SIMULIZI hii ni ya ukweli, ukizani uongo basi shauri yako; hususani wewe mwanaume mwenzangu upendae kujikweza mbele ya vidosho!!
In short ni kwamba, siku hizi nimechoka mbaya lakini enzi zile ilikuwa ni TOO MUCH!! Basi kipindi kile cha msoto wa kutisha, nikabahatika kukutana na msichana mmoja..
mzuri wa haja; mama Mnyamwezi, baba Masalia ya Waarabu! Hebu pata picha, huyo kinda linalotoka hapo litakuwaje!! Hata hivyo, yule shori hakuwa mwenyeji sana hapa Dar
ni product ya Nzega, Tabora!
Basi bwana, tukaachiana contacts! Ikawa mara kwa mara tunawasiliana hadi penzi likachanua na kukomaa!!
Siku moja, nikiwa sina hili wala lile; binti wa watu akaenda hewani! Bila kutarajia, akaniambia anataka kuja ghetto! Kucheki saa, nikakuta inakaribia saa 11.30 jioni! NIKASHANGAA! Nikashangaa kwavile aliniambia anaishi Pugu wakati mimi naishi Temeke! Nikajiuliza, mida yenyewe ni jioni kabisa inayokaribia machweo
na Pugu na Temeke ni mbali ile mbaya! Nikajiuliza kwao atarudi saa ngapi! Nilipomuuliza atarudi saa ngapi wakati mida imeenda sana, akajibu anakuja kulala kwangu!
Liudenda likanimwagika, na kijasho chembamba nacho kikanitiririka kidume cha watu! Nilipoingia mfukoni, nikajikuta nina buku unusu (TZS 1,500/=) pekee! Kwa mida ile, nisingeweza kufanya makaratee yoyote! Nilipoenda kwenye friji, nikakuta kumbe maharage yangu niliyopika mchana bado yapo! Kucheki kwenye kindoo change, nikakuta kuna mchele wa kutosha! Nikajua hapa anasa hamna lakini kulala njaa vile vile hakupo!
Kuona hivyo, nikaenda hewani, ile binti kupokea nikampa full data..!! Nikamwambia wazi, kwamba hapa nipo alosto ile mbaya kwahiyo kama ana mpango wa kuja akae akijua nini atakutana nacho! Nikamwambia wazi kwamba nilikuwa na buku unusu tu ambayo ndo bajeti yangu ya siku inayofuata!
Sina hakika kama alizani natania au vipi! Akajibu kwa kujiamini, kwamba POA TU! Kama masihara vile, binti akapanda daladala na akaniambia nimfuate TAZARA. Hivyo basi, ile kufika TAZARA tu, nikajikuta nimeshatumia TZS 300/- na hivyo kubakiwa na TZS 1,200/=! Muda kidogo, binti akafika! Kwa sababu ninazozijua mwenyewe, nikakata shauri la kupanda magari ya kwenda Posta badala ya kuchukua ya moja kwa moja! Ile kufika Posta, kidume nikajikuta nimebakiwa na TZS 600/- tu! Toka posta, tukachukua daladala za TMK
ile kufika ghetto, sina hata thumuni
.!!!
Kilichomtoa kwao, akakipata!
Siku ya pili akabaki ghetto hadi mchana! Ile anajiandaa kuondoka, nikajikooza na kujiweka sawa!! Huku nikiwa na macho makavu, nikamwambia:
Dont forget ile jana nilikuambia nilikuwa na 1,500/- tu ambayo ilikuwa ndo bajeti yangu ya leo! Hata hivyo, hivyo, ela yote iliishia kwenye nauli na hapa sina hata senti tano!
Kwahiyo? Binti wa watu akaniuliza!
inabidi uniache angalau na buku!
Bibti yule alicheka hadi basi
kasha akazama kwenye kipochi chake na kuniacha na gwala (5,000/=)! Kidume nikaua ndege wawili kwa kajiwe kamoja!!
Nilizani binti yule asingekuja tena; kumbe wapi!!
MWANAUME MWENZANGU vipi, yashawahi kukuta haya?! Kama hapana, je kama yangekukuta katika situation ambayo nilikuwa nayo ungefanya nini?! Ungeenda kukopa au ungejifanya umesafiri?! Au ungejifanya leo ghetto kuna mgeni kwahiyo aje siku nyingine?! Au na wewe ungeyafanya haya niliyofanya mimi?! Usisahau, hiyo ilikuwa ndo mara yetu ya kwanza kukutana faragha!
NAWE mdada, ungekuwa ndie wewe
.nikakupa ukweli huo, ungekuja tu ghetto au ndo ungekuwa mwisho wa mchezo?!