Umeumizwa moyo mara ngapi mapenzini?

Umeumizwa moyo mara ngapi mapenzini?

Once never 2 b 4gtn!!! even 2dy it makes me cry!!!! Tatizo Wazazi....mmmhhhhhhhh
 
nshaumiza mara moja sijawahi kuumizwa.....

Kama nyinyi waumizaji msingekuwapo ina maana watu wasingeumizwa.. Shosti si vyema kuumiza wenzio.... ona sasa watu wanavyolalamika kuumizwa humu.. na wewe yuko anaye kulalamikia kwa kumuumiza....:A S cry::A S cry:
 
mtu anayeumizwa mara ya mwanzo then ikatokea kuumizwa tena zaidi kwa mara nyengine, basi huyo kajitakia. Moyo wa mtu siwezi kuujuwa ukoje, hivyo siwezi kusema nimeumiza mara ngapi ila ni mara moja tu niliyoumizwa na sidhani kama inaweza kutokea kuumizwa kwa mara nyengine.

ACHA TU,Hayajakufika mshukuru Mungu
 
Mara 2n ila ya pili sitakaa nisahau.
wa kwanza nilimfumania kwa ushaidi wa 99.99% maana walikua wamelala wote kitandani wamejifunika ilikua asubuhi,
kuvuta shuka,kama walivyozaliwa!!!!
Mwanaume anadai hawakufanya chochote.

Ya pili sikuona chochote ila nilikua masomoni basi ikawa kila asubuhi sana au usiku wa manane napokea simu ya kijana anaongea mwanamke ananipa ukweli wa yaliyotendeka walivyolala.
ilikua wiki nzima,kaka anajifanya hajui lolote wakati inatumika namba yake.
Loh!
 
mapenz sio ya kuyaendekeza sana yatakugeuza chizi...just relax and enjoy life,when u met a snitch just quit early

'MIMI NINA MSEMO WANGU AMBAO SIKUZOTE UNATEMBEA KICHWANI...KWAMBA SIKUZALIWA NA MTU NA WALA HAKUNA ALIYEUMBWA KWA AJILI YANGU

Good Call!!!!!!!!!!!
 
Nshaumiza sana, kabla yapo nilitendwa mimi nikajifunza kutenda wengine!
 
BIG UP MAJOKI tena huu undugu tunaoutengeneza ukubwani tunataka uwe una nguvu kama undugu wa damu shida sana ooh swetie,ooh honey ooh darling
 
Pole sana Da Pretty. Duh! Manake bora hiyo mara ya mwanzo "unaweza kuamini" kuwa hawakubanjuana (sio kufanya lolote, kwani huko kulala pamoja uchi hakutoshi kuwa ndio kufanya?), lakini hili la pili huyu kaka anaongopa mchanaaaaaa, na kama angekuwa kama Pinocho basi pua angekuwa analiburura.
 
Inasemekana kuwa katika Mapenzi na Vita, chochote kinafaa, zikiwemo mbinu safi na chafu, na wala sio kama tunavyotaka iwe kuyaona Mapenzi kama barabara iliyopambwa kwa mawaridi. Hii ni kwa sababu kwanza, kama ambavyo kuna mapenzi, vilevile kuna chuki/kutoendelea kupenda, pili kama ambavyo huzaliwa, vilevile yanakufa; na linapotokea moja katika haya manake "hakuna mapenzi tena" na kubali matokeo.

Labda tunachoweza kuwalaumu ma-ex wetu ni kutokuwa wawazi. Ikiwa kaamua kurejesha majeshi, ni sawa tu lakini sio tena anaanza visa na vyengine vya kuudhi sana. Wengine hawachukui hio. Mimi binafsi, kama ingekuwa kila baada ya kuumizwa unabakia na chale usoni, wangu ungekuwa kama sanamu ya kimakonde. Lakini kila ikitokezea, "ninajipangusa michanga, ninaweka sawa magwanda/kombati" safari inaendelea, ninaishi, na sio kukaa tu ninalalamika nilivyotendwa. Sifikiri kama nimewahi kumtenda mtu, kwani daima nimekuwa muwazi na mkweli. Sera yangu "bora nikuumize kwa ukweli kuliko kukufariji kwa uongo".
 
Kuumizwa bado....bahati mbaya nimeshaumiza mara mbili!!
 
ACHA TU,Hayajakufika mshukuru Mungu

Experiance kutokana na matukio yanayowapata watu inaweza kuwa njia moja ya kujifunza. Lkn experiance unayoipata kutokana na yaliyokukuta ww mwenyewe ni nzuri zaidi coz unaweza kujua furaha, karaha, maumivu, misukosuko na mengine mengi. Hivyo kurudia kuingia ktk matazo na mateso ZAIDI KWA MARA NYENGINE ni uzembe.
Na kwa kuwa ushahidi uliopo miongoni
mwetu unaonesha kuwa mapenzi si kitu
cha kudumu kwa miaka mingi, hivyo anayesema anaweza kupenda
jambo moja milele kwa kiwango kilekile ni mtu anayejiwekea mtengo
utakaomnasa mwenyewe na
kumtesa.
Na kwanini ujiwekee possibility ya
kudumisha mapenzi yako
kwa watu/kitu ilhali uliyo/ulivyovipenda
udogoni sivyo
unavyovipenda saivi?

"Mungu niepushe na maumivu hasa ya mapenzi, moyo wangu hauhimili"
 
Kuumizwa bado....bahati mbaya nimeshaumiza mara mbili!!

tofautisha baina ya kuumiza na kuacha.
Wengine masononeko ni kama maigizo tu ya
kutaka kukurudisha ili
muwe pamoja kwa mara
nyengine. Lkn mtu kuumia
huwa anajuwa mwenyewe.
 
Nshaumiza sana, kabla yapo nilitendwa mimi nikajifunza kutenda wengine!

Kwa hiyo ulikuwa ualipiza kisasi? kama ndivyo wewe si mtu mzuri tena badilika haraka kwani haipendezi kwa waungwana, jifunze kusamehe na kuwaonea wenzako huruma hata kama ulishawa kuumizwa
 
Nshaumiza sana, kabla yapo nilitendwa mimi nikajifunza kutenda wengine!
Mwombe Mungu akuondolee hiyo roho chafu, usilipize mtu asiyehusika, ni kweli kutendwa inauma bt sina hakika kama kulipiza inaondoa maumivu. Bora kujiweka pembeni kuliko hivyo unavyofanya. Muheshimu sana mtu akikupa moyo wake cz anajua ndio kapata kumbe wewe moyoni unawaza tofauti! Badilika ndugu yangu. Mungu akutangulie.
 
mapenz sio ya kuyaendekeza sana yatakugeuza chizi...just relax and enjoy life,when u met a snitch just quit early

'MIMI NINA MSEMO WANGU AMBAO SIKUZOTE UNATEMBEA KICHWANI...KWAMBA SIKUZALIWA NA MTU NA WALA HAKUNA ALIYEUMBWA KWA AJILI YANGU

Mkuu umenena ukweli kabisa.
Kuendekeza kuwa heartbroken ni kujitakia tu only watu wenye udhaifu ndio wenye kuendekeza huo ujinga. Penda, ukitoswa hey, move on. Don't be weak!!
 
hii kitu ni noma, tunaumizwa moyo na hatuachi kupenda tena.

nimeumizwa mara moja lakini maumivu yake usipime!nikajua ndiio mwisho wa dunia!
faraja ni alipoondoka tu maisha yangu yakawa super ile mbaya hadi sasa nikimkumbuka tu namshukuru mungu kuondoa lile gundu!
 
Back
Top Bottom