Jesusfreak08
JF-Expert Member
- Jul 20, 2019
- 822
- 1,803
Habari zenu wapendwa natumai mnaendelea vizuri na mimi pia sijambo
Kwasababu kilimo pia ni sayansi basi hata mambo yanayofanywa kwenye kilimo huzingatia sana mambo pia yakisayansi
Kupalilia ni sehemu muhimu sana katika kusaidia mazao yako kukua na kama usipo inzingatia hii stage basi na kuhakikishia unaweza ukapelekea hata mazao yako kufa.
Sasa kuna umuhimu wa kufanya palizi pale mazao yako yanapokuwa madogo kwasababu ni kipindi ambacho mazao yanakuwa hajakua mizizi kwa kiwango ambacho ni kikubwa kwahiyo hata madini mmea unayohitaji yakiwa mbali basi sio rahisi kufanikiwa kuyapata na inaeweza kupelekea kifo cha mmea/zao lako.
Tunapongelea palizi namaanisha ni kuondoa mimea yote isiyohitajika wakati wa uukuaji wa mazao yako kwenye shamba lako sasa.
Lakini magugu na majani(mimea) isiyo hitajika inahitaji madini yale yale ambayo pia mazao yako madogo yanahitaji yanaweza kutokea mambo mawili jambo la kwanza ni kuchukua madini yote au kunyang'anyana kwa madini kati ya mazao na magugu & majani
Je, kwanini uondoe?
●Ili kuhakikisha upatikani rahisi wa madini kwa mmea husika
●Ili kuondoa ushindani wa kutumia hayo madini kati ya mmea na magugu
●Kuondoa vizuizi vya mwanga wajua kwasababu magugu yanaweza kukua zaidi ya mazao
● Kuupa mmea eneo ya wenyewe kukua vizuri.
Kwaiyo palizi ni muhimu sana kwenye shamba lako usipofanya hivyo unaweza kupelekea hata shamba mimea yako kufa na baadae mavuno machache.