Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Pranks si vitu vigeni. Tumefanya toka utotoni. Social media ni zimezifanya ziwe maarufu sana. Mimi ilikuwa hii.
Tulikuwa na jamaa yangu tumetoka chuo Muhimbili tunaelekea Mabibo hostel. Ndiyo tunaanza shule. Tunatembea hadi mtaa wa Congo kuchukua gari za kutoka Mnazi Mmoja.
Sasa kufika jengo la soko la Kariakoo kulikuwaga na wazee machinga wengi wanauza suruali za mtumba. Jamaa akataka suruali lakini wakajaa wengi sana kumzunguka. Ghafla akaanza kuongea kiingereza. Jamaa wakaanza kubabaika. Wananiuliza jamaa anavyosema mimi nawatafsiria.
Nikawaambia jamaa ni Mzambia. Basi wanataja bei kubwa, mimi namtafsiria jamaa. Jamaa anajidai, "Too expensive, too expensive." Wazee walihangaika sana wale.😀😀