kuna chuki/kutoendelea kupenda, pili kama ambavyo huzaliwa, vilevile yanakufa; na linapotokea moja katika haya manake "hakuna mapenzi tena" na kubali matokeo.
Labda tunachoweza kuwalaumu ma-ex wetu ni kutokuwa wawazi. Ikiwa kaamua kurejesha majeshi, ni sawa tu lakini sio tena anaanza visa na vyengine vya kuudhi sana. Wengine hawachukui hio. Mimi binafsi, kama ingekuwa kila baada ya kuumizwa unabakia na chale usoni, wangu ungekuwa kama sanamu ya kimakonde. Lakini kila ikitokezea, "ninajipangusa michanga, ninaweka sawa magwanda/kombati" safari inaendelea, ninaishi, na sio kukaa tu ninalalamika nilivyotendwa. Sifikiri kama nimewahi kumtenda mtu, kwani daima nimekuwa muwazi na mkweli. Sera yangu "bora nikuumize kwa ukweli kuliko kukufariji kwa uongo".